Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Watu wengi wa mataifa mengine khasa wazungu ili uweze kumzidi kimaarifa ni uwezo wa kujenga hoja, kuitetea hoja hiyo na pia kuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi hoja yako kwa kutumia mifano mbalimbali.

Wakikuona una sifa hizo kuna mawili, wakuhonge au wakutumie.

Hivyo ukipewa TANESCO utapiga na hata wizara ya nishati utaingia mikataba ya kiupigaji.

Lakini jambo kubwa kabisa ambalo latufanya waafrika tufanye mambo ya ajabu ni “inferiority complex” ambayo yatokana na historia yetu.

Kwahiyo wanasheria tunao, washauri wa serikali au “government advisors” tunao lakini ni watu wa aina gani na wana uwezo gani kuishauri vema serikali inapokwama kwenye mambo yake?

Tukumbuke kuna washauri wa serikali na kuna washauri wa raisi ambao hutakiwa kutoka kila sekta, je wapo?

Wabunge tupo nao ndio usiseme, je unapomteua Mbunge kwenda Dubai ana sifa?

Au kamati husika ya bunge itojadili DP World ina wajumbe wenye uelewa?
 
Mbona alishitakiwa KABLA ya kuvuliwa ubalozi???????? Hii imekaaje
Kesi inayo mwandama Dr Slaa Ni uhaini unaotokana na bandari .alikiuka kiapo chake Cha kuitetea na kuirinda hadhi ya Taifa la Tz Kama lakini Yeye akaisemea vibaya

Haya Ni onavyo Mimi
 
unasema, nakunukuu, 'mmemuona au mwadhani mtamkomoa' Mimi na nani? mie ni mimi nipo mwenyewe na haya ni maoni na mtazamo wangu juu ya hoja iliyotolewa na Paskali.
Hayo ni baadhi ya mambo niyajuavyo kuhusu diplomasia na hivyo ndivyo ninavyodhani serikali inavyomchukulia dr.slaa.

Suala la kua ni threat na kwamba serikali inamkomoa na haiwezi kufua dafu, hayo ni mawazo na mtazamo wako but mzee anaumia na anazidi kuchoka, na kwakweli namuhurumia sana na ninamuombea kwa mwenyezi Mungu aendelee kumkirimia zawadi ya Uhai, Nguvu, Maarifa, Matashi mema, Afya njema Kimwili na Kiroho ili kusudi tuendelee kushuudia namna ambavyo anapambana nasi tuchote maarifa na mbinu ili baadae nasi tushike hatamu za mapambano..

so sihusiki na kundi lolote kwenye mawazo na mtazamo wangu.
 
Mkuu samahani kama nimekukwaza kwa kusema ninyi au vingine kukujumisha maana umeongea kama mtu mwenye "inside knowledge".

Kama raisi ahitaji msaada wa mawazo na uelewa wa masuala mengi yalo juu ya uwezo wake na wale wanomsaidia kwa ushauri basi aruhusu watu kama Dr Slaa wamsaidie kwa kuwa huru kutoa maoni yao.

Ni mmoja wa "think tank" wazuri sana na wangesaidia sana nchi kwenda mbele badala ya kurudi nyuma kutoka uchumi wa kati kwenda uchumi wa kufikirika.
 
Bandiko lako linabielimisha kuwa Jamhuri ilitenda jinai kumkamata Balozi akiwa ktk hadhi yake.

Je sanctions gani za kisheria dhidi ya hili?


Pia, unapindisha kiswahili kuwa kukosoa si kosa. Lakini tumeona wakosoaji wamebimbiwa ihaini. Je unadhani sisi si waelewa?
 
Je, wateuzi wake, ambao pamoja na kufanya kazi kwa niaba yake, wanampa ushauri unaofaa?

Wabobezi wa masuala ya utawala wamethibitisha, pasipo shaka kuwa According to the principle of absolute responsibility (e.g. the President by the Constitution), authority can be delegated but responsibility and accountability cannot be delegated

Hivyo mhusika ababe msalaba wake tu kwa Katiba ya nchi aliyoapa kuitetea na kuilinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…