IGP Wambura awaonya vikali wanaotaka kuandamana, asema huo ni uhaini akitaka "Wakome" na Wasitishe matamshi yao ya Kichochezi...

IGP Wambura awaonya vikali wanaotaka kuandamana, asema huo ni uhaini akitaka "Wakome" na Wasitishe matamshi yao ya Kichochezi...

We ni mbumbumbu,

Uhaini hufanya majeshi, Si raia asiye na silaha.

Maandamano ya Amani yameruhusiwa kikatiba.

Msizoeee kutaja mambo msiyoyajua maana mdomo huumba,

Mlimsingizia Mbowe ugaidi, mkamuumba gaidi halisi Hamza kada wa CCM.
Kaaandamane uone nani anafanya uhaini kama ni majeshi au raia na hakuna dhamana
 
Screenshot_2023-01-12-11-03-14-749_com.facebook.lite.jpg
 
Siungi mkono hayo maandamano, wamuache hangaya mbona anapiga kazi fresh tu, nchi imetulia, amanita, hela imemwagika mtaani yaani watu wanafuraha ya kutosha.

Muacheni mama bhana, kama mlishindwa kuandamana kipindi cha jiwe wkt anaikanyaga katiba sioni umuhimu wa maandamano kwa sasa.
 
Kaaandamane uone nani anafanya uhaini kama ni majeshi au raia na hakuna dhamana
Watishe wajinga wenzio,

Rais mbunge , IGP nk huapa kulinda wananchi, Si kuua wananchi.

Msafara wa Rais Kila kukicha watu huenda na mabango kueleza kero zao Ili zitatuliwe,

Hatujawahi ona polisi wakiwashtaki wabeba mabango Kwa uhaini.

Hii Nchi inaongozwa na SHERIA na Katiba.
 
Watishe wajinga wenzio,

Rais mbunge , IGP nk huapa kulinda wananchi, Si kuua wananchi.

Msafara wa Rais Kila kukicha watu huenda na mabango kueleza kero zao Ili zitatuliwe,

Hatujawahi ona polisi wakiwashtaki wabeba mabango Kwa uhaini.

Hii Nchi inaongozwa na SHERIA na Katiba.
Si ukaandamane mbona unaongea upuuzi jf,Toka humu nenda barabarani ndugu zako watatoka definition ya TiananMen Square
 

Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo za Maandamano.

=====

IGP Wambura acharuka, asema kuna watu wanataka kuiangusha Serikali, “wasitikise kiberiti”

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amesema kuna kundi la watu ambao wamepanga kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – awamu ya sita kabla ya mwaka 2025.

Amesema watu hao ambao wamefanya kosa la uhaini, wanahusisha maandamano hayo na kushawishi watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za kuhusu mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Agosti 2023 jijini Dar es salaam, IGP Wambura amesema aliamini hoja za bandari hujibiwa kwa hoja.

Pia amesema aliamini kwa vile baadhi ya watu hao walienda mahakamani wangeheshimu mahakama lakini badala yake wametoka na kuanza kutafuta ushawishi na kuchochea kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima.

“Lakini mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanangusha serikali ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kabla ya mwaka 2025. Huu ni uhaini,” amesisitiza.

IGP Wambura amewaonya watu hao kwamba wakome na wasitishe matamshi yao hayo ya kichochezi lakini pili amesema watachukuliwa hatua za kisheria kutokana na uchochezi wanaoufanya na uhaini wanaoupanga kwani vyote ni makosa ya jinai.

Amesema Jeshi la polisi halitakaa kimya na kuwavumilia, kama walidhani lipo kimya litaenda kuwaonesha kuwa halipo kimya kwa yeyote atakayevunja sheria za nchi.
“Pili niwaombe watanzania wawapuuze watu hawa, Tanzania ni nchi ya amani ni nchi salama hawa wasitake kushawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko, hatujawahi kufika huko na hatutakaa tufike huko.

“Niwataarifu wachochezi hawa kuwa jeshi la polisi ni imara, wasitikise kiberiti kama waliwahi kutikisa wakaguswa kule nyuma wasiende hatua nyingine, huku wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya. Ninawaonya wasijaribu tena kuendelea kufanya ushawishi na uchochezi huo,” amesema.

Aidha, amewaomba wananchi wawe watulivu waendelee kuishi kwa amani na utuvuli kama ambavyo ni mazoea, taratibu na desturi za Tanzania.

Ameongeza kuwa jeshi hilo halitakubaliana na aina yoyote ya uhalifu wa aina yoyote kwani walitegemea kama ni malengo ya kisiasa yaende kwenye hoja za kisiasa lakini yasitoke yakarudi kwenye matendo ya kihalifu.

“Maana nimeona na jeshi tumeona maneno ya uchochezi na kutisha na kuanza kuibuka kwenye mitandao ya kijamii na kuweka ushawishi kwa jamii yetu ambayo ni tulivu.

“Aina hii ya uchochezi na kwa hatua waliyofika ni hatua mbaya kwa sababu mikutano ya hadhara haijazuiliwa, lakini tunachozungumza ni matamko, mtu yeyote asijaribu kusogea huko. Kama hajaona mamlaka ya vyombo vya dola basi this time atayaona,” amesema.
Kauli hiyo ya IGP Wambura imekuja siku moja baada ya Wakili Boniface Mwabukusi kutangaza kuwa wataandaa maandamano yasiyo na ukomo nchi nzima iwapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halitafanyia marekebisho vifungu vya mkataba huo wa bandari ndani ya siku 14.

Jana tarehe 10 Mahakama Kuu kanda ya Mbeya ilitoa huku na kutupa mbali hoja sita muhimu zilizowasilishwa na wakili huyo aliyewakilisha wananchi wane waliofungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Chanzo: Mwanahalisi online
View attachment 2714475

Mama alipe madeni ya watu na aachane na mikopo yenye masharti magumu
 
jipeni matumaini tu kuwa haelewi halafu mje muende mkaandamane yatayowakuta hatahusika mbowe wala lissu mtajuta wenyewe
Wewe wasiwasi wako nini, unadhani Nyerere na Mandela wangekuwa waoga kama wewe wangekuwa marais na kufa kwa heshima.
 
Kwa mtandao ulivyo kuna kila dalili polisi watashindwa haya maandamano.
Wanaounga mkono maandamano ni ccm, polisi, cdm , raia.
Idadi ya polisi iliyopo na mpango uliopo vitakinzana.
 
Kwa mtandao ulivyo kuna kila dalili polisi watashindwa haya maandamano.
Wanaounga mkono maandamano ni ccm, polisi, cdm , raia.
Idadi ya polisi iliyopo na mpango uliopo vitakinzana.
Bila kusahau wadau wote wa Bandari na wanufaika wake.

KAZI IPO!!
 
Ni hatari kwa kiongozi wa Umma kutoa matamshi kama haya

Tumevumilia sana,na IGP amevumilia sana. Kuanzia sasa mtashangaa watu watapigwa mabomu kule ambako wameambiwa waache kwenda na polisi,

Huyu ataupata mwisho anaoutafuta,waliokaribu nae wamshauri kusimamia jukumu lake kwa mujibu wa sheria maana yeye sio wa kwanza
 
Hawa ndio walio enda kusikiliza presentation ya haki jinai.

Leo tayari ana badilisha statement ana sema kuna watu wana taka kupindua serikali.

Tukisema polisi ni mabingwa wa kubandikia watu kesi wao wana bisha.

Sasa huyo ndio boss wa polisi anaonge hivyo

Ati maandamano ni kuvunja sheria?

Ipi?
 
Back
Top Bottom