IGP Wambura: Wanaume nao wanapitia ukatili wa kimya kimya

IGP Wambura: Wanaume nao wanapitia ukatili wa kimya kimya

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura amesema wanaume nchini wana haki ya kulindwa, kusikilizwa na kupewa heshima ambapo wametakiwa kutumia ofisi za Dawati la Jinsia kuripoti ukatili wanaofanyiwa majumbani.

IGP Wambura amesema hayo wakati akifungua Mradi wa jengo la ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Tarime, Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya ambapo jengo pamoja na Samani zake limegharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni mia tatu chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Edward Gowele amesema kuwa, hali ya usalama wilayani humo ni shwari na kwamba wananchi wapo mstari wa mbele katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Naye Dkt. Majaliwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Watu Duniani - UNPA amesema kuwa, kukamilika kwa jengo la ofisi za Dawati la Jinsia kutasaidia katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwamba UNPA itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Chanzo: ITV​
 
Mke kama huyu tayari ni ukatili tosha aiseee
 

Attachments

  • Chuma.jpg
    Chuma.jpg
    61.3 KB · Views: 39
Nimepitia ukatili sana kutoka kwa wapenzi, Hadi nimeamua kuwa bikra na mapenzi kiyatupa kando.. hakuna mnyanyasaji mmnaya kama mwanamke 😬😬 Bora unyanyaswe na mama wa kambo kuliko mwanamke mpenzi jini
 
😂😂😂 muende kwenye dawati la jinsia mkifanyiwa ukatili
Halafu unamkuta mwanamke ndiye unamueleza shida yako, unategemea upate haki.

Ilibidi huko dawati la jinsia wakae wale wenye jinsia zote, hormone zote sawa na wasiegemee upande mmoja.
 
Back
Top Bottom