Ijue Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na Wajumbe wake

(12) Unapofika wakati wa Uchaguzi, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itashughulikia mambo yafuatayo:-

(a) Kuteua jina la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM, na majina mawili ya Wanachama watakaosimama katika uchaguzi wa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM.

(b) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa majina yasiyozidi matatu ya Wanachama wanaogombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuyawasilisha mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa.

(c) Kuchagua jina moja la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar

(d) Kuwachagua Katibu Mkuu wa CCM, Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi, Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Organaizesheni kutoka miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

(e) Kuwachagua Wanachama wasiozidi kumi (10) kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kutokana na mapendekezo ya Mwenyekiti wa CCM.

(f) Kuwachagua Wajumbe sita (6) wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa watatu (3) kutoka Tanzania Bara na watatu (3) kutoka Zanzibar, wakiwemo wanawake wasiopungua wawili mmoja kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar.

(g) Kufikiria na kufanya uteuzi wa mwisho wa majina ya Wanachama wanaoomba nafasi ya Ubunge na majina ya Wanachama wanaoomba nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa sheria zilizopo za uchaguzi huo.

(h) Kufikiria na kufanya uteuzi wa mwisho wa majina ya Wanachama wanaoomba nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa; Uenyekiti wa CCM wa Wilaya na Mikoa.

(i) Kufanya uteuzi wa mwisho wa majina ya Wanachama wa CCM wanaogombea Uenyekiti wa Mkoa, Uenyekiti na Makamu Wenyeviti wa Taifa wa kila Jumuiya ya CCM.

(j) Kuwachagua Wajumbe wanane wa Baraza la Wadhamini kutoka Tanzania Bara na Zanzibar


Inaendelea...
 
(13) Kujaza kwa niaba ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa, nafasi za uongozi zitakazokuwa wazi, isipokuwa ya Mwenyekiti wa CCM na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM.

(14) Kuunda Kamati au Tume kwa shughuli maalum bila kuathiri majukumu ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.

(15) Kupokea na kujadili taarifa za Tume na Kamati Maalum za CCM, Kamati ya Wabunge wa CCM, na Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.

(16) Kuweka kiwango cha kiingilio katika CCM, ada za Uanachama na michango maalum.

(17) Kusimamisha kwa maslahi ya CCM utumiaji wa kifungu chochote cha Katiba ya CCM au kuruhusu kifungu kutumika kabla ya kuingizwa ndani ya Katiba. Uamuzi huo sharti uungwe mkono na theluthi mbili ya Wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili za Wajumbe kutoka Zanzibar. Hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafikisha uamuzi wake mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa uamuzi wa mwisho.

(18) Kushughulikia uhusiano kati ya CCM na Jumuiya mbalimbali za wananchi na kuziorodhesha Jumuiya za CCM.

(19) Kutengeneza na kurekebisha Muundo wa CCM katika maeneo na nyanja mbalimbali kwa kadri itakavyoonekana inafaa.

(20) Kumsimamisha Mwenyekiti wa CCM au Makamu Mwenyekiti wa CCM iwapo mwenendo na utendaji wake wa kazi vinamwondolea sifa za uongozi. Hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafikisha mapendekezo yake mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa uamuzi wa mwisho.

(21) Kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.

(22) Kuunda Kamati ya Usalama na Maadili.

(23) Kuidhinisha Kanuni za Kamati za Wabunge wote wa CCM, Wawakilishi wote wa CCM, Madiwani wote wa CCM; Katiba/Kanuni za Jumuiya za CCM na kuidhinisha marekebisho ya Katiba/ Kanuni hizo.

(24) Halmashauri Kuu ya Taifa yaweza kukasimu madaraka yake kwa Kamati Kuu kuhusu utekelezaji wa kazi zake kwa kadri itakavyoona inafaa.
 
Kaeni mkao wa kula nitaanza kuelezea hatua kwa hatua
 
Mjumuiko wa majizi ya Mali zetu yote haya Yana ukwasi wakutosha yamevuna vyema Kodi zetu pumbafu sana
 
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu na asiye mnafiki anafuatilia hizi hadithi? Sijui huko nyuma kaandika nini lakini ikitokea hajaandika jinsi CCM ni chuo cha kuzalisha mafisadi na wezi wa mali ya umma andiko lake halina maana kabisa.

Waliiba mali za wananchi na kujimilikisha kama zao. Mali walizoiba ni pamoja na majumba, magari, viwanja, mashirika ya umma, vyama vya ushirika, vyuo na shule pamoja na jumuiya mbali mbali za wananchi. Ngoja niachie hapo.
 
Kwahyo hao wote kwenye ukumbi Ndio imefamya hyo total iwe buku mbili jumla ya wajumbe wote
 
Naona wengi wanaenda nje ya mada
 
Nafasi za kupeana ulaji tu, hakuna lolote wanalofanya wote hao.
 
Duh!! Toa maelezo yaliyoshiba
Kama spika wa bunge ni mjumbe kwenye halmashauri kuu ya CCM ataweza kuikosoa na kuisimamia serekali vizuri unavyoona. Atakuwa tayari kuliona bunge likimuwajibisha raisi ambaye ni mwenyekiti wake wa chama. Katiba yetu inamapungufu mengi mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…