IGP Wambura awaonya vikali wanaotaka kuandamana, asema huo ni uhaini akitaka "Wakome" na Wasitishe matamshi yao ya Kichochezi...

Pamoja na wizi wa kura wa CCM ,CHADEMA Ilikuwa na wapiga kura milioni 6 uchaguzi wa 2015.Uchaguzi wa 2020 Jiwe akaona isiwe tabu akaweka mpira kwapani.Huyo Wambuya anajua nguvu iliyopo nyuma ya upinzani kwa wingi wao.vinginevyo asingeanza mikwara bubu yake!
Ccm inao mil.13
 
DP world ya Waarabu wa Dubai inazidi kufanya maji yakorogeke.
 
Watanzania sio watu wa kuandamana, ila mtu anaweza kumezeshwa polonium akatulia zake na kwenda kwa Allah taratibu bila haraka.
Tanzania Hatuna polonium tena Putin kashaitumia yote tangu vita ianze kwa hiyo chukua nyongo ya mamba na sio kila mtu atakufa kwa hiyo kwani wengine ni sugu
 
Amani maana yake nini?
Amani ya Tanzania ni ile ya wananchi kuwa wanyonge kufanyiwa chochote na serikali yao kama vile kuuwawa kutekwa kubakwa kubabizikiwa kesi kulawitiwa kunyanyanganywa mali zao watoto wao pesa zao na kulipa kodi kandamizi na kutawaliwa na viongozi na watoto wao na mahawara zao yote hiyo ni mfumo wa amani na utulivu katika jamii ya Tanzania.Usipokubali hayo wewe sio mzalendo kawe mkimbizi au andamana uone cha mtema kuni
 
Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo za Maandamano.

=====

IGP Wambura acharuka, asema kuna watu wanataka kuiangusha Serikali, “wasitikise kiberiti”

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amesema kuna kundi la watu ambao wamepanga kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – awamu ya sita kabla ya mwaka 2025.

Amesema watu hao ambao wamefanya kosa la uhaini, wanahusisha maandamano hayo na kushawishi watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za kuhusu mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Agosti 2023 jijini Dar es salaam, IGP Wambura amesema aliamini hoja za bandari hujibiwa kwa hoja.

Pia amesema aliamini kwa vile baadhi ya watu hao walienda mahakamani wangeheshimu mahakama lakini badala yake wametoka na kuanza kutafuta ushawishi na kuchochea kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima.

“Lakini mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanangusha serikali ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kabla ya mwaka 2025. Huu ni uhaini,” amesisitiza.

IGP Wambura amewaonya watu hao kwamba wakome na wasitishe matamshi yao hayo ya kichochezi lakini pili amesema watachukuliwa hatua za kisheria kutokana na uchochezi wanaoufanya na uhaini wanaoupanga kwani vyote ni makosa ya jinai.

Amesema Jeshi la polisi halitakaa kimya na kuwavumilia, kama walidhani lipo kimya litaenda kuwaonesha kuwa halipo kimya kwa yeyote atakayevunja sheria za nchi.
“Pili niwaombe watanzania wawapuuze watu hawa, Tanzania ni nchi ya amani ni nchi salama hawa wasitake kushawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko, hatujawahi kufika huko na hatutakaa tufike huko.

“Niwataarifu wachochezi hawa kuwa jeshi la polisi ni imara, wasitikise kiberiti kama waliwahi kutikisa wakaguswa kule nyuma wasiende hatua nyingine, huku wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya. Ninawaonya wasijaribu tena kuendelea kufanya ushawishi na uchochezi huo,” amesema.

Aidha, amewaomba wananchi wawe watulivu waendelee kuishi kwa amani na utuvuli kama ambavyo ni mazoea, taratibu na desturi za Tanzania.

Ameongeza kuwa jeshi hilo halitakubaliana na aina yoyote ya uhalifu wa aina yoyote kwani walitegemea kama ni malengo ya kisiasa yaende kwenye hoja za kisiasa lakini yasitoke yakarudi kwenye matendo ya kihalifu.

“Maana nimeona na jeshi tumeona maneno ya uchochezi na kutisha na kuanza kuibuka kwenye mitandao ya kijamii na kuweka ushawishi kwa jamii yetu ambayo ni tulivu.

“Aina hii ya uchochezi na kwa hatua waliyofika ni hatua mbaya kwa sababu mikutano ya hadhara haijazuiliwa, lakini tunachozungumza ni matamko, mtu yeyote asijaribu kusogea huko. Kama hajaona mamlaka ya vyombo vya dola basi this time atayaona,” amesema.
Kauli hiyo ya IGP Wambura imekuja siku moja baada ya Wakili Boniface Mwabukusi kutangaza kuwa wataandaa maandamano yasiyo na ukomo nchi nzima iwapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halitafanyia marekebisho vifungu vya mkataba huo wa bandari ndani ya siku 14.

Jana tarehe 10 Mahakama Kuu kanda ya Mbeya ilitoa huku na kutupa mbali hoja sita muhimu zilizowasilishwa na wakili huyo aliyewakilisha wananchi wane waliofungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Chanzo: Mwanahalisi online
View attachment 2714475
Kituo chake cha kazi kimehamia Serena Hotel?
Press kama hiyo huchukuliwa light sana maana inaonekana ni mtu kaenda zake kula maharage pale akashiba halafu akaongea
Afanyie press kwenye eneo la polisi watu waone Yale Majengo Yao yanavyotisha hakuna mtu atajaribu kuinua hata kidole siku ya maanamano
Pili Hakuna mtanzania wa kuiondoa serikali madarakni hata ingekuwa serikali ya nyumba 10
Tanzania ndio nchi pekee duniani yenye viumbe vioga kuanzia watu mpaka wanyama wake ni waoga.
 
Kuna gazeti moja la kiswahili likiita Tazama Tanzania lilikuwa linaandika makala ndefu kuhusu illuminat/freemason. Katika muendelezo wa makala zake kuhusu kundi hilo duniani kupanga njama za kuangusha serikali nyingi duniani ili kutimiza mipango yao duniani (NWO) Tuliona maandamano ya arab spring na matokeo yake. Tukaona mapinduzi ya kijeshi nchi kadhaa za afrika. Kuna nchi wanazilia timing waziangushe serikali zake kwa njia wanazoona inafaa. Sasa hayo maandamano nyuma ya pazia hawakosekani wahuni hao wa dunia. Nia ni kuleta vurugu duniani ili wafanikiwe kutimiza mipango yao
 
Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo za Maandamano.

=====

IGP Wambura acharuka, asema kuna watu wanataka kuiangusha Serikali, “wasitikise kiberiti”

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amesema kuna kundi la watu ambao wamepanga kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – awamu ya sita kabla ya mwaka 2025.

Amesema watu hao ambao wamefanya kosa la uhaini, wanahusisha maandamano hayo na kushawishi watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za kuhusu mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Agosti 2023 jijini Dar es salaam, IGP Wambura amesema aliamini hoja za bandari hujibiwa kwa hoja.

Pia amesema aliamini kwa vile baadhi ya watu hao walienda mahakamani wangeheshimu mahakama lakini badala yake wametoka na kuanza kutafuta ushawishi na kuchochea kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima.

“Lakini mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanangusha serikali ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kabla ya mwaka 2025. Huu ni uhaini,” amesisitiza.

IGP Wambura amewaonya watu hao kwamba wakome na wasitishe matamshi yao hayo ya kichochezi lakini pili amesema watachukuliwa hatua za kisheria kutokana na uchochezi wanaoufanya na uhaini wanaoupanga kwani vyote ni makosa ya jinai.

Amesema Jeshi la polisi halitakaa kimya na kuwavumilia, kama walidhani lipo kimya litaenda kuwaonesha kuwa halipo kimya kwa yeyote atakayevunja sheria za nchi.
“Pili niwaombe watanzania wawapuuze watu hawa, Tanzania ni nchi ya amani ni nchi salama hawa wasitake kushawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko, hatujawahi kufika huko na hatutakaa tufike huko.

“Niwataarifu wachochezi hawa kuwa jeshi la polisi ni imara, wasitikise kiberiti kama waliwahi kutikisa wakaguswa kule nyuma wasiende hatua nyingine, huku wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya. Ninawaonya wasijaribu tena kuendelea kufanya ushawishi na uchochezi huo,” amesema.

Aidha, amewaomba wananchi wawe watulivu waendelee kuishi kwa amani na utuvuli kama ambavyo ni mazoea, taratibu na desturi za Tanzania.

Ameongeza kuwa jeshi hilo halitakubaliana na aina yoyote ya uhalifu wa aina yoyote kwani walitegemea kama ni malengo ya kisiasa yaende kwenye hoja za kisiasa lakini yasitoke yakarudi kwenye matendo ya kihalifu.

“Maana nimeona na jeshi tumeona maneno ya uchochezi na kutisha na kuanza kuibuka kwenye mitandao ya kijamii na kuweka ushawishi kwa jamii yetu ambayo ni tulivu.

“Aina hii ya uchochezi na kwa hatua waliyofika ni hatua mbaya kwa sababu mikutano ya hadhara haijazuiliwa, lakini tunachozungumza ni matamko, mtu yeyote asijaribu kusogea huko. Kama hajaona mamlaka ya vyombo vya dola basi this time atayaona,” amesema.
Kauli hiyo ya IGP Wambura imekuja siku moja baada ya Wakili Boniface Mwabukusi kutangaza kuwa wataandaa maandamano yasiyo na ukomo nchi nzima iwapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halitafanyia marekebisho vifungu vya mkataba huo wa bandari ndani ya siku 14.

Jana tarehe 10 Mahakama Kuu kanda ya Mbeya ilitoa huku na kutupa mbali hoja sita muhimu zilizowasilishwa na wakili huyo aliyewakilisha wananchi wane waliofungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Chanzo: Mwanahalisi online
View attachment 2714475

Kumbe Katiba hairuhusu maandamano kwa jambo ambalo wananchi hawakubaliani nalo?
 
Back
Top Bottom