Ijue Aquamation, Archbishop Desmond Tutu's aliomba achomwe kwa njia hii badala ya moto

Ijue Aquamation, Archbishop Desmond Tutu's aliomba achomwe kwa njia hii badala ya moto

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,914
Reaction score
168,320
Archbishop Desmond Tutu amepumzishwa kwa amani kwenye makao yake ya milele mjoni Cape Town baada ya kufanyiwa taratibu zote za kuuaga mwili wake kwa heshima za kiserikali na kidini ambapo kukafanyika shughuli nyingine ndogo nyuma ya mimbari aliyokuwa akiitumia kukemea na kuupinga vibaya utawala dhalimu wa kibaguzi wa rangi ulikuwa ukitumiwa na Makaburu dhidi ya watu weusi.

Askofu Tutu AMBAYE alipata tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1984 ameombolozewa na watu wote duniani na anakutumia kwa namna alivyopambana na ubaguzi wa rangi bila ya matumizi ya nguvu.

Askofu Tutu alikuwa ni mtetezi mkubwa wa mazingira, alitoa hutuba nyingi za kukemea uharibufu wa mazingira na aliandika machapisho mengi ya kutetea mazingira na kupambana na mabadiliko ya Hali ya nchi. Hivyo aliagiza mwili wake uteketezwe kwa maji badala ya kuzika au kuchomwa Moto, kwani kuzika kunapunguza eneo la ardhi ambalo lingetumiwa kwa matumizi mengine endelevu, na hakutaka mwili wake uchomwe Moto kwani kwa kufanya hivyo kungezalisha kiasi kikubwa cha hewa chafu. Njia ya kuteketeza miili kwa maji NI njia salama na rafiki kwa mazingira.

Aquamation Ni Nini?​

Aquamation Ni aina ya kuteketeza mwili wa marehemu kwa kutumia maji njia ambayo inatajwa kwamba ni rafiki wa mazingira na ya kisasa zaidi.

Mchakato huu pia hujulikana kwa jina la "alkaline hydrolysis",
Ambapo mwili wa marehemu huwekwa ndani ya maji yaliyochanganywa na alkali kali sana kama vile potassium hydroxide kwa masaa matatu hadi manne ukiwa ndani ya pressurised metal cylinder na kupashwa Moto hadi kufikia nyuzi joto 150 degrees Celsius.

Mchakato huu hufanya kila kitu kigeuke kuwa maji isipokuwa mifupa tu, ambayo baada ya hapo hukaushwa kwenye oven, Kisha kuvunjwavunjwa na kuwa vipande vidogo vidogo ambavyo huwekwa kwenye chombo maalum.

Kisha baada ya hapo maji Yale huruhusiwa yaende kwenye mfumo rasmi wa maji taka.

Ni kwa muda gani mfumo huu umekuwepo?​

Mfumo huu uligunduliwa miaka ya mwanzo ya 1990s kama njia ya kuteketeza miili ya mabaki ya wanyama waliotumika kwa majaribio mbalimbali ya kisayansi maabara.

Pia njia hii ilitumuka kuteketeza ng'ombe kipindi ambacho Marekani ilikumbwa na janga la ugonjwa wa kichaa cha ng'ombe.

Mtafiti wa Kimarekani Philip R Olson anasema kwenye miaka ya 2000s, vyuo vya utabubu vya USA walitumia aquamation kuteketeza maiti za kujifunza ( cadavers, ) kabla haijawa njia rasmi ya kuteketeza miili kibiashara, aliandika kwenye chapisho lake la mwaka 2014.

Nijia hii pia hutumika kwenye machinjio kuteketeza takataka zitokanazo na wanyama kama vile damu, kinyesi na sehemu za nyama zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.
 
Bado haujatueleza alkaline iliyotumika inaokolewaje au nayo inakwenda kwenye mfumo wa maji taka na haitakuwa na madhara?
 
Back
Top Bottom