Ijue Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na Wajumbe wake

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Leo katika kujifunza masuala ya siasa, ningepeda kuwaelezea kuhusu NEC ya CCM. Kuna watu wengi hawaijui na hawawajui wajumbe wake. Baada ya marekebisho madogo ya katiba ya CCM kumekuwa na ongezeko la viti.

Ngoja nianze kulingana na KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa na wajumbe wafuatao:-

(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Makamu mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
(c) Makamu mwenyekiti wa CCM (Bara)
(d) Katibu Mkuu wa CCM
(e) Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana na CCM.
(f) Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM.
(g) Manaibu wa Katibu Mkuu wa CCM
(h) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaotokana na CCM.
(i) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni.
(j) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.
(k) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
(l) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.
(m) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa kila Jumuiya ya CCM
(n) Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM
(o) Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.
(p) Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anaye tokana na CCM, na Spika wa Baraza la Wawakilishi anayetokana na CCM
(q) Wenyeviti wote wa CCM wa Mikoa.
(r) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa mmoja kutoka kila mkoa wa Tanzania Bara na wanne kutoka kila mkoa wa Zanzibar waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Mkoa.
(s) Wajumbe ishirini kutoka Tanzania Bara na Wajumbe ishirini kutoka Zanzibar waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kutoka Orodha ya Taifa.
(t) Wajumbe watano kutoka kila Jumuiya ya CCM, waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Jumuiya.
(u) Wajumbe kumi waliochaguliwa na Halmashauri kuu ya Taifa kutokana na mapendekezo ya Mwenyekiti wa CCM.
(v) Wajumbe watano waliochaguliwa na Wabunge wote wa CCM.
(w) Wajumbe watatu waliochaguliwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM kutoka miongoni mwao.

Tujadili sasa.......
 
UTARATIBU WA KUFANYA MIKUTANO

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja katika kila miezi sita (6),
lakini inaweza kufanya mkutano usiokuwa wa kawaida wakati wowote endapo itatokea haja ya kufanya hivyo au kwa maagizo ya kikao cha juu.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa utakaofanyika katika kipindi cha miezi sita ya mwisho wa kila mwaka utakuwa pia na kazi maalum ya kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM unaofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka wa fedha uliopita wa Serikali hizo ambao ulimalizika tarehe 30 Juni ya mwaka unaohusika.
 
CCM DEMOKRASIA NI KUBWA

Katika mikutano yote ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, uamuzi utafikiwa kwa makubaliano ya jumla, au kwa wingi wa kura za Wajumbe waliohudhuria na kupiga kura.
Lakini ukitokea uamuzi unaohitajika kutolewa kuhusu vyombo vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au vyombo vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au kuhusu muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
uamuzi huo ni lazima upitishwe kwa azimio lililoungwa mkono na theluthi mbili ya kura za Wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya kura za Wajumbe kutoka Zanzibar.
 
Demokrasia ya kuchagua Mtu na kibuli dunia ya leo?
 
CCM NI MFUMO SIYO MTU

Mwenyekiti wa CCM atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, lakini Mwenyekiti wa CCM asipoweza kuhudhuria, mmoja wa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM atakuwa Mwenyekiti wa muda wa Mkutano huo.
 
Sasa kaa mkao wa kula maana nakuletea Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM wa Taifa
 
Leo katika kujifunza masuala ya siasa, ningepeda kuwaelezea kuhusu NEC ya CCM. Kuna watu wengi hawaijui na hawawajui wajumbe wake. Baada ya marekebisho madogo ya katiba ya CCM kumekuwa na ongezeko la viti.

Ngoja nianze kulingana na KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa na wajumbe wafuatao:-

(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Makamu mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
(c) Makamu mwenyekiti wa CCM (Bara)
(d) Katibu Mkuu wa CCM
(e) Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana na CCM.
(f) Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM.
(g) Manaibu wa Katibu Mkuu wa CCM
(h) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaotokana na CCM.
(i) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni.
(j) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.
(k) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
(l) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.
(m) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa kila Jumuiya ya CCM
(n) Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM
(o) Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.
(p) Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anaye tokana na CCM, na Spika wa Baraza la Wawakilishi anayetokana na CCM
(q) Wenyeviti wote wa CCM wa Mikoa.
(r) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa mmoja kutoka kila mkoa wa Tanzania Bara na wanne kutoka kila mkoa wa Zanzibar waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Mkoa.
(s) Wajumbe ishirini kutoka Tanzania Bara na Wajumbe ishirini kutoka Zanzibar waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kutoka Orodha ya Taifa.
(t) Wajumbe watano kutoka kila Jumuiya ya CCM, waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Jumuiya.
(u) Wajumbe kumi waliochaguliwa na Halmashauri kuu ya Taifa kutokana na mapendekezo ya Mwenyekiti wa CCM.
(v) Wajumbe watano waliochaguliwa na Wabunge wote wa CCM.
(w) Wajumbe watatu waliochaguliwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM kutoka miongoni mwao.

Tujadili sasa.......
Sasa G na B mbona ni mtu mmoja au kwenye kura anapiga mara mbili
 
Wakristo wasisahulike tu

Kwa maana walivyofanyiwa kwenye chaguzi za mikoa, wilaya na jumuiya si haki
 
Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa zitakuwa zifuatazo:-
(1) Kutoa uongozi wa Siasa ya CCM kwa jumla kwa Tanzania nzima. Kwa hiyo itakuwa na uwezo wa kubuni, kujadili, kuamua na kutoa Miongozo ya Siasa ya CCM katika mambo mbalimbali.

(2) Kueneza Itikadi na Siasa ya CCM, kuongoza mafunzo ya Siasa ya CCM na kukuza nadharia na Itikadi ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea.

(3) Kuongoza na kusimamia ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea nchini.

(4) Kuandaa Ilani ya CCM ya Uchaguzi na kutoa msukumo wa utekelezaji wa Ilani hiyo.

(5) Kufikisha maazimio na maagizo ya CCM katika Mikoa na kufikiria na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo kutoka vikao vya CCM vya chini.

(6) Kuona kwamba shughuli za Maendeleo na za Ulinzi na Usalama wa Taifa zinazingatiwa.

(7) Kuandaa mikakati na mbinu za kampeni za uchaguzi na kampeni nyinginezo za kitaifa.

(8) Kudumisha uangalizi juu ya vitendo vya Wanachama na Viongozi wa CCM na endapo itadhihirika kwamba tabia na mwenendo wa Mwanachama fulani vinamwondolea sifa za Uanachama au Uongozi itakuwa na uwezo wa kumwachisha au kumfukuza Uanachama au Uongozi alionao. Kuhusu mtu aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ndiyo itakayokuwa na uwezo wa mwisho wa kumrudishia Uanachama wake kwa mujibu wa Katiba, endapo itaridhika kuwa amejirekebisha.

(9) Kuziongoza Halmashauri Kuu za CCM za Mikoa kuhusu vitendo na njia zinazofaa za kuimarisha CCM na za kuleta maendeleo.

(10) Kuandaa Katiba, Kanuni na kuweka taratibu za kuongoza shughuli mbalimbali za CCM.

(11) Kuandaa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa.

Inaendelea......
 
Back
Top Bottom