Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la Leo.
Kwa vile huu ni mwaka wa Uchaguzi, na mimi mwandishi wako wa makala hizi, zaidi ya kuwa ni mwandishi na mtangazaji wa kujitegemea, pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, na kwa muda mrefu, nimeandika sana kuhusu katiba ya nchi, hivyo nimeonelea, hakuna ubaya, kuwaelimisha watu kuhusu katiba za vyama, na tukianzia kuijua Katiba ya Chama cha Mapinduzi, CCM.
Uchaguzi wa kuanza na katiba ya CCM, ni kufuatia Jumatano ya wiki hii ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa CCM.
Tuanze na historia ya Chama cha Mapinduzi, kilianzishwa lini na kilianzaje anzaje.
Chama cha Mapinduzi CCM, kilianzishwa kwa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa wa pamoja, cha TANU na ASP, kuwa jukumu lao ni kuimarisha Umoja, kuleta Mapinduzi ya Kijamaa Tanzania na kuendeleza mapambano ya Ukombozi katika Afrika na kote Duniani, kwa kuzingatia na kuthamini kazi nzuri ya kimapinduzi iliyokwishafanywa na TANU na ASP katika kumwondoa Mwafrika kutoka kwenye unyonge wa kunyonywa, kunyanyaswa na kudharauliwa na kumfikisha kwenye uhuru na kuheshimiwa.
Tamko lenyewe la kuiunda CCM ni hili
“Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa pamoja wa TANU na ASP tuliokutana leo tarehe 21 Januari, 1977 mjini Dar es Salaam, chini ya uongozi wa pamoja wa Mwalimu Julius K. Nyerere Rais wa TANU na Ndugu Aboud Jumbe, Rais wa ASP, kwa kauli moja tunaamua na kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shirazi Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari 1977 na wakati huo kuundwa kwa Chama kipya cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika mambo yote kwa mujibu wa Katiba”
Hivyo CHAMA CHA MAPINDUZI, kwa kifupi CCM kikazaliwa Tarehe 5/2/1977 na makao makuu ya CCM ni Dodoma na Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na kuna Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Lumumba jijini Dar es Salaam.
Imani za Chama Cha Mapinduzi ni Binadamu wote ni sawa. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake na Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
CCM ina malengo 19 lengo kuu likiwa ni Kushinda katika Uchaguzi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande mmoja na Zanzibar kwa upande wa pili. Kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi
Malengo mengine ni kulinda na kudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake.
Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.
Kusimamia utekelezaji wa Siasa ya CCM pamoja na kuendeleza fikra za viongozi waasisi wa vyama vya TANU na ASP, kama zilivyofafanuliwa katika maandiko mbalimbali ya Vyama hivyo.
Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria.
Mengine ni kuona kwamba katika Nchi yetu kila mtu aliye na uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi; na kazi maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu riziki yake.
Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.
Mengine ni Kuona kwamba kwa kutumia Vikao vilivyowekwa, raia anayo haki ya kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi wa mambo ya Taifa na yanayomhusu, na kwamba anao uhuru wa kutoa mawazo yake, wa kwenda anakotaka, wa kuamini Dini anayotaka na kukutana na watu wengine, maadamu havunji Sheria au Taratibu zilizowekwa.
Mengine ni Kuona kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia na ya kijamaa.
Kuhifadhi, kukuza na kudumisha imani na moyo wa kimapinduzi miongoni mwa Watanzania pamoja na ushirikiano na wanamapinduzi wenzetu kokote waliko.
Kuweka na kudumisha heshima ya binadamu kwa kufuata barabara Kanuni za Tangazo la Dunia la Haki za Binadamu.
Mengine ni
Kuona kwamba Dola inakuwa Mhimili wa Uchumi wa Taifa.
Kuona kwamba Serikali na Vyombo vyote vya Umma vinasaidia kwa vitendo kuanzishwa na kuendeleza shughuli za Ushirika na za ujamaa, na shughuli nyinginezo halali za Wananchi za kujitegemea.
Kuona kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya Wananchi na hasa jitihada za kuondosha umasikini, Ujinga na Maradhi.
Wiki ijayo nitaendelea kuhusu uanachama wa CCM, nguvu za mwanachama na nguvu za Mkutano Mkuu wa CCM.
Wasalaam.
Paskali