Bigmaaan
JF-Expert Member
- Nov 25, 2023
- 660
- 1,438
Heri ya Christmas wakuu.
Kuna Flyer nimeiona ya Ndg Nchemba, akitoa salamu za Christmas. Lakini pia anasema "WAMEJIFUNZA". Wamejifunza nini? Imekuwaje wamejifunza?
Kuna line moja ya Tupac, inasema
"I will not change the world, but I guarantee that I will spark the brain that will change the world"
Siasa za Tanzania za kupigania watu na kubadilisha nchi, zilizaliwa upya 21.01.2025. Mahubiri ya kufanya mabadiliko makubwa ya Siasa za nchi hii yalianzia hapo. Miezi kadhaa ya kuamsha fikra wananchi yalianza. Watawala wakaamini kuwazuia wahubiri wangezuia, ila walikosea. Walipambana na wahubiri, na sio neno. Neno lilikuwa tayari vichwani mwa watu. Waliohubiriwa. Waamini, wakachukua hatua Oct 29, 2025.
Leo tuko hapa. Tuko kwenye sintofahamu kubwa. Ndg M.Nchemba anasema kuwa "WAMEJIFUNZA".
Wamejifunza nini?
Kuwa nchi hii ni yetu sote?
Kuwa uongozi wa nchi hii unatoka kwa wananchi?
Kuwa viongozi ni watumishi wa wananchi?
Kuwa wananchi sio subjects wa viongozi?
Kuwa kikundi kidogo cha watu hakiwezi waamuliwa wananchi nani awe Mwenyekiti wao wa Mtaa, nani awe Diwani wao, nani awe Mbunge wao?
Kuwa lengo kuu la Serikali ni ustawi wa wananchi?
Swali kuu. TUWAAMINI?
Cc: Pascal Mayalla MALCOM LUMUMBA zitto junior