Ijue Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na Wajumbe wake

Ijue Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na Wajumbe wake

(13) Kujaza kwa niaba ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa, nafasi za uongozi zitakazokuwa wazi, isipokuwa ya Mwenyekiti wa CCM na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM.

(14) Kuunda Kamati au Tume kwa shughuli maalum bila kuathiri majukumu ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.

(15) Kupokea na kujadili taarifa za Tume na Kamati Maalum za CCM, Kamati ya Wabunge wa CCM, na Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.

(16) Kuweka kiwango cha kiingilio katika CCM, ada za Uanachama na michango maalum.

(17) Kusimamisha kwa maslahi ya CCM utumiaji wa kifungu chochote cha Katiba ya CCM au kuruhusu kifungu kutumika kabla ya kuingizwa ndani ya Katiba. Uamuzi huo sharti uungwe mkono na theluthi mbili ya Wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili za Wajumbe kutoka Zanzibar. Hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafikisha uamuzi wake mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa uamuzi wa mwisho.

(18) Kushughulikia uhusiano kati ya CCM na Jumuiya mbalimbali za wananchi na kuziorodhesha Jumuiya za CCM.

(19) Kutengeneza na kurekebisha Muundo wa CCM katika maeneo na nyanja mbalimbali kwa kadri itakavyoonekana inafaa.

(20) Kumsimamisha Mwenyekiti wa CCM au Makamu Mwenyekiti wa CCM iwapo mwenendo na utendaji wake wa kazi vinamwondolea sifa za uongozi. Hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafikisha mapendekezo yake mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa uamuzi wa mwisho.

(21) Kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.

(22) Kuunda Kamati ya Usalama na Maadili.

(23) Kuidhinisha Kanuni za Kamati za Wabunge wote wa CCM, Wawakilishi wote wa CCM, Madiwani wote wa CCM; Katiba/Kanuni za Jumuiya za CCM na kuidhinisha marekebisho ya Katiba/ Kanuni hizo.

(24) Halmashauri Kuu ya Taifa yaweza kukasimu madaraka yake kwa Kamati Kuu kuhusu utekelezaji wa kazi zake kwa kadri itakavyoona inafaa.

Maandishi makubwa kama tuna matatizo ya macho
 
UTARATIBU WA KUFANYA MIKUTANO

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja katika kila miezi sita (6),
lakini inaweza kufanya mkutano usiokuwa wa kawaida wakati wowote endapo itatokea haja ya kufanya hivyo au kwa maagizo ya kikao cha juu.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa utakaofanyika katika kipindi cha miezi sita ya mwisho wa kila mwaka utakuwa pia na kazi maalum ya kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM unaofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka wa fedha uliopita wa Serikali hizo ambao ulimalizika tarehe 30 Juni ya mwaka unaohusika.
Utekelezaji wa serikali inaongozwa/inayotokana na CCM. Ikitokea chama kingine kikachukua nchi ,agenda za mkutano zitapungua
 
Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa zitakuwa zifuatazo:-
(1) Kutoa uongozi wa Siasa ya CCM kwa jumla kwa Tanzania nzima. Kwa hiyo itakuwa na uwezo wa kubuni, kujadili, kuamua na kutoa Miongozo ya Siasa ya CCM katika mambo mbalimbali.


(2) Kueneza Itikadi na Siasa ya CCM, kuongoza mafunzo ya Siasa ya CCM na kukuza nadharia na Itikadi ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea.

(3) Kuongoza na kusimamia ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea nchini.

(4) Kuandaa Ilani ya CCM ya Uchaguzi na kutoa msukumo wa utekelezaji wa Ilani hiyo.

(5) Kufikisha maazimio na maagizo ya CCM katika Mikoa na kufikiria na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo kutoka vikao vya CCM vya chini.

(6) Kuona kwamba shughuli za Maendeleo na za Ulinzi na Usalama wa Taifa zinazingatiwa.

(7) Kuandaa mikakati na mbinu za kampeni za uchaguzi na kampeni nyinginezo za kitaifa.

(8) Kudumisha uangalizi juu ya vitendo vya Wanachama na Viongozi wa CCM na endapo itadhihirika kwamba tabia na mwenendo wa Mwanachama fulani vinamwondolea sifa za Uanachama au Uongozi itakuwa na uwezo wa kumwachisha au kumfukuza Uanachama au Uongozi alionao. Kuhusu mtu aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ndiyo itakayokuwa na uwezo wa mwisho wa kumrudishia Uanachama wake kwa mujibu wa Katiba, endapo itaridhika kuwa amejirekebisha.

(9) Kuziongoza Halmashauri Kuu za CCM za Mikoa kuhusu vitendo na njia zinazofaa za kuimarisha CCM na za kuleta maendeleo.

(10) Kuandaa Katiba, Kanuni na kuweka taratibu za kuongoza shughuli mbalimbali za CCM.

(11) Kuandaa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa.


Inaendelea......
Huu "ujamaa" hapa ( kaya ya 2 na 3)
ni upi,maana najua sasa hutuna mfumo wa ujamaa .ila ubepari hiv
 
Back
Top Bottom