Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Mkuu upo sahihi kwa upande mmoja na upande mwingine haupo sahihi kuhusu ngozi nyeusi maeneo hayo hizi enzi za kati.Kumbuka Waarabu sio wa kwanza kuingia hapo, na Wamisri hao wa kale walikuwa na vituo vya elimu hasa eneo la Alexadria ambalo watu wa mataifa mbalimbali walikuwa wanakuja kusoma hapo, hivyo Waarabu ni race ya mwisho kuingia hapo Misri baada ya Wayunani-Greeks na kisha Warumi chini ya Alexander the great
Hiyo picha hapo chini inaonyesha watu wa race mbili tofauti, hao wanaotahiri ni watu Weusi ambao ndio wenye huo ujuzi na utamaduni, wakiwapa tohara hao wageni watu weupe? Wagiriki, Warumi, Waarabu?
View attachment 463577
Hayo uliyoongea hapo wewe ni historia ya maelfu ya miaka kabla ya uzao wa Yesu.
Lakini enzi aliyozaliwa Yesu toka kabila la Yuda, tayari hayo unayoongelea yalishapita enzi na enzi.
Hayo makabila 12 ya Wayahudi yanayoongelewa ktk "bible" yapo mpaka leo, moja wapo likiwemo la Yesu.
Pia usome historia inasema, Baba wa uzao wa Israel ni Abrahamu ama Ibrahimu. Huyo mzee Ibrahimu na mkewe Sara, alitokea Babeli(Iraki ya sasa) na kundi lake la ngamia kupitia mji wa Damascus (Syria ya leo) kuelekea upande wa kusini ili kuifuata nchi ya ahadi aliyooteshwa na Mungu.
Alipofika hiyo nchi ya ahadi, hakukuta aridhi tupu isiyokaliwa na watu. Bali alikuta wenyeji ambao ni Wafilisti (Wapalestina wa leo) na wakamuwekea pingamizi. Kwakuwa alikuwa na utajiri wa kutupwa, alinunua kipande cha aridhi, haijulikani ukubwa wa aridhi hiyo ili kuanzisha makazi.
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa waisrael kuishi Maeneo ya asili ya wa-Palestina
Tukirudi kwenye mada, tuangalie sasa "nature" ya Waisrael na Wapalestina wa leo kutokana na simulizi za historia niliyoiweka hapo juu kama walikuwa ni ngozi nyeusi kweli!