McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillius Wambura, amezindua kampeni ya msamaha wa usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari, 2026 jijini Dodoma, akiwahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kusalimisha silaha walizonazo kinyume cha sheria bila hofu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, IGP Wambura amesema kampeni hiyo inalenga kuimarisha usalama wa wananchi na kuzuia matumizi ya silaha haramu katika vitendo vya uhalifu, akieleza kuwa ushirikiano wa Wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama ni nguzo muhimu ya kudumisha amani nchini.
“Tunawaomba wananchi wajitokeze kusalimisha silaha haramu walizonazo kwa hiari. Lengo letu ni kuimarisha usalama na kulinda amani ya nchi yetu,” amesema IGP Camillius Wambura.
Aidha, IGP Wambura amesema Jeshi la Polisi litaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kumiliki silaha kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa, huku akisisitiza kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za kuondoa silaha haramu katika jamii.