Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Kama kawa, kila nipatapo fursa hushuka na kwa maslahi ya taifa ambazo huwa na swali, jibu utatoa mwenyewe.
Swali la leo ni kuhusu kuijua katiba yetu. Je wajua kuwa kila kura Iliyomchagua Rais Magufuli kwenye ule uchaguzi mkuu wa 2020, pia Ilimchagua Samia?. It's not right kusema Rais Samia hakuchaguliwa!. Kama vipi basi 2025 Tumchague?.
Katiba ni kakitabu kadogo sana ukilinganisha na Quran Tukufu na Biblia Takatifu, na kila mtu anayejua kusoma na kuandika, anaweza kuisoma katiba, lakini kuielewa katiba, ni shughuli nzito!.
Katiba ndio Msahafu wetu wa kuendesha nchi yetu, kila kinachofanyika nchini, lazima kifanywe kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni, lakini kwa bahati mbaya sana, wengi wa viongozi wetu, hawaijui katiba yetu, wakiwemo wanaopaswa kuijua, ndio maana kila uchao viongozi wetu wanaikiuka hii katiba.
Watu wa kwanza waliopaswa kuijua katiba ni wanasheria, lakini very unfortunately wengi wa wanasheria wetu ni mbumbumbu wa Katiba.
Mimi japo fani yangu rasmi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea.
Sheria yangu nimeisom ea UDSM na moja ya masomo niliofanya vizuri na kupata alama ya A, ni somo la katiba ambalo enzi zetu likifundishwa na Prof. Issa Gullamhuseein Shivji, mitihani yake nilikuwa naofumua utadhani nimetunga mimi.
Ni baada ya kuhitimu sheria, nikajikuta napenda sana kuisoma katiba, ndipo nikawa nashangaa jinsi viongozi wetu wasivyoijua katiba na kila uchao wanakiuka katiba.
Ikawa kila nikipata fursa kukutana nao, huwauliza maswali ya katiba mfano ni swali hili [URL unfurl="true" media
Kufuatia viongozi wetu wengi hawaijui katiba, kama viongozi wanaopaswa kuijua katiba hawaijui, unategemea nini kwa wananchi wa kawaida?, hivyo nimejitolea kufundisha katiba, sheria na haki [URL unfurl="true" media=
Inapotokea miongoni mwa wasio ijua katiba ni wanasheria na ni viongozi wa vyama vya siasa, hili ni jambo la hatari sana kwasababu wanaweza kuwaingiza chaka wanachama wao, wafuasi wao na wananchi kwa ujumla.
Mfano mzuri ni huu [URL unfurl="true" media=
Naomba kumsaidia mdogo wangu TL kumuelimisha kuhusu katiba.
Si kweli kuwa Rais Samia ni Rais ambae hakuchaguliwa na Watanzania, kwa vile Rais Samia alikuwa mgombea mwenza wa Rais Magufuli, kila kura aliyopigiwa Rais Magufuli, pia alimpigia Rais Samia. Sio sahihi kusema Rais Samia hakuchaguliwa!.
Ukiachia kumpigia kura kwenye kura za Magufuli, aliyempa urais Samia ni kwa mujibu wa Katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977, na mwenye katiba ni mwananchi, hivyo Rais Samia amechaguliwa na katiba kuwa rais wetu.
Ikitokea likatokea jambo litakalomfanya VP wa sasa Dr. Mpango kuwa rais wa Tanzania, hapo ndipo TL, atakuwa right kuwa rais huyo, atakuwa hakuchaguliwa na Watanzania, lakini Rais Samia, alichaguliwa na Watanzania tulipomchagua Magufuli, na hata uchaguzi wa 2025, ameisha chaguliwa tena kwa mitano tena, uchaguzi wa rais kwa 2025 ni kukamilisha tuu taratibu wa lile takwa la katiba la uchaguzi ni kila baada ya miaka mitano, hata kama rais tayari tunaye, tutafanya tuu igizo la uchaguzi.
Karibuni sana kuijua katiba.
Paskali