IGP Wambura: Wahalifu wakae chonjo, huu ni wakati mbaya kwao

IGP Wambura: Wahalifu wakae chonjo, huu ni wakati mbaya kwao

Majambazi, wauza madawa ya kulevya, wavuta bangi na wahalifu wa aina zingine tunawaficha sisi wananchi, wapo kwenye mitaa yetu.

Narudia tena Jeshi la Polisi likishirikiana kwa karibu na Viongozi wa Serikali za Mitaa haswa kwa Mkoa wa DSM na hakika uhalifu utatokomezwa kwa 99%
 
Niwakati sasa wajumbe wa nyumba kumi kuhusika kwa asilimia 100 katika kuwatambua wakazi wa eneo lao,Wote na shughuli zao,hats kama ni tegemezi ajulikane ni dependent wa nani?,na utengenezwe utaratibu mhalifu atakapoonekana anatoka katika shina husika la mjumbe Fulani mjumbe ahusike,Kwa kutomtambua mkazi huyo au mzazi pia ahusike,wazazi wahusike katika kutoa taarifa za watoto wao ambao wanamienendo isiyojulikana bila kuficha,ili serekali isaidie kuwanyoosha mapema,intact wako watoto ambao wamechapwa na wazazi mpaka wazazi wamechoka,Toto halisikii mishowe linamtesa mzazi kulitoa mahabusu mpaka uchumi wa familia kutetereka,pia SI vibaya NDANI ya jeshi letu kukawa na kitengo cha kurekebisha watoto manunda ambao wanawachosha wazazi,ili wazazi Kwa hiyari yao wawapeleke katika kuwanyoosha,na kuwarudisha katika mstari sahihi.
Hivi kitengo hiki hakipo katika jeshi la polisi? Sio wale dawati la jinsi! Na mm nauliza mwenye ufahamu zaidi utupe ufafanuzi.
 
Hali si nzuri, usiku wa jana kuna familia imevamiwa baba yao akiwa safarini. Bahati hakuna aliyeumizwa zaidi ya kuporwa fedha na vitu vingine!
 
Hakuna aliye juu ya sheria na nchi inabidi iendeshwe kisheria, huwezi kukurupuka na kuanza ku arrest watu bila ya kuwa linked na crime scene kuna watu makatili mno humu JF, mijitu anayofurahia damu ya binadamu, igp fuata sheria, arrest only when una case mkononi sio mihemko, jeshi la police linahitaji kuundwa upya ili liendane na technology ya sasa, utumiaji wa mabavu umeshapitwa na wakati

Nchi zote unazoziona zimeendelea zilijengwa Kwa mabavu.

Hakuna mabavu hakuna maendeleo katika taifa lolote lile.

Mkishapata maendeleo ndio mnaendelea na mambo ya demokrasia.

Nchi Masikini na wajinga wengi bado usiiendeshe kimabavu.

Mabavu yasitumike Kwa watu wema Hilo ndio angalizo lakini wahalifu ni Shaba tuu
 
Wakitaka kuwa effective yaani kusiwe na kesi, tuwakute watuhumiwa (panya road) mortuary
 
TUFUKIE CHEMCHEM ZA PANYA ROAD WAPYA,KWA KUDHIBITI WATOTO WA MITAANI,MAANA WANAKUWA BILA KUWA NA FORMULA YA MSINGI YA KIMAISHA,PIA JESHI LETU LIJUE PANYA ROAD NI GENGE LINALOUNDWA KIMKAKATI YAANI HUTOKA MAJUMBANI MWAO,KUUNGANA NA KUFANYA TUKIO,WAKIMALIZA TUKIO HUREJEA MAJUMBANI MWAO,NDIO MAANA NIKAPENDEKEZA HATUA ZA UTAMBUZI WA NYUMBA KWA NYUMBA ZOEZI LIKIENDESHWA NA WAJUMBE WENYEVITI NA SUNGUSUNGU,NA POLISI JAMII.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura ametoa onyo kwa wahalifu wote kwani wakati huu ni wakati mbaya sana kwao.


Wambura ameyasea hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo ljumaa Septemba 16, 2022 kwenye kikao cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun kuhusu hali ya usalama nchini.

View attachment 2358932

Ana maana kulikuwa na wakati mzuri kwao kwa ruksa yao?
 
Back
Top Bottom