Ijue KADCO, kampuni hewa iliyokuwa ikiendesha uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airport

Ijue KADCO, kampuni hewa iliyokuwa ikiendesha uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airport

Niliiangalia ule mjadala bungeni Hadi Mwanasheria Mkuu akawa na evassive answers.

Nikajua hapa tayari Pana shida
Mimi nilizima TV sikuamini kama eti Tanzania hakuna wanasheria mpaka tukaangukia kwa kile kiazi kwa kweli
 
Yaani shetani yuleyule wa miaka yote anaendelea kuwakamata viongozi wetu na kuwatumia kuharibu na kuumiza wananchi na nchi...

Angalieni, huyu mama (Rais Samia Suluhu Hassan) naye keshamvaa shetani huyo huyo na keshaingizwa mkenge na yeye mwenyewe kwa mkono wake kusaini mkataba hatari na angamizi na kampuni ya waarabu iitwayo DP World...

USHAURI:

Wandugu, haya mambo hayako kama tunavyoyaona Kwa macho ya damu na mwili huu tulionao. It's beyond that..

Hii kitu haiwezi kukoma unless nguvu kuu inayozidi ile iliyowashika viongozi na watawala wetu itachukua nafasi yake..

Ni Rahisi tu. Zingatieni haya👇👇

1. Kila mwana wa nchi hii mwenye mapenzi na nchi yake, na anayeamini kuwa yupo Mungu aliye hai aliyetupa nchi hii kuwa urithi wetu na vizazi vyetu, basi aombe kwa lugha yake ili kuruhusu mkono wa Mungu wetu aliye hai uwe juu ya nguvu hii ya uharibifu inayowatawala na kuwaongoza viongozi wetu kufanya maamuzi hatari na angamizi kwa nchi yetu..

2. Kila mwana wa nchi hii anayeamini katika nguvu na mamlaka iliyo kuu zaidi (yaani Mungu - Yehova katika Yesu Kristo) akiombee KITI CHA U - RAIS wa nchi yetu. Katika kiti cha u - Rais wa nchi yetu ndipo ambapo chanzo (source) ya maamuzi yote ya nchi na taifa hili la Tanzania yawe mabaya au mazuri yanapotoka...

Na kwa jinsi ilivyo sasa, ni wazi kuwa nguvu ya MKUU WA MAPEPO na WACHAWI ndiye inayekimiliki na kukitawala kiti hicho. Yeyote anayekikalia hata awe msafi namna gani, hata awe na makusudi na malengo mazuri kiasi gani juu ya nchi yetu wakati anaingia, lakini mara akikaliapo kiti hicho kama nguvu hana iliyo kuu kuliko inayokitawala kiti hicho, Rais huyo lazima ata - compromise na matakwa na miongozo ya ubaya ya yule mwenye nguvu mchawi mkuu - shetani anayekimiliki kiti hicho...

Wakati mwingine nguvu hii ya kishetani na kichawi, huchagua yenyewe mtu wa kuja kukikalia kiti hicho kuanzia ktk hatua za michakato ya uchaguzi...

Nguvu hii ndiyo inayodhibiti mifumo ya kisiasa na kiutawala ya nchi yetu ili ibaki kama ilivyo na ubovu wake pasipo kuruhusu mwanya wa mtu anayemjua Mungu na anayejua siri ya utendaji kazi wa nguvu za kipepo na kichawi zinavyofanya kazi ktk tawala za nchi kuchukua uongozi wa nchi..

Mashetani, wachawi na MAPEPO yanajua mtu wa namna hii akichukua nafasi ya kukikalia kiti cha maamuzi katika nchi a.k.a Kiti Cha U - Rais, basi ndo itakuwa mwisho wa nguvu na utawala wao na ndiyo itakuwa ndo mwisho wa mifumo yao ya uovu kuendelea kutawala nchi...

KWA HIYO;

✍️Tatizo siyo watu. Tatizo sio Mkapa wala Kikwete wala Magufuli na wala tatizo sio Rais Samia Suluhu Hassan kwa sasa. Tatizo ni nguvu iliyo nyuma yao kusukuma maamuzi yao ambayo huleta athari hasi katika nchi..

✍️Kwa kuwa akili na ufahamu wao halisi unakuwa umedhibitiwa na nguvu za kipepo na kichawi, obvious wao huwa hawaoni ubaya wa maamuzi yao. Wao huona wamefanya kwa wanachokiita "uzalendo wa nchi yao", lakini ukweli ukiwa kinyume chake. Huja kugundua kuwa wamefanya maamuzi ya hovyo baadaye wakiwa hawapo kwenye position zao..

✍️Kwa hiyo, tukitaka kumshinda adui huyu asiyeonekana kwa macho ya mwili na tukitaka kuikoa nchi yetu, basi hatupaswi kufanya vita kwa jinsi mwili na damu. Badala yake vita viwe vya kiroho kama ilivyoandikwa;


2 Kor 10:3‭-‬6 SUV

"......Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome😉 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia..."

✍️Pia silaha zetu za kutumia katika vita hii si hizi tunazohimizwa na kina Mwabukusi na kina Dr Wilbroad Slaa (physical congratulation) kama vile kuandamana, migomo nk . Bali silaha zetu za kumwangamiza kabisa na kumtiisha adui huyu zimeanishwa very clearly na Mungu mwenyewe katika Neno lake..

Wefeso 6:11‭-‬14‭, ‬16‭-‬18 SUV
".......Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;...."


Walio upande wangu na kuijua elimu hii wamenielewa vizuri sana..

Namtakia kila mtu kila la kheri ktk kuchukua hatua..
Shetani mkubwa ni CCM yaani chama cha mashetani huyu hatoki kwa kumkemea toka huyu unamng'oa kama nduli Idd Amin Dadaa.
 
Hizo share za South Africa Ni akina Mkapa, barozi mpungwe etc.wote hawako kwenye system ndo maana wanarundisha serikalini. Kuna watyu wametafuna pesa kwenye nchi hii, cha ajabu nao uzeeka na kufa. Akina mpungwe Sasa hivi hawezi maliza hata laki moja kwa kula, mzee sana, hata kutembea Ni shida sana.

Binadamu hatujui tuanchotafuta hapa duniani, uwe na majumba, mahotel ,pesa kwenye account zote Ni upepo tu. Watu wangapi wamekufa kwa kukosa hizo pesa kwenye matibabu, shule, maji safi, madawa etc. JPM angeweza kuvunja lakini kwa vile alikuwa kijana wa Mkapa akapotezea.
Wewe ndio umenifungua macho

Nilikua najiuliza, inakuaje Magufuli akaacha KADCO ikaendelea kuwepo kumbe ni kampuni ya mzee wake.

Watu wa kadco walitakiw akichinjwa hadharani mchana kweupe jua limewaka uwanja wa taifa pale.
 
Hata kandarasi za mamia ya bilioni yaliyopewa makampuni bila ushindani yawezekana yalihusisha ufisadi mkubwa.
 
Usalama wa Taifa hawakunusa hii kitu muda wote huo?
Huu ndo ulikuwa uchochoro wa kupakia wanyama pori rejea wale waliosafirisha twiga enzi ya JK wafanyakazi karibia wote waliokamatwa walikuwa niwa KADICO.
Hivyo hata Kama walinusa kulikuwa na wakubwa wanahusika hapo
 
Kuna quatation yako toka kwenye Biblia kitabu cha Mhubiri 1:17...."Yote ni kujilisha upepo" imenifurahisha lakini, je unaelewa maana yake ktk context ya maisha haya tunayoishi leo hapa duniani?

Pls, don't get offended kwa kukuliza swali hilo. It's just ktk kujaribu kukuleta karibu nami tujadiliane haya mambo. Nishee nawe kile ninachokijua mimi na mimi pia nipate kutoka kwako kile ujuacho.

Hopefully, twaweza kukutana mahali na tukaelewana..
Mimi ni mjinga wa kiroho mkuu.
Ok. Natambua kuwa umekwoti toka ktk jibu langu kwako kule ☝️juu ile jana. Yaonekana ulikwazika kwa sentesi hiyo. Pole sana. Halikuwa kusudi langu kukukwaza..

Lakini ndivyo nilivyooona baada ya kusoma maandishi yako na kuona wazi kuwa ni kama hauko aware kabisa kuwa maisha yetu hapa duniani yako controlled na mojawapo ya mifumo miwili; wa aidha wa mabaya (tusiyoyapenda, tusiyoyataka) au mazuri (tuyatakayo, tuyapendayo). Kila mtu ukiwemo wewe na mimi tuko ktk moja ya hiyo mifumo. Hakuna aliye katikati..!!

Na ni uchaguzi (choice) ya mtu mwenyewe kuamua kuishi ktk moja ya mifumo hiyo. Unaweza kuwa uchaguzi wa hiari au wa kulazimishwa na hali au mazingira...

Mantiki ya kuibua mjadala huu ni hoja hiyo ☝️.

Kwamba, Tanzania kama nchi/taifa tunalazimishwa kuishi katikati ya mfumo wa ubaya kwa sababu tu kuna watu wachache tuliowaamini na kuwapa dhamana ya uongozi ili kutuongoza lakini wakaitumia vibaya dhamana na mamlaka yao ya kiutawala na kimaamuzi kwa kufanya maamuzi ya kujiungamanisha na mifumo hatari na angamizi duniani na kuliingiza taifa lote ktk taabu na shida..

Swali kubwa ambalo tunajiuliza wote ni: Haya mambo chanzo chake ni nini? Tufanye nini tutoke hapa tulipo?

Hakuna mtu achaguaye kuishi katikati ya ubaya kama ufisadi, ulevi, uasherati, ujambazi, wizi na yafananayo na hayo. Isipokuwa hulazimishwa au hujikuta anaishi maisha ya hivyo pasipo kujua anawezaje kujitoa huko unless amepata ufahamu wa namna ya kutoka..
Nitasema nini sasa kwa mlokole aliyeiva katika ulimwengu wa kiroho na Neno + utakatifu kama wewe?
"Mlokole" ndio kitu gani, ndiyo nini? Mimi si kitu nisichokijua. Mimi ni Mkristo ninayeelewa na kujitambua...
Hata mjadala utafanyikaje wakati hakuna mahali pa kukutania panapotuunganisha (common ground)?
Una maana gani kusema "hakuna common ground" ya kukutana ktk mjadala? Je, mada iliyo mezani sio common ground?
Ulimwengu wa kiroho...ulimwengu wa kiroho! Ukiuliza huko ulimwengu wa kiroho ni wapi? Panafikikaje kwa mtu wa kawaida kama mimi? Pakoje?
Ili ujue kuwa ulimwengu wa roho upo na ni halisi jiulize tu maswali kadhaa kama vile: Maovu kama ufisadi, wizi, uzinzi, uasherati, masengenyo nk chanzo chake nini? Yanatoka wapi? Kwanini yanaumiza watu?
Majibu yake sasa kama siyo kutukanwa na kubezwa na wakazi wa huko utashangaa.
Unajishitukia tu. Acha hizi, jiamini. Na ilitokea umetukanwa, potezea na focus kwenye unachokihitaji..
Hata sijui ni kwa nini huwa mnapenda kupaleta huku kwenye ulimwengu wa kawaida kama huko kwenu ulimwengu wa roho ni mahali pa siri na wanaofika huko ni watakatifu wachache na wateule (walokole!) 😬😬😬
Ni Kwa sababu hujui tu. Unadhani hizi ulimwengu mbili hazikuhusu wewe na zinawahusu wengine tu...

Nikuambie kitu kimoja tu ndugu Shimba ya Buyenze, kwamba, katika kila unachokiona ktk ulimwengu huu wa damu na mwili kiwe kizuri au kibaya; unakipenda au hukipendi, basi tambua kuwa yupo asiyeonekana kwa macho haya (unless otherwise) aliyesababisha hicho kitu kutokea..!

Kikiwa ni kizuri na ni kile unachokitaka ktk maisha yako basi iamini, itambue na i - embrace hiyo nguvu iendelee kukuongoza kukupa utakacho...

Kikiwa ni kibaya, usichokitaka au kukipenda ktk maisha yako, basi hakikisha unapigana na nguvu hiyo ili isiendelee kukuharibu.
Kwa heshima tu tuufunge huu mjadala mtumishi mwema wa Bwana.
Hapana, haufungiki. Ila mtu anaweza kuamua mwenyewe kukaa kimya tu..
Mara moja moja ukipata muda usisite kutuombea sisi wajinga wa kiroho ili nasi siku moja tuwe watakatifu kama wewe & Co.
Unapaswa kwenda mwenyewe mbele za Mungu na kumuomba utakacho. Mlango uko wazi kwa kila mtu ukiwemo wewe..

Ninachoweza kukusaidia mimi ni kukuonesha njia ya kwenda huko kama huifahamu. Na njia yenyewe ni hii👇👇👇👇
Yohana 14:6
"...Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na Kweli na uzima. Mtu haki Kwa Baba, ila Kwa njia ya mimi...."
Bila shaka tutakutana mbinguni mtumishi. Tuombeane 🙏🏿😁😁🖐🖐🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
Literally, there's no place called "mbinguni" mzee Shimba ya Buyenze na kwamba tutakuja kukutana huko siku moja mimi na wewe...

Mbingu yako ni wewe mwenyewe, iko ndani yako na ukimruhusu Mungu - Yehova Kwa njia ya roho wake mtakatifu kuishi ndani yako unakuwa umeifanya mbingu yako kuwa salama na takatifu..

Karibu Tena..
 
Wewe ndio umenifungua macho

Nilikua najiuliza, inakuaje Magufuli akaacha KADCO ikaendelea kuwepo kumbe ni kampuni ya mzee wake.

Watu wa kadco walitakiw akichinjwa hadharani mchana kweupe jua limewaka uwanja wa taifa pale.
Kadco Ni Hawa jamaa hapa chini shares za uko South Ni zao
 

Attachments

  • Screenshot_20231111-002601.png
    Screenshot_20231111-002601.png
    159.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_20231111-002843.png
    Screenshot_20231111-002843.png
    100.2 KB · Views: 4
  • Screenshot_20231111-003227.png
    Screenshot_20231111-003227.png
    80.2 KB · Views: 3
  • Screenshot_20231111-002317.png
    Screenshot_20231111-002317.png
    123.2 KB · Views: 5
  • Screenshot_20231111-003646.png
    Screenshot_20231111-003646.png
    155.6 KB · Views: 3
Enhee,,kelele za November zimefikia wapi?
Watu wako palepale--hakuna cha TAA wala nini.
 
𝗥𝗘𝗩𝗘𝗔𝗟𝗘𝗗: 𝗛𝗼𝘄 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝘀𝗶𝗴𝗻𝗲𝗱 𝗮 𝗰𝗿𝗮𝘇𝘆 𝗱𝗲𝗮𝗹 𝘄𝗶𝘁𝗵 𝗮 𝗺𝘆𝘀𝘁𝗲𝗿𝘆 𝗰𝗼𝗺𝗽𝗮𝗻𝘆 𝘁𝗼 𝗼𝗽𝗲𝗿𝗮𝘁𝗲 𝘁𝗵𝗲 𝗰𝗼𝘂𝗻𝘁𝗿𝘆'𝘀 𝗺𝗮𝗶𝗻 𝘁𝗼𝘂𝗿𝗶𝘀𝘁 𝗮𝗶𝗿𝗽𝗼𝗿𝘁

The government announced today that Kilimanjaro International Airport (KIA) will finally be handed over to the state-run Tanzania Airports Authority (TAA) tomorrow, but the real beneficiaries of KADCO, the company that operated the airport for 25 years and collected billions in revenues, remain shrouded in mystery

* KIA is the third-busiest airport in Tanzania and is the gateway to the country's main safari tourism hotspots in the northern circuit

CHRONOLOGY OF EVENTS:

✅ 11 March 1998, Kilimanjaro Airports Development Company Limited (KADCO) is registered at BRELA, with mystery shareholders Mott MacDonald International Ltd (99%) and Inter Consult Ltd (1%)

✅ Just 3 months after KADCO was registered (17 July 1998), it enters into a new shareholding agreement, where the Tanzania government got 24% of the shares of the company, Mott MacDonald International Ltd (41.4%), South Africa Infrastructure Fund (30%) and Inter Consult (T) Ltd (4.6%)

✅ On 10 November 1998, just 8 months after KADCO was established, the company signs a 25-year concession agreement with the Tanzania government, giving it exclusive rights to develop and operate KIA, despite having no track record nor previous experience in running an airport

✅ In 2006, the government reviewed the performance of KIA and discovered the following anomalies:

* Shareholders failed to invest in infrastructure upgrade at KIA, leading to poor performance of the airport

* KADCO was NOT PAYING any concession fee to the government for operating the airport despite collecting revenue. There was no concession fee clause in the agreement

* There is also no clause for TERMINATION of the concession in the agreement. The agreement only has a clause for renewal of the lease after every 15 years when the 25-year concession expires

* The concession agreement PROHIBITS the construction of any international airport within a 240km radius of any side of KIA, hence effectively giving KADCO exclusive rights to operate the only international airport in the region

✅ When government sought a review of the unconscionable terms of the concession agreement, the shareholders REJECTED any amendments. In 2009, the government decided to buy out the shareholders of the company and acquired 100% ownership of KADCO. It remains unclear how much the government PAID the shareholders to reliquish ownership

✅ KADCO continued to operate KIA, despite the government taking 100% ownership of the company amid audit queries from the CAG and Parliament on the WHEREABOUTS of revenue collected by KADCO as operator of the airport

✅ 9 November 2023, the Minister of Transport, Prof. Makame Mbarawa, announced in Parliament that KIA will now officially be handed over to TAA on 10 November 2023
So after 14 years, the 'Government (100% shareholder) handed-over the KIA operations to the 'government' (TAA). This is ubsurb!
 
Back
Top Bottom