Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.
Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya Ubalozi ni kwasababu ya ukosoaji wake wa mkataba wa DPW na Bandari zetu.
Kwanza naomba ifahamike wazi, hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote, mwenye hadhi yoyote, kufanya ukosoaji wowote, wa jambo lolote, as long as ukosoaji huo haukiuki sheria yoyote.
Hivyo Dr. Wilbroad Slaa ana haki ya kukosoa jambo lolote kama ilivyotolewa na ibara ya 18 ya Katiba yetu kwenye freedom of speech and expression.
Ubalozi ni hadhi ya kimataifa inayoendana na rights na privileges fulani fulani zikiandamana na immunities, hivyo ubalozi una masharti ya kufuatwa mtu unapokuwa Balozi na kuna vitu hutakiwi kuvifanya.
Hili ni bandiko elimishi kuhusu
Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr.Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?
Miongoni mwa privileges na immunities za diplomatic status ni pamoja na kinga ya kibalozi, ya kutokushitakiwa popote kwa kosa la jinai.
Mtu yoyote mwenye hadhi ya Ubalozi akitenda jinai yoyote, kabla hajapandishwa mahakamani kushitakiwa, hatua ya kwanza ni kuvuliwa kwanza hadhi ya Ubalozi, ndipo aweze kushitakika kwasababu hadhi ya Ubalozi ina kinga ya kibalozi kutokushitakiwa.
Kuna msemo wa Kiswahili usemao, ukiona zinduna, ujue ambari iko nyuma!, au dalili ya mvua ni mawingu na panapo fuka moshi chini kuna moto!.
Kuvuliwa huku Ubalozi kwa Dr. Slaa ni Zinduna, ni mawingu, ni kufuka tuu kwa moshi, ajiandae kuipokea Ambari, kujikinga na mvua na kuuzima moto unaokuja.
Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mwenye hadhi ya Ubalozi kuvuliwa hadhi hiyo, wa kwanza ni balozi wetu wa kwanza jijini London nchini Uingereza Balozi Christopher Kasanga Tumbo, alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwa jinai enzi za Nyerere. Mwingine ni Balozi Antony Pastor Ngaiza alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982. Pia Balozi Prof. Costa Rick Mahalu akivuliwa hadhi ya Ubalozi na kushitakiwa kwa uhujumu ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania jijini Rome nchini Italy, alliposhinda kesi na kukutwa hana hatia, alirejeshewa Ubalozi wake.
.
Hivyo hata kwa Dr. Slaa, tusubirie yatokanayo na kufutiwa hadhi hii ya Ubalozi, yakishindwa kuthibitishwa, anarejeshewa Ubalozi wake.
Kwa vile hili ni bandiko elimishi, nitakuelimisha kidongo na kwa kifupi
- Hadhi ya Ubalozi ni nini?
- Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi?
- Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa.
- Privileges za diplomatic status ni zipi?.
- Ijue diplomatic immunity
- Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?
- Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi?
- Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi
- Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi?
- Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?.
- Ijue diplomatic Bag?
- The Doctrine of Diplomatic Reciprocity
- Jee mwenye diplomatic status ni Balozi?.
- Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats?
- Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc.
- Wajue Wafanya Biashara Matajiri wenye diplomatic status na sio mabalozi!
Paskali
Mwandishi ni mwana habari aliyefanya kazi ubalozi fulani kwa miaka 4, as a local staff na kufutia fani yake ya uandishi wa habari, ametembelea Balozi za Tanzania katika nchi nyingi za Africa, Ulaya. Asia na America, atawaletea visa na mikasa mbalimbali ya balozi zetu mbalimbali