IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

IGP Sirro jana umetoa kauli nzito na ngumu mno kutolewa na kiongozi wa aina yako na mtu mwenye umri mkubwa kama wewe na mtu anayeheshimika kwa cheo chake kama wewe.

Angalia sana ulimi wako jinsi unenavyo, muombe sana Mungu akupe hekima ili kabla ya kutamka neno lolote hekima ikutangulie.

Jana ulitamka maneno haya nami nakunukuu.
" Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?".
Mwisho wa kunukuu.

IGP Sirro, hakuna mzazi anayepanga azae mtoto wa aina gani, Binadamu tunazaa mwili hatuzai Roho.
Kuna kijana anasumbua sana mitaani, anajitapa kwamba hakuna wa kumfanya lolote kwa sababu Baba yake ana cheo kikubwa mno serikarini, kijana huyo huvuta unga na kwenda hadi kwenye Hotel ya Baba yake iliyoko Chanika ambako hufanya vituko vya ajabu,ukiwemo kupiga watu.

Je?! unajua huyo mtoto ni wa nani? Tafadhali sana, wazazi wa Hamza hawakujua kama wanazaa mtoto wa aina gani, hata wazazi wako wewe Sirro hawakujua kama ipo siku utakuja kuwa IGP.

JITOKEZE UIOMBE MSAMAHA FAMILIA YA HAMZA ILI ULINDE HESHIMA YAKO.
Wajiulize wao kwanza,haya maaskali yanayo bambikia watu kesi yalizaliwa na nani?
Viongozi wa nchi hii,badala ya kutumia akili/ubongo kufikiri sasa yanatumia makamasi na makalio kufikiri.
 
Vipi kuhusu huyu wa chanika? Ambaye ni mtoto wa inspector general na bado anapulizia watu bangi usoni? Baba yake ndiye alimfundisha hivyo?

Kwani aliyoongea kwa hamza hakusema kwambq yanamhusu hamza peke yake.....?
Yanahusu malezi ya kila mzazi kwa watoto
 
IGP Sirro jana umetoa kauli nzito na ngumu mno kutolewa na kiongozi wa aina yako na mtu mwenye umri mkubwa kama wewe na mtu anayeheshimika kwa cheo chake kama wewe.

Angalia sana ulimi wako jinsi unenavyo, muombe sana Mungu akupe hekima ili kabla ya kutamka neno lolote hekima ikutangulie.

Jana ulitamka maneno haya nami nakunukuu.
" Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?".
Mwisho wa kunukuu.

IGP Sirro, hakuna mzazi anayepanga azae mtoto wa aina gani, Binadamu tunazaa mwili hatuzai Roho.
Kuna kijana anasumbua sana mitaani, anajitapa kwamba hakuna wa kumfanya lolote kwa sababu Baba yake ana cheo kikubwa mno serikarini, kijana huyo huvuta unga na kwenda hadi kwenye Hotel ya Baba yake iliyoko Chanika ambako hufanya vituko vya ajabu,ukiwemo kupiga watu.

Je?! unajua huyo mtoto ni wa nani? Tafadhali sana, wazazi wa Hamza hawakujua kama wanazaa mtoto wa aina gani, hata wazazi wako wewe Sirro hawakujua kama ipo siku utakuja kuwa IGP.

JITOKEZE UIOMBE MSAMAHA FAMILIA YA HAMZA ILI ULINDE HESHIMA YAKO.
Akimaliza kuomba msamaha kwa wazazi wa Hamza awaombe msamaha na Watanzania
 
Hamza angekuwa na mama yake nae ana bunduki pale Salenda angestahili dharau hizi lakini maskini hata yeye atakuwa amejua kupitia vyombo vya habari kama Sisi. Sirro angekuwa umewahi kubeba mimba hata wiki moja usingeharisha huo utumbo wake.

Wewe umesikia maelezo ya awali yalotolewa na nduguze?

Ulimsikia IGP akisema kama nduguze wangechukua hatua ya tahadhari mapema uovu usingeweza kufanyika wa kuua watu huyo Gaidi?!
 
Acheni kuwatoa watu kwenye mstari wa kujadili Ugaidi kwa kumnyooshea kidore IGP.

Msomali asingefanya ule Ugaidi IGP asingeyasema hayo na ameyasema kwa uchungu mkubwa kitendo kile cha kuua wale watu kinauma sana!
 
Wekeni picha ya hilo litoto lake hapa. Kumbe naye ana kimeo halafu anatukana wazazi wengine?
Huwa wanakuwa na akili za punda hao.Mwingine aliita watoto wa watu vilaza.Mara hataki wanafunzi waliopata watoto waendelee na masomo.Tafrani tupu.Saa hizi anapiga soga na mashetani wenzie tu huko kuzimu.😝😝😝😝😝
 
Halafu anaitwa wa wenzake vilaza kumbe na binti lake nalo zilikuwa hazimo!
 
Back
Top Bottom