stonecutter
JF-Expert Member
- Jun 12, 2022
- 1,724
- 2,584
Naona tupo pamoja kwenye baadhi ya mambo ya msinginaunga mkono hoja, nothing is impossible under the sun, hivyo lolote linawezekana.
P
Mkuu P, hakuna mahali nimeongelea suala la Bandari na ukosoaji wake.Mkuu Jidu, hakuna demage control yoyote, hapa ni uendeshaji umma tuu, kuna watu wanadhani kafutiwa ubalozi kwa ukosoaji wa mkataba wa DPW na Bandari zetu, hakuna mkosoaji mkubwa kama Balozi Prof. Anna Tibaijuka!, na hakuna kosa lolote kukosoa jambo lolote Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!
P
Zile privileges baadhi ni only ukiwa kazini, maana yake ukiwa on duty, ukisha staafu baadhi zinaondolewa na nyingine ni for life, mfano diplomatic passport na kupitia VIP ni for life, ile diplomatic immunity ya kutokamatwa na kushitakiwa ni for life, ila ile privileges ya kulipwa foreign allowances zinaondolewa, dependants kulipiwa international School, inaondolewa na kununua vitu tax free kunaisha, na kutembelea plate number ya ubalozi kuna keisha, wanaondelea na privilege hiyo ni wale wabunge wa EALA.Paskali,umetoa darasa zuri Sana uzidi kutoa elimu Kama hizi siku zijazo.
Lakini nina swali moja,hizi diplomatic immunities na benefits ni wakati ukiwa kazini au kwa maisha yao yote.
Hakuhusiani na ukosoaji, hakuna critic mkubwa wa mkataba wa DPW na Bandari zetu kama Prof. Tibaijuka, kama ni kufutiwa ubalozi kwa ukosoaji, Tiba angefutiwa!.
Hiyo why him utaijua soon kwa yatokanayo.
yes naunga mkono hoja
Sii kweli, waoga wapo na ma bold tupo!.
Naomba niyaheshimu mawazo yako hata kama sikubaliani nayo.
Asante
P
Viongozi wakuu wote wa UN Agencies wana hadhi ya ubalozi by virtue of their positions hivyo ni Mabalozi!.Tibaijuka, I suppose you meant Anna. To the best of my knowledge, hajawahi kuwa Balozi Wa kuteuliwa na JMT. Balozi alikuwa mume wake ambaye alishatangulia mbele ya haki.
i stand to be corrected.
But, hakuteuliwa na Rais wa JMT huo Ubalozi, hivyo nadhani Rais wa JMT hawezi muondolea hiyo hadhi. I stand to be correctedViongozi wakuu wote wa UN Agencies ni Mabalozi
P
Hizi mbwela mbwela zako wakati wa utawala wa Jiwe ulifumba mdomo wako kama mbwa koko na mkia kuitia ndani .Huyu Mama munamchezea sana aah waswahili bana chakula cha simba tu lkn fitna zako hazifui dafu peleka mahkamani basi kesi yake na wewe umsimamie zaibala chorni.Mimi sio mshauri wa yoyote, ni mtu tuu mwenye ufahahamu wa issues za kidplomasia hivyo kujitolea kuelimisha watu humu kuhusu mtu kufutiwa hadhi ya Ubalozi Hakutokani na Ukosoaji, bali kufutiwa kule ni Zinduna tuu, Ambari iko nyuma...
P
Kuwa kabisa mzee wa kanisa mkuuNi topic ndefu hivyo nakwenda nayo mdogo mdogo, saa hizi nawahi misa ya kwanza, baada ya misa nitaikamilisha
P
No, kwa vile najiandaa kuanzisha kanisa langu, siwezi kuwa Mzee wa kanisa ili kutakapoanza nisinyoonyeshewe vidole vya uasi!.Kuwa kabisa mzee wa kanisa mkuu
Uwezi amini mzee ila kiukweli ukija na agenda kamaNo, kwa vile najiandaa kuanzisha kanisa langu, siwezi kuwa Mzee wa kanisa ili kutakapoanza nisinyoonyeshewe vidole vya uasi!.
P
Litakuwa ni kanisa la African Scientology Church, tutachukua mazuri ya dini za asili ikiwemo kuoa wanawake wengi, na kuzi blend na Agano la kale na agano jipya. Uongo wa wazungu tutaachana nao.Uwezi amini mzee ila kiukweli ukija na agenda kama
Pascally Mayalla kuwaponya wajane dhidi ya ujane
Pascally Mayalla na kanisa la wamama
Pascally mayala jibu la wanasiasa wasaliti wa utu.
Kanisa litafanikiwa
Umetisha🤣🤣🤣🤣Litakuwa ni kanisa la African Scientology Church, tutachukua mazuri ya dini za asili ikiwemo kuoa wanawake wengi, na kuzi blend na Agano la kale na agano jipya. Uongo wa wazungu tutaachana nao.
P
Nitaanza na ujumbe huuUwezi amini mzee ila kiukweli ukija na agenda kama
Pascally Mayalla kuwaponya wajane dhidi ya ujane
Pascally Mayalla na kanisa la wamama
Pascally mayala jibu la wanasiasa wasaliti wa utu.
Kanisa litafanikiwa
Mkuu chipa GM , karibu mitaa hii ukimaliza karibu darasa langu Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake? haya mambo ya diplomasia pia nimeyaongea hapa Membe amejuaje Contents za 'Diplomatic Bag'? Uwezo kukanusha kaupata wapi? - Tusidanganyane!Mi binafsi nilikuwa namkubali sana pasco japokuwa tunatofautiana mitazamo ya vyama vya siasa mi in chadema yeye ni km Kwa magamba., but nilimdharau sana pasco alipo mtetea Steven masele na kumuita shujaa wa kisukuma., nilishangaa sana inamaana pasco hajui mambo ya diplomatic, au immunity granted to the ambassador na mambo ya foreign affairs., huwezi kumdis balozi kitoto vile bungeni alafu ukaitwa shujaa wa kisukuma. Pasco ulitutukana sana sisi wasukuma kwamba ni mashujaa wa kulopoka. Alichofanya masele ule ni ulopokaji.,not hero that was stupi..dness
Mkuu mwaka umepita hakuna muendelezo.Mkuu chipa GM , karibu mitaa hii ukimaliza karibu darasa langu Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake? haya mambo ya diplomasia pia nimeyaongea hapa Membe amejuaje Contents za 'Diplomatic Bag'? Uwezo kukanusha kaupata wapi? - Tusidanganyane!
P
Andiko zuri saanaa.Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.
Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya Ubalozi ni kwasababu ya ukosoaji wake wa mkataba wa DPW na Bandari zetu.
Kwanza naomba ifahamike wazi, hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote, mwenye hadhi yoyote, kufanya ukosoaji wowote, wa jambo lolote, as long as ukosoaji huo haukiuki sheria yoyote.
Hivyo Dr. Wilbroad Slaa ana haki ya kukosoa jambo lolote kama ilivyotolewa na ibara ya 18 ya Katiba yetu kwenye freedom of speech and expression.
Ubalozi ni hadhi ya kimataifa inayoendana na rights na privileges fulani fulani zikiandamana na immunities, hivyo ubalozi una masharti ya kufuatwa mtu unapokuwa Balozi na kuna vitu hutakiwi kuvifanya.
Hili ni bandiko elimishi kuhusu
Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr.Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?
Miongoni mwa privileges na immunities za diplomatic status ni pamoja na kinga ya kibalozi, ya kutokushitakiwa popote kwa kosa la jinai.
Mtu yoyote mwenye hadhi ya Ubalozi akitenda jinai yoyote, kabla hajapandishwa mahakamani kushitakiwa, hatua ya kwanza ni kuvuliwa kwanza hadhi ya Ubalozi, ndipo aweze kushitakika kwasababu hadhi ya Ubalozi ina kinga ya kibalozi kutokushitakiwa.
Kuna msemo wa Kiswahili usemao, ukiona zinduna, ujue ambari iko nyuma!, au dalili ya mvua ni mawingu na panapo fuka moshi chini kuna moto!.
Kuvuliwa huku Ubalozi kwa Dr. Slaa ni Zinduna, ni mawingu, ni kufuka tuu kwa moshi, ajiandae kuipokea Ambari, kujikinga na mvua na kuuzima moto unaokuja.
Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mwenye hadhi ya Ubalozi kuvuliwa hadhi hiyo, wa kwanza ni balozi wetu wa kwanza jijini London nchini Uingereza Balozi Christopher Kasanga Tumbo, alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwa jinai enzi za Nyerere. Mwingine ni Balozi Antony Pastor Ngaiza alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982. Pia Balozi Prof. Costa Rick Mahalu akivuliwa hadhi ya Ubalozi na kushitakiwa kwa uhujumu ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania jijini Rome nchini Italy, alliposhinda kesi na kukutwa hana hatia, alirejeshewa Ubalozi wake.
.
Hivyo hata kwa Dr. Slaa, tusubirie yatokanayo na kufutiwa hadhi hii ya Ubalozi, yakishindwa kuthibitishwa, anarejeshewa Ubalozi wake.
Kwa vile hili ni bandiko elimishi, nitakuelimisha kidongo na kwa kifupi
Paskali
- Hadhi ya Ubalozi ni nini?
- Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi?
- Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa.
- Privileges za diplomatic status ni zipi?.
- Ijue diplomatic immunity
- Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?
- Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi?
- Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi
- Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi?
- Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?.
- Ijue diplomatic Bag?
- The Doctrine of Diplomatic Reciprocity
- Jee mwenye diplomatic status ni Balozi?.
- Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats?
- Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc.
- Wajue Wafanya Biashara Matajiri wenye diplomatic status na sio mabalozi!
Mwandishi ni mwana habari aliyefanya kazi ubalozi fulani kwa miaka 4, as a local staff na kufutia fani yake ya uandishi wa habari, ametembelea Balozi za Tanzania katika nchi nyingi za Africa, Ulaya. Asia na America, atawaletea visa na mikasa mbalimbali ya balozi zetu mbalimbali