Ijue minara kumi ya kuvutia mirefu zaidi duniani

Ijue minara kumi ya kuvutia mirefu zaidi duniani

Ila usijali mkuu nipo likizo now nitakuwa napisti hapa intelligence kuhusu "10 kubwa" hivyo uwe unachungulia mara moja moja ila nitakuwa nadondosha kidogokidogo
Kumbe lengo lako ni kutohold??
 
sikuwa na nia mbaya mkuu.

ila watu wengi wanaishi kusoma thread basi. wachache sana wanasoma kila post.
nadhani umenielewa vibaya ngoja nikuache ila mimi nasoma post zote hata kama ukipost uharo nasoma
Kuwa na amani jomba
Hapa ni Jukwaa la Intelejensia hivyo kupost kitu hapa hadi mtu ajipange

Kuhusu hao wanaosoma post 1 tu hiyo haina tatizo jukumu langu ni kuandika kihusu kuifymuatilia thread inabaki kuwa uamuzi binafsi wa mtu maana hakuna ninacholipwa kwa mtu kusoma post zote au kutosoma
 
5/The Oriental Pearl Tower
97f22d98b73ff670b400cbc46bce2e3a.jpg
09dc42ca7977e5827666d0e8ef392630.jpg

Mnara huu unapatikana karibu na mto Hangpu huko Pudong New Area Shanghai nchini China<br
Ndo mnara unaotegemewa kwa matangazo ya radio na luninga jojini Shanghai
Ulianza kujengwa mwaka 1991 na kukamilika mwaka 1994
Ni mnara mahususi kurushia matangazo ya vyombo vya habari ila pia una migahawa na hoteli, bila kusahau unatumika kulitazamia jiji la Shanghai

Una urefu wa futi 1,535
 
4/Ostankino Tower
f7b8f04b25860aff03bdfde92852593b.jpg
eb823cad267903b595e1694b8de5cae7.jpg

Huu ndo mnara mrefu zaidi barani Ulaya
Upo kule kwa "Kumsamehe gaidi ni kazi ya Mungu ila kumpeleka gaidi kwa Mungu ni kazi ya Putin" .......Sasa ole wao ISIS wakaulipue kitakachowapata watajua wenyewe tunaweza tukaokota hadi bongo vichwa vilivyojaa ndevu kama kambale

Upo jijini Moscnow nchini Urusi
Ulianza kujengwa mwaka 1963 na kukamilika ujenzi wake mwaka 1967
Unatumika kwa ajili ya kurushia matangazo ya luninga na radio,kutizama jiji la Moscow na utalii
Pia ndo jengo refu zaidi barani Ulayaa na kwa dunia unakamata # 11 kwa urefu wa jengo ukipambanishwa na majengo yote

Mnara huu una urefu wa futi 1,772
 
3/CN Tower
6a5f42318fbc9e78267b188422b0bc17.jpg
1ab896c30d49819a986465dac038fc83.jpg

Umesimama huko Toronto nchini Canada
Ulishikilia rekodi ya mnara/jengo refu zaidi duniani kwa miaka takribani 32 hadi pale ilipofika mwaka 2007 rekodi yake ikafa kifo cha mende

Uojenzi wake ulianza mwaka 1973 na kukamiltika mwaka 1976...mnara huu umejengwa kwenye njia ya zamani ya. Treni huko Toronto
Pia upo karibu na machimbo. Ya dhahabu ya Ontario hapohapo Toronto
Ni maalimu kwa ajili ya kurushia matangazo ya luninga na radio ila pia unatumika kibiashara maana kuna migahawa kibao imejengwa na wartalii hufika kwa wingi

Una urefu wa futi 1,815
 
5/The Oriental Pearl Tower
97f22d98b73ff670b400cbc46bce2e3a.jpg
09dc42ca7977e5827666d0e8ef392630.jpg

Mnara huu unapatikana karibu na mto Hangpu huko Pudong New Area Shanghai nchini China<br
Ndo mnara unaotegemewa kwa matangazo ya radio na luninga jojini Shanghai
Ulianza kujengwa mwaka 1991 na kukamilika mwaka 1994
Ni mnara mahususi kurushia matangazo ya vyombo vya habari ila pia una migahawa na hoteli, bila kusahau unatumika kulitazamia jiji la Shanghai

Una urefu wa futi 1,535
Huu mnara nimeshawahi kuupanda, urefu wake ni 350m, mleta maana jaribu kuweka sahihi vipimo vya minara hii
 
2/Canton Tower
de8230ee70f96b54f7b2b48a400f6a93.jpg
98ee62437c9f288f2704661dd72d0d43.jpg

Upo huko Guangzhou nchini China karibu na Pearl River
Zamani ulijulikana kama Guangzhou Tv Astronomical &Sightseeing Tower

Ulianza kujengwa nwaka 2005 na kukamilika mnamo mwaka 2010
Matumizi yake makuu ni kurushia matangazo ila pia utalii na biashara

Una urefu wa futi 2,000
 
Huu mnara nimeshawahi kuupanda, urefu wake ni 350m, mleta maana jaribu kuweka sahihi vipimo vya minara hii
Mita 1 = Futi 3.3
350m X 3.3 =1155 ft

Nilichogundua umehesabu urefu wa mnara yaani lile zege pekee ila kumbuka juu kuna antena ya kunasia matangazo nayo ukijumlisga ndio unapaka urefu kamili wa huu mnara
 
1/Tokyo Skytree
e7851c26c8106445d4d162b376daa204.jpg
8af75b1f002592653d5fe77a6b226c6b.jpg

Unapatikana huko kwa akina Takuma Asano,Shinji Kagawa,Junichi Inamoto na Hidetoshi Nakata au ukipenda tu waite wazee wa Toyota
Ndio mnara mrefu zaidi duniani ,umejengwa jijini Tokyo nchini Japan
5ef8edfadcd520e624919d8f20c8bf59.jpg

Kuufananisha mnara huu na ule wa Paris ni kama kumsimamisha kistuli na Hasheem Thabeet tu<
Ulianza kujengwa mwaka 2008 na kukamilika mnamo mwak 2012
Unatumika kurushia matangazo,utalii na biashara kwahiyo kama unataka kuuona mnara mrefu zaidi duniani kwa macho yako nenda huko achana na ule wa Paris

Una urefu wa futi 2,080

.
.
.
Mwisho
The Bitoz
...............
 
Huu mnara nimeshawahi kuupanda, urefu wake ni 350m, mleta maana jaribu kuweka sahihi vipimo vya minara hii
Nadhani yupo sahihi na wewe upo sahihi ila record inaonyesha hivyo hapo chini;

Antenna spire 467.9 m (1,535 ft)
Top floor 350.0 m (1,148 ft)
 
Kwa nchi za Kiafrika suala la kujenga minara kama utambulisho wa jiji na kivutio cha utalii au kurushia matangazo ya redio na televisheni halipewi kipaumbele .
Pia inaonekana kama matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi
Dikteta Mobutu Sese Seko alwahi kuanzisha ujenzi wa mnara huko nchini Zaire(DRC) lakini hadi anaondolewa madarakani haukukamilika na kuishia kutelekezwa tu na kuwa makazi ya bundi
Kwa Wakristo kuna Mnara wa Babeli ila sijajua ni mnara wa kiimani tu au upo kweli duniani

Tuangalie minara 10 mirefu zaidi duniani
......................................................... .......

10/Zhongyuan Tower
0fb881ded16ffde2e7199cef283aa1a2.jpg
ea9ff670dd138ad32cd8954e61ac38d6.jpg

Unapatikana Zhengzhou katika jimbo la Henan nchini China
Unaaminika kuwa ndio mnara mrefu zaidi duniani uliotegenezwa kwa vyuma.....ikumukwe hata ElfeltTtower huko jijini Paris Ufaransa umetengenezwa kwa vyuma na ndo chanzo cha jamaa fkani hivi kuwatapeli wafanyabiashara wakubwa kwa kuwadanganya kuwauzia ili wapate vyuma
Sasa tuendelee.....mnara huu ujenzi wake ulikamilika mwaka 2011 na ndo ukawa mnara mrefu zaidi wa chuma hadi pale mwingine ulipojengwa Tokyo Japan
Mnara huu una migahawa takribani 200 ya kuhudumia wageni/watalii
Hutumika pia kurushia matangazo ya luninga

Una urefu wa futi 1,273

Boss ule uzi wa yule jamaa tapeli aliyetapeli kupitia mnara wa ufaransa meutafuta kwa kitambo bila mafanikio ukiwa unaweza upata nisaidie link
 
Boss ule uzi wa yule jamaa tapeli aliyetapeli kupitia mnara wa ufaransa meutafuta kwa kitambo bila mafanikio ukiwa unaweza upata nisaidie link
Mkuu hapa intelligence sijawahi kuliona andiko linalomwelezea yeye kama yeye zaidi ni orodha tu ya matapeli(hata mimi ninayo ipo siku nitaweka)
 
Boss ule uzi wa yule jamaa tapeli aliyetapeli kupitia mnara wa ufaransa meutafuta kwa kitambo bila mafanikio ukiwa unaweza upata nisaidie link
Mkuu hapa intelligence sijawahi kuliona andiko linalomwelezea yeye kama yeye zaidi ni orodha tu ya matapeli(hata mimi ninayo ipo siku nitaweka)
 
Nadhani yupo sahihi na wewe upo sahihi ila record inaonyesha hivyo hapo chini;

Antenna spire 467.9 m (1,535 ft)
Top floor 350.0 m (1,148 ft)
Upo sahihi mkuu
Urefu ninaousema ni kuanzia chini hadi kwenye antena maana ni mnara wa kurushia matangazo
 
Back
Top Bottom