IGP Sirro: Ni aibu sana kuruhusu jambazi kutawala nchi yetu

Nadhani hapa Sirro anataka kuwahamisha watz na kuwatoa kwenye kashfa za Jeshi la polisi za kuua ua watu na maonezi yaliyokithili yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini.
Siyo siri kwa hali ilivyo sasa hivi gaidi wa kwanza nchini kwetu ni polisi wenyewe. Tumeshindwa kujenga taifa lililostaarabika/ linaloendelea kustaarabika kutokana na polisi wetu kushindwa kufanya kazi kwa weledi na pia kushindwa kulinda viapo vyao. Watz sasa hivi tumekuwa kama wanyamapori, huwezi jua kipi ni haki,/ halali na kipi ni haramu au kosa.
Ni kosa kubwa sana kwa kiongozi mkubwa wa kiwango kama cha kwake kushindwa kuheshimu na kulinda katiba, sheria na miongozo mbalimbali na kufikiri kwamba nchi inaweza kuongozwa kwa matamko kama anavyofikiri.
Hii pia inatokana na jeshi letu kuwa walinzi wa haramu na ndiyo maana na wao hawaoni shida kuishi katika mfumo huo.
 
nadhani kwasababu sirini yupo affiliated na chama fulani cha siasa ambacho kimeshika dola na yeye kulinda maslahi ya chama chake ni kutoa kauli kama Hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…