Uchaguzi 2020 IGP Sirro: Kuna baadhi ya vyama wana ajenda ya kufanya vurugu ili uchaguzi usifanyike

Uchaguzi 2020 IGP Sirro: Kuna baadhi ya vyama wana ajenda ya kufanya vurugu ili uchaguzi usifanyike

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema ana uhakika Uchaguzi Mkuu utafanyka kwa amani na utulivu, japo kuna baadhi ya vyama wanataka kuwa na vurugu ili uchaguzi usifanyike.

Amesema Jeshi la polisi limejipanga vizuri na ndio maana wanayakamata makundi ambayo yanakuwa yamepangwa kutekeleza uhalifu. Pia amesema majina ya watu wanataka kufanya fujo wanayo hivyo wanawakamata.

Amesema wanataarifa kuwa kuna watu wanaandaliwa kutoka Kenya ili kuja kufanya fujo wakati wa uchaguzi. Hivyo ameongea na viongozi wa siasa ili wazungumze kuhusu mambo haya waliyotaarifiwa.

IGP Sirro amesema wanaona maeneo ya Tarime kuna shida hivyo watatuma Polisi wakutosha watakaovaa kiraia ili kuhakikisha amani.
 
Siro Ni aibu mtu uliyeheahimika kupakwa matope namna hii na ccm. Hivi fujo Askari wako wanazofanya huoniiii? Uvccm chini ya usimamizi wa polisi wako huoni wanachofanyaaaaa? Inatia hasira vby Sana.
 
Juzi Chato wale ni kina nani walioleta vurugu...ccm imeshaanza mkakati wa kubaki kwa kutumia Dollar??
 
Huu ni utopolo wa hali ya juu,jana tumeyaona waliofanya polis zidi ya esta matiko,ila haongelei hilo,kisa ni watu wake?!tunayoyaona kwa macho yanatisha sana, jana lissu kanyimwa kivuko ili asiende tena ukerewe, tumechoshwa.
 
Kuna maajabu duniani mjue!

yaani mtu mwenye dhamana kubwa anaongea ongea ujinga mbele ya dunia!

Hana aibu, hajui au amesahau kama wanaomfahamu wanamshangaa!

Ndugu na rafiki zake wanabaki na maswali juu yake kwa ajiri ya matamshi ya hulinda hila
Za watawala, siku kikinuka wanaomfahamu ndo wanakuwa Hatari kwake!
 
Si aseme ni vyama gani tu.

Aseme na atupe uthibitisho ili na wao wakane au lah.

Then tubaki na jukumu la kuilinda amani
 
Sirro nae bwana sijui amekula maharage ya wapi yaani IGP Mzima hujui AMANI inaletwa na nn sasa kama IGP hajui kwamba AMANI NI TUNDA LA HAKI police wake watajua kweli.

ALUTACONTINUA.
 
..video hii ni nzuri zaidi kuhusu mikutano ya IGP mkoani Mara.

..sikiliza toka dakika 12:00 ambapo wagombea ubunge wa CCM na wa CDM wamezungumza.

 
Kamanda Sirro naona dhamira yake inakataa kutekeleza alichoagizwa cha kuhakikisha ccm inatangazwa washindi kwa lazima. Sasa anaanza kutengeneza vitisho kwa watu waogope kulinda ushindi wao.

Sirro sio lazima uwe IGP kwa kumwaga damu za watu, ccm haina uwezo tena wa kutawala nchi hii kwa ushindi wa zaidi ya 50%.
 
Akili ndogo imapojaribu kuiongoza Akili kubwa, wewe IGP Taarifa unazopewa ni za kitoto ndio maana mnakamata Wafuasi wa Vyama vya Upinzani. Kule Chato wahuni wa CCM walifanya vurugu mchana kweupe kwenye mkutano wa Tundu Lissu na polisi walikuwa wanajifanya hawaoni, Amani gani hiyo unayosema unataka kuilinda?

Ujitafakari, hivyo viatu sio saizi yako, Ungejiuzuru ulinde heshima yako
 
Siro naye kaamua kujiingiza kwenye uchafu wa ccm
 
Back
Top Bottom