DOKEZO IGP tuokoe na wizi ulioibuka Arusha unatisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sio kimandolu tu,Lemala,daraja mbili na Uzunguni bara bara ya blue stone,kwa week mbili mfululizo wameuawa watu watatu kwa kuchomwa visu na tatu mzuka,bara bara za uzunguni uporaji hufanyika mchana,Sijaona jitihada kuwadhibiti,Mbaya zaidi wameanza kugusa wageni.
Jitihada za royal tua zinarudishwa nyuma.
 
Kuwa makini tu mkuu, pale picnic, xo, Africana nk Kuna wajomba ni wazee wa kuchora ramani sana na ukijichanganya unaweza pigwa tukio ukiondoka kwani unaondoka na unafuatiliwa vizuri tu .
Basi Arusha imeshakuwa tatizo. Ila Arusha kuna ushkaji sana wa polisi na hawa wahalifu. Miaka ya 2012 nilikuwa naonaga maafisa wa hili jeshi wakipiga bia na watu wanaosemwa kwa uhalifu pale Anless bar kona ya kwenda Ilboru. Nadhani wakati wa Magu hawakuwa wakionekana
 
Kuna tofauti kati ya Panya road na hawa wezi wa Arusha. Panya road ni watoto ambao wanaishi mitaani na wanafahamika kabisa ila kwa upumbavu wa watu wa Dar wanafichiana siri. Utakuta kitoto cha miaka 13 kinasumbua mtaa mzima halafu watu wazima wa mtaani kwao wanamtazama tu. Hao wa Arusha wengi wao kuwafahamu ni hadi upelelezi.
Mkuu wezi wanaishi mtaani na wanafahamika. Inakuwa kama we humfahamu mzazi au rafiki yake anamfahamu. Tuwafichue la sivyo tunazid umizwa pia jamaa zetu
 
Kumeibuka wizi mkoa wa Arusha unaotishia usalama wa wananchi wa kawaida na wafanyabiashara mbalimbali kuvamiwa na kuibiwa either kwa ujambazi wa kutumia pikipiki (tatu mzuka) ama kuibiwa manyumbani na wezi wa kawaida.

Wezi wa pikipiki ama tatu mzuka wamekuwa wakiwaibia watu kwa nguvu huku wakiwadhuru kwa kuwachoma visu ama spoko za baiskeli hata mchana kabisa, huku wakiwanyanganya vitu walivyobeba huku wananchi wa kawaida wakiogopa kuingilia kwa kuhofia maisha Yao.

Hawa wameua watu wengi sana wanojaribu kupambana nao ili kuzuia wizi.

Wezi wa pili ni wezi wa nyumbani na kuvamia sehemu za biashara. Hapa ndio watu wengi wanapoumizi watu zaidi .

Mfano.... Kata ya kimandolu imekumbwa na wezi wanaoiba kila nyumba na sehemu za biashara . Yaaani imekuwa kama imehalalishwa watu kuibiwa nyumba kwa nyumba na sehemu za biashara kila siku bila jeshi la polisi kuchukua hatua zozote za kuzuia wizi huo huku wakijua wahusika wa matukio yote ya wizi .

Mfano kwa kimandolu wanajua kuwa kuna kijana anaitwa ADAM ambaye amekuwa ni mwizi mkuu na ndiye anaye organize wizi wote unaotokea kimandolu. Mwezi watano mwaka Jana kama sijakosea kijana huyo alikamatwa akiwa amekodisha nyumba zaidi ya mbili zikiwa kama warehouse zake za kuifadhi vitu vyake anavyoibia wananchi.

Mwaka jana mwezi wa tano ama wa sita alikamatwa na laptop zaidi ya 30, pikipiki zaidi ya tano , generators zaidi ya kumi , tv haziesabiki na accessories kibao ila akaachiwa kutokana na polisi wasio waaminifu kutoa taarifa za whisle blowers waotoa taarifa. Hivyo wananchi waaogopa kwenda toa ushahidi mahakamani utakoweza kumtia hatiani kwa kuogopa kuja kuuliwa na mtuhumiwa.

Kinachotokea polisi wa doria na baadhi ya polisi central wanakuwa sehemu ya huu ujambazi unaotokea kila siku.

Huyu kijana na washirika wake wamekuwa tishio kwa Kimandolu na sehemu za karibu kwa sababu amekuwa na watu wake ndani ya Jeshi la polisi wanaompa taaarifa.

Chondechonde IGP tunaomba uingilie Kati wizi huu unaotusumbua mjini Arusha . Huyu kijana yupo well trained kiasi cha kwamba ana uwezo wa ku bypass camera na ana mavazi ya kujikinga na camera kutokana na polisi ambao wasio wema wamemtaarifu namna ya kujikinga ili asionekane kwenye camera sehemu mbalimbali anazokwenda kuiba.

Tunaomba IGP na viongozi waandamizi waaingilie kati kuingilia hili tatizo kwa mkoa wa Arusha maaana wananchi tumechoka
 
Tunaomba IGP na viongozi waandamizi waaingilie kati kuingilia hili tatizo kwa mkoa wa Arusha maaana wananchi tumechoka .
...mida kama hii wakulungwa ndio huwa tunatafuta chumba cha kupanga sifa nyumba isiwe na fence na dirisha liwe la wavu tu NO ALUMINIUM maeneo ya Kimandolu ili tuoneshane ushababi dadeki, yani kidume anatamba vidume wa Chuga mnafyata mnaogopa bisbis na spoke za baiskeli???
 
Mwanao ukimkosa mahabusu nenda kamtafute hospitalini ~~~~ Amos Makalla (mkuu wa mkoa Dar)

Baada ya hii kauli iliyopingwa na chadema, panya road wakaisha mitaani.
Inatakiwa kauli kali kama hii!! Uliwachekea hawa watu utavuna majambazi ya hatari
 
IS THIS COUNTRY HAS A LEADER? AU KUNA MWAKILISHI WA KIONGOZI...KILA MTU ANAFANYA ANACHOTAKA...HAKUNA WA KUMZUIA...MADHALI HAGUSI MASLAHI YA HAO WANAOITWA VIONGOZI...NYIE WENGINE PAMBANENI NA HALI ZENU...

WEWE FIKIRIE YULE PGI TOKA ATEULIWE MAUAJI NA JINAI ZIMEKITHIRI...RUSHWA NDIO USISEME NA DHULMA...ALAFU NOBODY CARES.
 
Hakuna kitu chenye thamani duniani kama uhai wa mtu. Kuanzua mimba ya mwanafamu inapotungwa hadi kufikia kuzaliwa na kuwa mtu mzima na mwenye afya ni gharama kubwa za fedha na muda zimetumika, hivyo basi mtu huyo kuja kuuwawa kirahisi rahisi tena kwa ajili ya mali yake ni jambo la kusikitisha sana na linaumiza sana.

Kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia pamoja na mali zao, ila maeneo mengi usalama umezorota. Ushauri wangu kwa kamati za ulizi na usalama za mkoa wilaya, tarafa na kata na kijiji tuwatumie migambo kulinda raia usku na mchana naamini kama hawa mgambo watapatiwa posho kidogo tunaweza tukaanza kulala milango wazi binafsi na imani kubwa sana na jeshi la mgambo hivyo sio mbaya wakawasaidia polisi maana jeshi letu la polisi linamajukumu mengi sana.
 
Usiku wa kuamkia ijumaa wametuibia.
Wamekata bati wakaingia.Kuna frame nne zimeungana kila moja wameingia mbili tu ndio zimepona mana hawakuona cha kubeba ila hizi nyingine mbili wameiba.Na hawajachukua vitu vya kubebeka walichokua wanabeba ni voucher na hela tu.
Wanaturudisha nyuma sana.
Tukio limetokea maeneo gani ?
 
...mida kama hii wakulungwa ndio huwa tunatafuta chumba cha kupanga sifa nyumba isiwe na fence na dirisha liwe la wavu tu NO ALUMINIUM maeneo ya Kimandolu ili tuoneshane ushababi dadeki, yani kidume anatamba vidume wa Chuga mnafyata mnaogopa bisbis na spoke za baiskeli???
Arusha matukio ya ukibaka ni ya hao tatu mzuka ila wakija majambarika mzee wanakuja na muzburg (mjegeje/bunduki) wanakichafua mapema sana asubuhi saa nne wanaiba mahali popote na roho ya mtu inatoka kama akileta uduanzi.
 
Sio kimandolu tu,Lemala,daraja mbili na Uzunguni bara bara ya blue stone,kwa week mbili mfululizo wameuawa watu watatu kwa kuchomwa visu na tatu mzuka,bara bara za uzunguni uporaji hufanyika mchana,Sijaona jitihada kuwadhibiti,Mbaya zaidi wameanza kugusa wageni.
I
...mida kama hii wakulungwa ndio huwa tunatafuta chumba cha kupanga sifa nyumba isiwe na fence na dirisha liwe la wavu tu NO ALUMINIUM maeneo ya Kimandolu ili tuoneshane ushababi dadeki, yani kidume anatamba vidume wa Chuga mnafyata mnaogopa bisbis na spoke za baiskeli???
hao siku wanishobokee na mtalimbo wangu ntatangazwa kwenye vyombo vya habari ntamshanawena Mtoto wa mtu ndo akili ziwakae sawa!!!!
 
Arusha ipi unayokaa wewe ? Matukio haya ya ujambazi yamekifthiri kila mahali . Watu wamepoteza ndugu zao pamoja na wengine kujeruhiwa alafu unakuja kuongea mashudu humu ndani . Kama hujapata athari ya haya yanayoendelea ni bora ukakaa kimya mzee
Ukute ndio Adam mwenyewe huyo anapima upepo.

Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
 
Usiku wa kuamkia ijumaa wametuibia.
Wamekata bati wakaingia.Kuna frame nne zimeungana kila moja wameingia mbili tu ndio zimepona mana hawakuona cha kubeba ila hizi nyingine mbili wameiba.Na hawajachukua vitu vya kubebeka walichokua wanabeba ni voucher na hela tu.
Wanaturudisha nyuma sana.
Unaachaje vocha na hela dukani?
 
Back
Top Bottom