IGP Sirro: Ni aibu sana kuruhusu jambazi kutawala nchi yetu

IGP Sirro: Ni aibu sana kuruhusu jambazi kutawala nchi yetu


My Take 1
Sirro anapenda sana kuita-ita neno gaidi. Naona anarahisisha sana mziki wa magaidi.

My Take 2
Sirro kama hawezi kuondoka mwenyewe aondolewe kwa nguvu. Kashfa ya askari wake kufanya ujambazi haisafishiki

======

Kamanda Sirro: Ni viongozi ambao tunawategemea kwenda kuwasaidia watanzania na hasa kwenye masuala mazima ya makosa haya ya kutumia silaha na hasa makosa haya ya kutumia nguvu.

Huwa nawaambia siku zote, sisi tunafanya mafunzo ya promotion lakini mafunzo mengine ya utayari. Ni aibu sana kuruhusu jambazi kutawala nchi yetu.

Wanasema ni aibu sana gaidi kutawala nchi yetu, kwahiyo mheshimiwa waziri kwa kifupi ni kwamba tuko vizuri sana na nipeleke kwa ambao ni wachache bado wana tabu ile, nishawaambia kwamba biashara ya unyang'anyi kwa kutumia silaha, nguvu ilishapitwa na wakati.
Nadhani hapa Sirro anataka kuwahamisha watz na kuwatoa kwenye kashfa za Jeshi la polisi za kuua ua watu na maonezi yaliyokithili yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini.
Siyo siri kwa hali ilivyo sasa hivi gaidi wa kwanza nchini kwetu ni polisi wenyewe. Tumeshindwa kujenga taifa lililostaarabika/ linaloendelea kustaarabika kutokana na polisi wetu kushindwa kufanya kazi kwa weledi na pia kushindwa kulinda viapo vyao. Watz sasa hivi tumekuwa kama wanyamapori, huwezi jua kipi ni haki,/ halali na kipi ni haramu au kosa.
Ni kosa kubwa sana kwa kiongozi mkubwa wa kiwango kama cha kwake kushindwa kuheshimu na kulinda katiba, sheria na miongozo mbalimbali na kufikiri kwamba nchi inaweza kuongozwa kwa matamko kama anavyofikiri.
Hii pia inatokana na jeshi letu kuwa walinzi wa haramu na ndiyo maana na wao hawaoni shida kuishi katika mfumo huo.
 
nadhani kwasababu sirini yupo affiliated na chama fulani cha siasa ambacho kimeshika dola na yeye kulinda maslahi ya chama chake ni kutoa kauli kama Hizo.
 
Back
Top Bottom