IGP Sirro: Wale wachache wanaotaka nchi isitawalike kwasababu ya kukosa madaraka hatutawapa nafasi

Huyu Sirro kavunja sana haki za binadamu.
Ni mfungwa mtarajiwa , chini yake watu wengi wamekosa haki ya kuishi.
 
Mfano mzuri ni kesi ya Mbowe, watu walifika mahakamani kila kesi ilipotajwa hakuna hata siku moja kulitokea vurugu. Polisi hawakuvuruga! kwa maneno mengine

Kinachonishangaza ni Sirro kutishiwa na Wapinzani ambao hakuna ushahidi wowote wa vurugu.
Sirro hajakerwa na mauaji ya watu hadi VP Mpango kutoa tamko
Hakuwahi kukerwa na maiti za baharini au mitoni
Haakuwahi kukerwa na Raia kupotea na Familia zikibaki na machungu

Sirro alimwacha yule afande aliyesema '' CCM itashinda kule Hai' au yule aliyesema CCM oyee kule Mara na wale kwenye kongamano la Pole pole. Leo anatuambia wao ni 'law emforcers'

Jana Mh Rais kasema kule Dodoma, Polisi waache kufungua kesi zisizo na ushindi. Kwa maneno mengi waache kufanya mambo bila weledi ili kupunguza mahusubu.

Pamoja na yote, Mzee Sirro ni jasiri kwakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…