Ijue Biashara ya kunenepesha Ng'ombe yenye faida kubwa

Ijue Biashara ya kunenepesha Ng'ombe yenye faida kubwa

OK. IKO HIVII, MIMI NI MTUMISHI WA SERIKALI NIPO TOWN, NILICHUKUA SALARI LOAN NIKANUNUA DUME 4 WA LAKI 4 KILA 1, NA DUME 4 WA LAKI 3 KILA MOJA, NA DUME 4 WA LAKI 2 KILA MOJA. JUMLA WAKAWA DUME 12 NA GHARAMA YA MANUNUZI IKIWA 3.6M NINAWAFUGIA KIJIJINI KWETU BABATI VIJIJINI, WOTE NILIWAPA DAWA YA MINYOO BAADA TU YA KUWANUNUA, IKAWA WANALISHWA TU MAJANI KWA MIEZI 4,THEN NIKAJA NUNUA MASHUDU GUNIA 10 WAKATI YAKIWA BEI RAHISI SEHEMU PANAITWA HYDOM, MANUNUZI NA USAFIRI MPAKA KWETU IKAWA KAMA 170,000. IKAWA WALE 4 WAKUBWA WANALISHWA PUMBA NA MAJANI,THEN AFTER ANOTHER 4 MONTHS NIKAWAUZA JUMLA YA 2.7M,WAKABAKI ZILE BATCH 2 AMBAO NI DUME 8., ILE 2.7M NIKAONGEZEA LAKI 4 NIKANUNUA TENA DUME 12 WA SIZE TOFAUTI,JUMLA WAKAWA 20. NIKAWA SASA KILA BAADA YA MIEZI 3 NAUZA BATCH YA DUME 4 , MALISHO NI MAJANI,ILA ILE BATCH INAYOKARIBIA KUUZWA KWA MIEZI 3 NAWACHANGANYIA NA PUMBA, KWENYE MAJI NAWEKA CHUMVI KIDOGO, NA NAWAPA DAWA MINYOO SEASONALY,KILA MWEZI KUNA KIJANA WA KUCHUNGA NAMLIPA ELFU 40. NIKIPIGA MAHESABU YANGU VIZURI HUWA KILA MIEZI 3 SIKOSE 1M KAMA NET PROFIT WAKATI NIKIWA MJINI BILA HATA KWENDA KUWAANGALIA. KUHUSU SOKO SIKU HIZI LIPO NJE NJE MIE NIKITAKA KUUZA KUNA WATU NAWAPAGA TU TAARIFA WANAWAFUATA NYUMBANI
Mkuu bado unaendelea na hii biashara? Hydom wanauzaje mashudu kwa gunia?
 
Asante kwa uzi huu mzuri, binafsi changamoto kwenye ufugaji wa ng'ombe ni wizi yaani sijapata suluhu jinsi ya kudhibiti tatizo la wizi ....naomba mwenye ujuzi zaidi tusaidiane

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Wezi wanaturudisha nyuma, nahitaji kufuga 🐮 lakini nafsi inasita sababu ya wezi, kwangu wanashusha nazi kinyama, sasa 🐮 si ndio itakuwa kama kumsukuma mlevi.. Nafikiria ninunue cha moto 🔫 lakini nasikia mlolongo ni mrefu, kuna ile mishale ya kulenga kama bunduki ndio natafuta, ukipata huko tushituane, nataka nimtwange mtu mshale wa kalio tuheshimiane.😠
 
Huu uzi umekwama ..... hauna mirejesho wala muendelezo
 
Mkuu bado unaendelea na hii biashara? Hydom wanauzaje mashudu kwa gunia?
Hii biashara mzee wangu aliwahi kuifanya ila kwa kutegemea madume wanaozaliwa nyumbani wakue anenepeshe auze nakumbuka kuna dume mmja aliwah muunganish kwa wanaopakia ng'ombe kupelek arusha kwa yule dume tulipata lak8 na ushee na hakuwa mkubwa kivile alizingatia lishe,dawa na virutubisho vya kunenepesh mfugo ambavyo vilikuwa si bei kubwa na vingi tulikuwa tunapata kwa dada mmja alikuwa akifany kazi kwenye kampuni fln la mifugo....kama mtu anamtaji mzuri morogoro,manyara ni sehem nzur kwa biashr hii.....tatizo ni WEZI hawa watu wanarudsh nyuma san wafugaji wadogowadogo
 
Changamoto ya wizi tunaishughulikia vipi?
 
Kwa mbegu za ng'ombe nenda ranchi za serikali nunua Borani hii ni mbegu nzuri ya nyama,ng'ombe anakuwa mkubwa sana kufika hata 1000kg,dume wanauza 600,000/=.Maelezo zaidi utayapata huko
Kwa anayeanza kuanza na borani atakula hasara borani wanahitaji matunzo ya hali ya juu na kuna baadhi nya maeneo nchini hawawezi stahimili na hii biashara ya kunenepesha ng'ombe nenda hasa mkoa wa kagera wilaya ya Misenyi, Karagwe ndio kwenyewe nunua ng'ombe katka mazingira hayo hayo usiwatoe mbali kama Geita au Biharamuro wanaweza kufa pia baada ya nunua lipia vitalu kwa watu binafsi ambao hukodisha kwa mwaka yaani kila ng'ombe ni tsh laki moja kwa mwaka japo kwenye kitalu kunenepa hachukua miezi mitatu hadi minne kwa zile ngombe wanaita nyankole zenye mapembe makubwa na kwa ngombe mkubwa kwa Uganda wanauzwa hadi millioni mbili za TZ au million nne za UG kule kuna usindikaji na kuuzwa nje nyama na jamii ya kule ngombe kwao ni kama dhahabu ngoja waje wataalamu zaidi
 
Back
Top Bottom