IGP Wambura: Wahalifu wakae chonjo, huu ni wakati mbaya kwao

IGP Wambura: Wahalifu wakae chonjo, huu ni wakati mbaya kwao

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura ametoa onyo kwa wahalifu wote kwani wakati huu ni wakati mbaya sana kwao.

Wambura ameyasea hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo ljumaa Septemba 16, 2022 kwenye kikao cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun kuhusu hali ya usalama nchini.

View attachment 2358932
Kama hawaoni kinachoendelea.. Swali Bwana Wambura, kinachoendelea ni nini? Mliowashika juzi mmewaua? kama ulivyoua MKIRU?
 
Mpaka dakika hii wakati ni mbaya kwa raia..., nadhani ile kanuni ya less talk more actions awamu hii waichukue waende wakaitazame
 
Hakuna aliye juu ya sheria na nchi inabidi iendeshwe kisheria, huwezi kukurupuka na kuanza ku arrest watu bila ya kuwa linked na crime scene kuna watu makatili mno humu JF, mijitu anayofurahia damu ya binadamu, igp fuata sheria, arrest only when una case mkononi sio mihemko, jeshi la police linahitaji kuundwa upya ili liendane na technology ya sasa, utumiaji wa mabavu umeshapitwa na wakati
 
😳😳😳
 
Kushinda au kushindwa ni kupi ?!!! Kwani haya ni mashindano....

Nadhani hawa watu wanasahau kwamba crime prevention na kuwa pro-active kwa kutoa elimu kuwa na inteligensia na karibu na wadau (na sio maadui wa raia) ndio kushinda kwao..., Huwezi ukaniambia unashinda wakati uhalifu unaongezeka na wewe kujisifia ni wangapi umemwaweka lupango
 
Jeshi la Polisi likishirikiana kwa karibu na wenyevita wa Serikali za mitaa hakika uhalifu utakwisha kabisaa, viongozi wa Serikali za mitaa wanafahamu maeneo yote wanayo jificha wahalifu na wavuta bangi
 
Polisi hawaongozwi Kwa maadili wengi wanaishi maisha ya kutegemea vibaka wezi na majambazi, kila mkoa kila wilaya police ndio wanafunga vibaka, wezi na majambazi, wengine tetesi ndio wanawatuma na kuwaazima silaha za magendo, tunaishi na watu iwe ni majengo, chamwino, manzese, mjimpya , Soweto, Ndanguro la wezi vibaka na majambazi ni police wenyewe
 
Kushinda au kushindwa ni kupi ?!!! Kwani haya ni mashindano....

Nadhani hawa watu wanasahau kwamba crime prevention na kuwa pro-active kwa kutoa elimu kuwa na inteligensia na karibu na wadau (na sio maadui wa raia) ndio kushinda kwao..., Huwezi ukaniambia unashinda wakati uhalifu unaongezeka na wewe kujisifia ni wangapi umemwaweka lupango
Mimi najiuliza, inakuwaje kundi la vijana 40 wanajikusanya Temeke, wengine Kawe, Tabata n.k na kwenda kwa mguu kupiga tukio na wanatawanyika na kwenda kukutana tena kugawana vitu bila kujulikana?

Yani kila mtaa kundi lake la zaidi ya watu 30- 40 linajipanga na kufanikisha? Hawa vijana wakipata siraha je?
 
Niwakati sasa wajumbe wa nyumba kumi kuhusika kwa asilimia 100 katika kuwatambua wakazi wa eneo lao,Wote na shughuli zao,hats kama ni tegemezi ajulikane ni dependent wa nani?,na utengenezwe utaratibu mhalifu atakapoonekana anatoka katika shina husika la mjumbe Fulani mjumbe ahusike,Kwa kutomtambua mkazi huyo au mzazi pia ahusike,wazazi wahusike katika kutoa taarifa za watoto wao ambao wanamienendo isiyojulikana bila kuficha,ili serekali isaidie kuwanyoosha mapema,intact wako watoto ambao wamechapwa na wazazi mpaka wazazi wamechoka,Toto halisikii mishowe linamtesa mzazi kulitoa mahabusu mpaka uchumi wa familia kutetereka,pia SI vibaya NDANI ya jeshi letu kukawa na kitengo cha kurekebisha watoto manunda ambao wanawachosha wazazi,ili wazazi Kwa hiyari yao wawapeleke katika kuwanyoosha,na kuwarudisha katika mstari sahihi.
N.B,Naandika haya nikitumia akili ya hali ya juu kabisa ya kiintelegensia nikimaanisha huenda hawa panya road baada ya kusikia msako mkali wakarudi kwenye familia zao na kuvunja makambi yao ya kialifu,na ajabu wazazi wa kuwapokea majumbani kama mashujaa,ndio maana nikapendekeza zoezi hili lianzie kwenye ofisi za S/M.
 
Back
Top Bottom