Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camilius Wambura amemueleza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo kuwa kwa sasa hali ya usalama nchini ni shwari, na hivyo kuwapongeza Polisi, vyombo vya usalama na raia wapenda amani kuwezesha hilo.
IGP Wambura ameyasema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaoanza leo Septemba 12, 2024 mkoani Kilimanjaro.Mkutano ambao utajadili masuala ya kisera na kuweka mikakati ya kiutendaji ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
Kauli mbiu ni “Huduma Bora za Kipolisi kwa Umma Zitapatikana kwa Kubadilika Kifikra, Usimamizi wa Sheria na Matumizi ya TEHAMA”Naye Naibu Waziri Sillo amewapongeza makamanda wa Jeshi la Polisi katika kuhakikisha nchi inakuwa shwari, lakini vilevile amempongeza IGP kwa kuufanya mkutano wa mwaka huu wa kipekee kwa kuunganisha na kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi kinachotarajiwa kusherekewa Septemba 17, 2024.