Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wengi wa mataifa mengine khasa wazungu ili uweze kumzidi kimaarifa ni uwezo wa kujenga hoja, kuitetea hoja hiyo na pia kuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi hoja yako kwa kutumia mifano mbalimbali.Hivi sisi hatuna mwanasheria mkuu? Hatuna inside political analysts and advisers? Au washauri wetu wako nje ya mfumo? Mbona vitu vinafanyika halafu vinakuja kuonekana sheria zimekiukwa then unasikia mabadiliko.
Chukua mfano wa suala la ukodishwaji wa bandari. Tunapeleka timu ya wabunge dubai kujifunza na kuona uendeshaji wa DPW, tunarudi bungeni kuja kuridhia mkataba ambao ulishasainiwa tangu mwaka jana! Mfano Bunge lingesema (unless ilishapangwa) tubadilishe baadhi ya vipengele, ingekuwaje?
Suala hili hili tena, mkataba umeshasainiwa lakini tukajikuta kumbe kuna sheria ya ulinzi wa rasilimali inakinzana na baadhi ya vipengele vya mkataba.
Turudi kwenye mada, Dr Slaa amekamatwa na kushitakiwa kwa uhaini, tunakuja kugundua baadae kumbe alikuwa na hadhi ya ubalozi na alitakiwa avuliwe kwanza! Hatukuwa na watu wa kuyaona haya? Wewe umesoma sheria, au inatumika reversal kwa mtu kujipinga mwenyewe baada ya kutoa maamuzi ya awali?
Mbona alishitakiwa KABLA ya kuvuliwa ubalozi???????? Hii imekaajeWanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.
Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya Ubalozi ni kwasababu ya ukosoaji wake wa mkataba wa DPW na Bandari zetu.
Kwanza naomba ifahamike wazi, hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote, mwenye hadhi yoyote, kufanya ukosoaji wowote, wa jambo lolote, as long as ukosoaji huo haukiuki sheria yoyote.
Hivyo Dr. Wilbroad Slaa ana haki ya kukosoa jambo lolote kama ilivyotolewa na ibara ya 18 ya Katiba yetu kwenye freedom of speech and expression.
Ubalozi ni hadhi ya kimataifa inayoendana na rights na privileges fulani fulani zikiandamana na immunities, hivyo ubalozi una masharti ya kufuatwa mtu unapokuwa Balozi na kuna vitu hutakiwi kuvifanya.
Hili ni bandiko elimishi kuhusu
Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr.Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?
Miongoni mwa privileges na immunities za diplomatic status ni pamoja na kinga ya kibalozi, ya kutokushitakiwa popote kwa kosa la jinai.
Mtu yoyote mwenye hadhi ya Ubalozi akitenda jinai yoyote, kabla hajapandishwa mahakamani kushitakiwa, hatua ya kwanza ni kuvuliwa kwanza hadhi ya Ubalozi, ndipo aweze kushitakika kwasababu hadhi ya Ubalozi ina kinga ya kibalozi kutokushitakiwa.
Kuna msemo wa Kiswahili usemao, ukiona zinduna, ujue ambari iko nyuma!, au dalili ya mvua ni mawingu na panapo fuka moshi chini kuna moto!.
Kuvuliwa huku Ubalozi kwa Dr. Slaa ni Zinduna, ni mawingu, ni kufuka tuu kwa moshi, ajiandae kuipokea Ambari, kujikinga na mvua na kuuzima moto unaokuja.
Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mwenye hadhi ya Ubalozi kuvuliwa hadhi hiyo, wa kwanza ni balozi wetu wa kwanza jijini London nchini Uingereza Balozi Christopher Kasanga Tumbo, alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwa jinai enzi za Nyerere. Mwingine ni Balozi Antony Pastor Ngaiza alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982. Pia Balozi Prof. Costa Rick Mahalu akivuliwa hadhi ya Ubalozi na kushitakiwa kwa uhujumu ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania jijini Rome nchini Italy, alliposhinda kesi na kukutwa hana hatia, alirejeshewa Ubalozi wake.
.
Hivyo hata kwa Dr. Slaa, tusubirie yatokanayo na kufutiwa hadhi hii ya Ubalozi, yakishindwa kuthibitishwa, anarejeshewa Ubalozi wake.
Kwa vile hili ni bandiko elimishi, nitakuelimisha kidongo na kwa kifupi
Kufuatia hii topic ni topic ndefu hivyo nakwenda nayo mdogo mdogo, saa hizi nawahi misa ya kwanza, baada ya misa nitaikamilisha
- Hadhi ya Ubalozi ni nini?
- Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi?
- Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa.
- Privileges za diplomatic status ni zipi?.
- Ijue diplomatic immunity
- Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?
- Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi?
- Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi
- Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi?
- Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?.
- Ijue diplomatic Bag?
- Jee mwenye diplomatic status ni Balozi?.
- Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats?
- Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc.
- Wajue Wafanya Biashara Matajiri wenye diplomatic status na sio mabalozi!
Itaendelea...
Paskali
Mwandishi ni mwana habari aliyefanya kazi ubalozi fulani kwa miaka 4, ila kufutia fani yake ya uandishi wa habari, ametembelea Balozi za Tanzania katika nchi nyingi za Africa, Ulaya. Asia na America.
Ulinyooka!Ndiyo wewe na wenzako wapigania matumbo hapo chato
Ndoto za alinacha kwa upinzani gani wa kuing'oa ccm!Ingawa sina huruma na Slaa kwa uhuni aliotufanyia wana UKAWA lkn kumfungulia kesi ya ugaidi ccm watakuwa wanajichimbia kaburi
Sasa ni zamu ya wazalendo nyinyi sukuma gang mtakufa kwa njaaUlinyooka!
Hata jiwe alikuwa anasema hivyo kilichomtokea ni umautiNdoto za alinacha kwa upinzani gani wa kuing'oa ccm!
unasema, nakunukuu, 'mmemuona au mwadhani mtamkomoa' Mimi na nani? mie ni mimi nipo mwenyewe na haya ni maoni na mtazamo wangu juu ya hoja iliyotolewa na Paskali.Umetumia maneno mawili “very important”, kwamba Dr Slaa ni mkaidi na asie na shukrani.
Huo ni uthibitisho tosha kwamba mmeona au mwadhani mtamkomoa.
Lakini ukweli halisi ni kwamba Dr Slaa ni tishio (threat) kwenu hivyo mwatumia njia zozote ili kumdhibiti. Kama mmeweza kumdhibiti Job Ndugai na balozi Ali Karume, basi hamtashindwa angalau kujaribu kumdhibiti Dr Slaa.
Pia umeongelea kwamba mtamnyang’anya pasi yake ya kusafiria ya kibalozi. Hii pia haimzuii Dr Slaa kuendelea na maisha yake mengine akiwa raia wa kawaida ikiwemo kusafiri si ataomba viza mwenyewe na kupita geti lisilo la VIP?
Nadhani wafahamu ni nani waliwashauri muwaachie mlipowakamata kule Mbeya.
Kwahiyo mwatakiwa kutafakari kila hatua mnodhani aweza kuchukuliwa Dr Slaa.
Kuna kesi inaendelea kwa kosa alilolifanya?Uhuru wa kueleza maoni yako yanamipaka mkuu sasa huyu Dkt alivuka mipaka lugha aliyokuwa anaitumia haina staha Wala adabu kwa Mkuu wa Nchi
Mkuu samahani kama nimekukwaza kwa kusema ninyi au vingine kukujumisha maana umeongea kama mtu mwenye "inside knowledge".unasema, nakunukuu, 'mmemuona au mwadhani mtamkomoa' Mimi na nani? mie ni mimi nipo mwenyewe na haya ni maoni na mtazamo wangu juu ya hoja iliyotolewa na Paskali.
Hayo ni baadhi ya mambo niyajuavyo kuhusu diplomasia na hivyo ndivyo ninavyodhani serikali inavyomchukulia dr.slaa.
Suala la kua ni threat na kwamba serikali inamkomoa na haiwezi kufua dafu, hayo ni mawazo na mtazamo wako but mzee anaumia na anazidi kuchoka, na kwakweli namuhurumia sana na ninamuombea kwa mwenyezi Mungu aendelee kumkirimia zawadi ya Uhai, Nguvu, Maarifa, Matashi mema, Afya njema Kimwili na Kiroho ili kusudi tuendelee kushuudia namna ambavyo anapambana nasi tuchote maarifa na mbinu ili baadae nasi tushike hatamu za mapambano..
so sihusiki na kundi lolote kwenye mawazo na mtazamo wangu.
Kuna kesi inaendelea kwa kosa alilolifanya
Bandiko lako linabielimisha kuwa Jamhuri ilitenda jinai kumkamata Balozi akiwa ktk hadhi yake.Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.
Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya Ubalozi ni kwasababu ya ukosoaji wake wa mkataba wa DPW na Bandari zetu.
Kwanza naomba ifahamike wazi, hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote, mwenye hadhi yoyote, kufanya ukosoaji wowote, wa jambo lolote, as long as ukosoaji huo haukiuki sheria yoyote.
Hivyo Dr. Wilbroad Slaa ana haki ya kukosoa jambo lolote kama ilivyotolewa na ibara ya 18 ya Katiba yetu kwenye freedom of speech and expression.
Ubalozi ni hadhi ya kimataifa inayoendana na rights na privileges fulani fulani zikiandamana na immunities, hivyo ubalozi una masharti ya kufuatwa mtu unapokuwa Balozi na kuna vitu hutakiwi kuvifanya.
Hili ni bandiko elimishi kuhusu
Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr.Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?
Miongoni mwa privileges na immunities za diplomatic status ni pamoja na kinga ya kibalozi, ya kutokushitakiwa popote kwa kosa la jinai.
Mtu yoyote mwenye hadhi ya Ubalozi akitenda jinai yoyote, kabla hajapandishwa mahakamani kushitakiwa, hatua ya kwanza ni kuvuliwa kwanza hadhi ya Ubalozi, ndipo aweze kushitakika kwasababu hadhi ya Ubalozi ina kinga ya kibalozi kutokushitakiwa.
Kuna msemo wa Kiswahili usemao, ukiona zinduna, ujue ambari iko nyuma!, au dalili ya mvua ni mawingu na panapo fuka moshi chini kuna moto!.
Kuvuliwa huku Ubalozi kwa Dr. Slaa ni Zinduna, ni mawingu, ni kufuka tuu kwa moshi, ajiandae kuipokea Ambari, kujikinga na mvua na kuuzima moto unaokuja.
Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mwenye hadhi ya Ubalozi kuvuliwa hadhi hiyo, wa kwanza ni balozi wetu wa kwanza jijini London nchini Uingereza Balozi Christopher Kasanga Tumbo, alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwa jinai enzi za Nyerere. Mwingine ni Balozi Antony Pastor Ngaiza alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982. Pia Balozi Prof. Costa Rick Mahalu akivuliwa hadhi ya Ubalozi na kushitakiwa kwa uhujumu ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania jijini Rome nchini Italy, alliposhinda kesi na kukutwa hana hatia, alirejeshewa Ubalozi wake.
.
Hivyo hata kwa Dr. Slaa, tusubirie yatokanayo na kufutiwa hadhi hii ya Ubalozi, yakishindwa kuthibitishwa, anarejeshewa Ubalozi wake.
Kwa vile hili ni bandiko elimishi, nitakuelimisha kidongo na kwa kifupi
- Hadhi ya Ubalozi ni nini?
- Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi?
- Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa.
- Privileges za diplomatic status ni zipi?.
- Ijue diplomatic immunity
- Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?
- Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi?
- Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi
- Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi?
- Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?.
- Ijue diplomatic Bag?
- The Doctrine of Diplomatic Reciprocity
- Jee mwenye diplomatic status ni Balozi?.
- Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats?
- Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc.
- Wajue Wafanya Biashara Matajiri wenye diplomatic status na sio mabalozi!
Paskali
Mwandishi ni mwana habari aliyefanya kazi ubalozi fulani kwa miaka 4, ila kufutia fani yake ya uandishi wa habari, ametembelea Balozi za Tanzania katika nchi nyingi za Africa, Ulaya. Asia na America.
ItakiwaKwahiyo wewe ndiye mshauri wa rais wa JMT?
Eeehhee....Mimi ni mtu wa mastori mastori, sasa ni mastori mastori ya visa na mikasa iliyonikuta ubalozini kwetu kwenye nchi mbalimbali ikiwemo kisa cha ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam.
Je, wateuzi wake, ambao pamoja na kufanya kazi kwa niaba yake, wanampa ushauri unaofaa?...
Mama afanye kazi yake, hata maamuzi mengine kwake siyo ya lazima hana haja ya kupambana na Dr. Slaa, hana sababu naye kwa sababu hana mvuto wowote wa kumsumbua mbeleni, Yeye aconcentrate na kumalizia reli yetu na umeme wetu ikiwezekana hata kuanza miradi mipya mikubwa itakayo tuchelewesha aachane nayo. itazaliwa na kukamilika kwa hii iliyopo.
Ishi wewe milele lakini kuitoa ccm miaka elfuHata jiwe alikuwa anasema hivyo kilichomtokea ni umauti
Ubalozi wa Marekani siku hizi hawana shida sana kama zamani.Mimi ni mtu wa mastori mastori, sasa ni mastori mastori ya visa na mikasa iliyonikuta ubalozini kwetu kwenye nchi mbalimbali ikiwemo kisa cha ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam.
Nakuonea huruma wewe chawa wa jiweIshi wewe milele lakini kuitoa ccm miaka elfu