Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Wakati unajaribu kutuelimisha kuhusu haya kumbuka tuna precedent ya Ndugu Alphayo Kidata.

Rais Magufuli alimtengua kuwa Balozi wa Canada na akamvua hadhi ya ubalozi kabisa.

Katika kumbukumbu zangu Ndugu Kidata hakuwahi kufikishwa mahakamani kwa tuhuma yoyote ile wala hajawahi kurudishiwa hadhi ya Ubalozi.

Je una uhakika gani kama ni lazima Dr. Slaa atafikishwa mahakamani na atarudishiwa hadhi hiyo hata kama itatokea ameshinda??

Tuna precedent ya Balozi Mahalu licha ya kushinda kesi yake mwaka 2012 hakurudishiwa hadhi ya Ubalozi na Mh. Kikwete badala yake alirudishiwa hadhi hiyo mwaka 2018 na Hayati Magufuli. Bila shaka Magufuli alimrudishia hadhi kwa mamlaka yake na utashi wake binafsi tu.

Tujadili Pascal Mayalla
 
Mwili usio na Kinga ni uchochoro wa maradhi. Mwili utashambuliwa na kila aina ya magonjwa mwisho kifo.
Kumbe balozi anakinga ya kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai(bila shaka hata ya madai)!. Kama Kinga imeondolewa tutarajie yaleyale kama ya ukosefubwa kinga za mwili.
 
Alafu niliwahi kusikia pia kuwa hadhi/status ya ubalozi kiuhalisia huwa haivuliwi kama ilivyo jeshini....manake once a soldier always a soldier maishayako yote
 
Prof. Costa Mahalu alipewa Ubalozi na BW Mkapa, alivuliwa Ubalozi na JK (hila). Kumbuka hata Rais mstaafu BW Mkapa alisema Prof Mahalu ni mtu muadilifu sana.
Dk Magufuli alimpa Ubalozi Dk Slaa. Mama Samia amemvua hadhi ya Ubalozi Dk Slaa. (hila)
Dk atarudishiwa hadhi yake ya Ubalozi na Rais mpya atakaeingia 2025.
 
Hadi tuone hayo mashtaka yenu ya kubumba, la sivyo unachoeleza ni assumption
Hizi sekeseke dhidi ya Dr Slaa zimeanza baada ya kukosoa mkataba, kabla ya hapo hatukusikia hiyo kitu
Na Dr Slaa alishasema kwamba wametishia kumcutia huo ubalozi, na akawajibu "chukueni"
Mwambukusi alitishiwa na kushtakiwa kwenye chama cha mawakili ili aondolewe uwakili wake, na akawajibu "futeni, na mkiweza hata vyeti vya darasa la saba futa"
Imebidi nikupe ufafanuzi ili ujue kwamba watanganyika siyo wajinga, tunajua sababu ni ipi

Au wewe unaweza kutueleza Dr Slaa ana tuhuma zipi?
 
Serikali ilifanya makosa kumkamata kwanza Dr Slaa akiwa na Hadhi ya kibalozi. Hii yamaanisha kuwa kama Dr Slaa angekuwa upande mmoja na wanomtuhumu pengine angepewa nafasi ya Ubalozi katika nchi ingine au angeendelea kufaidi Hadhi hiyo ya kibalozi.

Hivyo bado makosa yaendelea kufanyika endapo Dr Slaa ataendelea kuzongwa na tuhuma zilezile ambazo hazikuwa na uzito kukabiliana na Hadhi yake ya kibalozi.

Mwisho, kuna masuala hapo juu hayana umuhimu sana kutokana na unyeti wake (namba 11) na haki ya faragha (namba 15) na usalama wa Taifa ( namba 13) ni:


7,8, 11, 13,14 na 15

Nakutakia Dominica njema.
 
Kumbukizi Chokozi:

Ila nakumbuka Mkuu ni kama vile uliwahi kutuaga humu?
 
Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi. ...

Mfa maji haachi kutapatapa, ndivyo ilivyo Serikali iliyoko madarakani (utenguaji na uteuzi).

Dr. Slaa, kwa sasa, ni habari kubwa, kwenye siasa nchini. Akisimamishwa kugombea Urais, hakuna wa kumshinda.
 
Jambo linakuwa likishafanyika sheria ndo inafuata kama fulivyoona dpw.
 
Una hoja mkuu, huenda Kidata alivuliwa huo ubalozi kama adhabu tu, hata Slaa ikawa hivyo pia
 
Nimestaafu, Umri wangu miaka 78, Furaha yangu ni asili, mifugo na kilimo. Nipo mashambani naangalia mifugo, nimepumzika, Ghafla mtoto anakuja akiendesha tairi la baiskeli huku ameshika karatasi nyeupe, Naifungua na kuisoma, UDSM wanasema wamenivua Shahada yangu!!..TAFAKURI
 
Mayala ninakuamini sana, wewe ni adimu sana na unapojitolea kusema unasema ukweli, nakumbuka wakati wa mwendazake, watu ndani ya janvi hili walimsema sana akaonekana ni Rais Mbabe hataki kufuata sheria nknk, leo watu wanauona utofauti mkubwa wa uongozi wa Nchi yetu, ukiwasikiliza walio wengi humu wanasema Mama katokota, nashawishika kusema janvi hili linajigawa makundi mawili, kundi linalokuwa fevered kwa upande wake hukaa tuli kama maji ya mtungi, na wanaumia ndo hupiga kelele. uongozi wa Nchi si kazi nyepesi na hajatokea kiongozi aliyefaulu katika uongozi wake akasifiwa na watu wote.
katika hili Mayala aksante kwa kutuelimisha ila wapambe wamuache Mama afanye kazi yake, hata maamuzi mengine kwake siyo ya lazima hana haja ya kupambana na Dr. Slaa, hana sababu naye kwa sababu hana mvuto wowote wa kumsumbua mbeleni, Yeye aconcentrate na kumalizia reli yetu na umeme wetu ikiwezekana hata kuanza miradi mipya mikubwa itakayo tuchelewesha aachane nayo. itazaliwa na kukamilika kwa hii iliyopo.
 
umeeleza vizuri sana tena short and claer.
Haja ya serikali ni kutaka kumkabili na kumdhibiti kisheria mkaidi huyu asie na shukrani bila kuathiri sheria za kimataifa zianazomlinda mtu mwenye hadhi ya balozi.
Pamoja na mambo mengine dr.slaa atapokwa pia diplomatic pasport alokuanayo atapewa ya kiraia, atakaguliwa na kupekuliwa kama raia wa kawaida, mathalani nyumbani kwake au anaposafiri ng"ambo, atakosa fursa za kuongoza mahirika ya kimataifa kwa kukosa endosement ya serikali yake na endapo atapata fursa hiyo kwa kupuuzwa endososment ya nchi yake, basi apewe uongozi for their own risks n.k
 
Asante mkuu.
 
Umetumia maneno mawili “very important”, kwamba Dr Slaa ni mkaidi na asie na shukrani.

Huo ni uthibitisho tosha kwamba mmeona au mwadhani mtamkomoa.

Lakini ukweli halisi ni kwamba Dr Slaa ni tishio (threat) kwenu hivyo mwatumia njia zozote ili kumdhibiti. Kama mmeweza kumdhibiti Job Ndugai na balozi Ali Karume, basi hamtashindwa angalau kujaribu kumdhibiti Dr Slaa.

Pia umeongelea kwamba mtamnyang’anya pasi yake ya kusafiria ya kibalozi. Hii pia haimzuii Dr Slaa kuendelea na maisha yake mengine akiwa raia wa kawaida ikiwemo kusafiri si ataomba viza mwenyewe na kupita geti lisilo la VIP?

Nadhani wafahamu ni nani waliwashauri muwaachie mlipowakamata kule Mbeya.

Kwahiyo mwatakiwa kutafakari kila hatua mnodhani aweza kuchukuliwa Dr Slaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…