Ijaribu hapa System inayoandika cover letter zenye mvuto

Ijaribu hapa System inayoandika cover letter zenye mvuto

Updates ..
System yetu imefikia kwenye hatua nzuri, tunatumaini hadi Ijumaa ya wiki hii (tar 23 December 2022) tutakuwa tumeiweka kwenye premium hosting kwa ajili ya matumizi ya jamii. Hivyo kwa wale wote ambao mlitoa suggestions mnaweza ipitia tena na kuangalia kama kuna kingine chochote ambacho mngependa kiwe included ili tuweze kukifanyia kazi kabla ya Ijumaa hii.

Ahsanteni.
Sijui niseme nn ila kifupi
Umeupiga mwingi sanaa mzee baba
Kitu inatoa mzgo piruuuu
Sasa hivi ni mwendo wa kutuma tu cover letter
 
Tumefanya baadhi ya mabadiliko makubwa ya lazima

1. Ili uweze kutumia system utahitaji ku_login (Sababu kubwa ni ili kuweza kuhifadhi barua ambazo umetengeneza kwenye account yako, ili wakati wowote ukizihitaji uweze kuzipata)
2. Kuondoa ulazima wa kuingiza taarifa zako kila unapotaka kutengeneza barua. - Hivyo kwa sasa utaingiza taarifa zako mara moja tuu. Baada ya hapo utakuwa ukiandika position unayoomba na system itatumia taarifa ulizo_save kukupa barua yako. Japo kuwa utakuwa na uwezo wa kuedit/kuongeza kitu kingine kwenye taarifa zako.
3. Ni maandalizi ya kuunganisha mfumo wa barua na mfumo wa kutengeneza CV
4. Ni maandalizi ya kuunganisha mfumo wa barua na mfumo wa kukuandikia email kwa kazi unayoomba. (Wengi wamekuwa wanapata shida kitu gani waandikie kwenye email ya maombi ya kazi wanapo_attach CV na cover letter zao)
5. Ni maandalizi ya kuunganisha system na SMS/WhatsApp notifications kwa kazi ambayo ina_match na Skills& Experience yako.
Hayo yote yamefanya kuweka mfumo huu kuhitaji mtumiaji ku_login, na pia tumefikia hatua hii kutokana na maoni ya wadau.

Mnaweza ujaribu tena na mkanipa feedback >> JOB ASSIST
 
Baada ya kujisajili hatua ya kwanza ingiza taarifa za profile yako ukianza na
1. Bonyeza User Information - jaza taarifa
2. Bonyeza Education Information - jaza taarifa zako
3. Experience information - jaza taarifa zako kisha bonyeza SAVE
1672751467711.png
 
Baada ya hapo ukihitaji kutengeneza barua bonyeza
create cover letter kisha itatokea sehemu ya kuandika position unayotaka kuomba
Andika kama hivi Program Manager - XYZ Company/Organization
kisha bonyeza process (baada ya hapo subiri kidogo utaletewa barua)

1672751644252.png
 
Barua iko na button mbili
1. Rewrite = kama hujaridhika na barua ya kwanza bonyeza hapo ili uweze kuandikiwa nyingine
2. Save this letter = kama umeipenda barua ha hutaki kuipoteza bonyeza save this letter kisha utaweza kuipata barua yako wakati wowote kwa kubonyeza saved letters
1672752125012.png
 
Barua zako zote ambazo ume_save utazipata ukibonyeza saved, hivyo wakati wowote utaweza kuzitumia

1672752687950.png
 
Nashughulikia changamoto ya kusave details (mmekuwa mkisave data za education, experience, na skills kwenye system lakini zimekuwa hazionekani) so naomba muda kidogo nitawajulisha ikiwa solved.
 
Nashughulikia changamoto ya kusave details (mmekuwa mkisave data za education, experience, na skills kwenye system lakini zimekuwa hazionekani) so naomba muda kidogo nitawajulisha ikiwa solved.
UPDATES: nime_solve changamoto ambayo ilijitokeza, sasa unaweza endelea kujaribu na kunipa feedback
 
UPDATES:

Nimeboresha grammar and spelling check kwenye barua, hivyo mnaweza mkajaribu na mkanipa feedback.

Nitaendelea kufanya maboresho mengine kuanzia jumamosi, kwa sasa napumzika najiandaa na interview ya kazi Ijumaa, niombeeni Mungu awe pamoja nami.
 
UPDATES
kama unataka kushare private link ya barua yako kwa mtu mwingine au public kwanza save barua, kisha bonyeza share to public then itakuletea option ya kuweza kushare kwenye WhatsApp na mitandao mingine
1673005551611.png
 
UPDATE

Tumeshughulikia changamoto ya kudownload_barua baada ya kuitengeneza ambayo ilikuwa inajitokeza kwa watumiaji wa simu

1673439899086.png
 
UPDATE
Tumefanya maboresho kidogo kwenye mambo ya grammars. So, kwa sasa utapata barua ambazo ziko na lugha ambayo imenyooka zaidi.

--
Pia, bado tunafanya internal testing kwenye issue ya CV, so ikiwa sawa tuta_activate ianze kuonekana.
 
UPDATE:
Tumeweka daily limit ya kuandika barua 5 kwa siku, na limit ya kuomba kuiandika upya barua ni mara 4 kwa siku.
Hii nikutokana na wengine kutokuwa na matumizi serious ya system.

unakuta mtu mmoja anaomba kuandika barua ya position hiyo hiyo mara 100 hicho sio kitu kizuri resources nilizonazo kwenye kusimamia system zipo limited, hivyo hiyo limit itasaidia kila ambaye yupo serious kuweza kutumia mfumo.
 
Back
Top Bottom