Ijue Mwanza jiji

Umeeleza vizuri sana, ila unachanganya kati ya wilaya na Halmashauri.

Majiji yanaundwa na Halmashauri wala sio wilaya.

Ndio maana utakuta yanaitwa HALMASHAURI YA JIJI LA ...
 
Umeeleza vizuri sana, ila unachanganya kati ya wilaya na Halmashauri.

Majiji yanaundwa na Halmashauri wala sio wilaya.

Ndio maana utakuta yanaitwa HALMASHAURI YA JIJI LA ...

Majiji yanaundwa na wilaya zenye hadhi ya Manispaa,

1.Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni(Kinondoni Municipal Council) hii ni wilaya lakni hadhi yake ni manispaa.
2.Halmashauri ya Mji Sengerema (Sengerema Town Council) hii ni wilaya lakni hadhi yake ni mji.

3.Halmashauri ya Jiji Dodoma (Dodoma City Council) hii ni wilaya yenye hadhi ya jiji.

Kwahiyo kuna majiji yanaundwa na wilaya zaidi ya mbili, mfano ni jiji LA Dar es salaam na Mwanza halafu kuna jiji linaundwa na wilaya moja tu yenye hadhi ya jiji kama jiji LA Dodoma, jiji LA Tanga, jiji LA mbeya na Arusha.
 
Inakuwaje umekutana na mtu katikati ya jiji mfano sokoni hamjuani lakini anakuongelesha kisukuma? Huu ni ushamba uliopitiliza.
Kama tu Ukiwa katika roundabout ya Impala au pale Mianzini au sanawari mataa unasalimiwa "TAKWENYA'
 
Majiji yanapata wp maeneo ya mashamba,!? Sheria za majiji ikoje kuhusu mashamba?

Hakuna sheria inayokataza kulima au kufanya shughuli za Kilimo na ufugaji ndani ya jiji.
Sheria iliyopo inakataza kufanya shughuli za Kilimo na ufugaji mkubwa katikati ya jiji.
Kwahiyo kama upo nje ya jiji kama huko Chanika,kigambani, mabwapande huko ruksa, ndio maana Sumaye alikuwa na ekari 300 za Kilimo na ufugaji huko mabwepande, mji unavyosogea ndio mashamba yanapoteza sifa.
Manji alikuwa na mashamba ya Ng'ombe Kijichi Temeke lakni baada ya mji kukua manispaa ya Temeke wakamlipa fidia na kupima viwanja mwaka 2000, mpaka Leo majiji yetu bado yana mapori pembezoni ndio maana unasikia miradi ya upimaji na uuzaji wa viwanja mpaka sasa.
 
Sio mwaka 2002 ni mwaka 2000 ndo Mwanza ilikuwa Jiji
 
Hapo kwenye wilaya mbili, mzee umetupiga kakamba flani hivi. Kuna wilaya nyingine kama magu, sengerema, ukerewe, misungwi n.k
Kuna vitu vingi sana hapa vinapwaya, but all in all tunashukuru kwa
Kwamba jiji la Mwanza lina kata 20?Yaani tumekukaribisha juzi juzi unaanza kujifanya kujua hili jiji?
 
Kwamba jiji la Mwanza lina kata 20?Yaani tumekukaribisha juzi juzi unaanza kujifanya kujua hili jiji?
Kata? Wapi nmeongelea kata mkuu?
Besides, i was born and raised in mwanza, how come umenikaribisha?
 
Jiji la mwanza haliwezi kufika watu mil 3 never, sensa iliyopita population ilikua laki sita na nusu ilemela na nyamagana sasa itafikaje mil 3 kwa muda mfupi hivi ?,mwanza iko over rated
Laki 6 ilikua Arusha na Mwanza ilikua 1.2 milion,ukiondoa Dar es Salaam mji wa Mwanza ni mji wa pili kwa kua na watu wengi zaidi

Hii ya miaka ya nyuma huko
View attachment 2321185
 
Mwanza nilijua ni jiji lenye hela kuliko Arusha, lakin kumbe limepitwa na Arusha banah,,
1. Dar-75.3B
2. Dom-45.1B
3. Arsh-24.3B
4. Mwnz-17.7B
5. Tanga-17.4B
6. Mby-16B
Yaani ikizubaa Tanga wanapga kiwiko
Hapo Ilemela ipo omitted soma vizuri uzi
 
Kata? Wapi nmeongelea kata mkuu?
Besides, i was born and raised in mwanza, how come umenikaribisha?
Mkuu inaonekana hujui hata ulichoandika.Hujazungumza habari za kata?🀣🀣
 
Hapo kwenye wilaya mbili, mzee umetupiga kakamba flani hivi. Kuna wilaya nyingine kama magu, sengerema, ukerewe, misungwi n.k
Kuna vitu vingi sana hapa vinapwaya, but all in all tunashukuru kwa kupaisha jiji letu
πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘† this is exactly what i wrote
Mkuu inaonekana hujui hata ulichoandika.Hujazungumza habari za kata?🀣🀣
Haya mtaalam mwenye PHD ya mwandiko, kusoma na ku-quote comments kutoka chuo cha Jamii Forum , nisaidie kunionyesha wapi nmeandika masuala ya kata hapo juu?
Au ulikurupuka usingizini vidole vinawasha kutype?
 
🀣🀣🀣🀣🀣Sorry mkuu nilikosea kuquote post yako nilimtarget mleta mada
 
Hapo kwenye wilaya mbili, mzee umetupiga kakamba flani hivi. Kuna wilaya nyingine kama magu, sengerema, ukerewe, misungwi n.k
Kuna vitu vingi sana hapa vinapwaya, but all in all tunashukuru kwa kupaisha jiji letu
Amezungumzia Jiji la Mwanza siyo mkoa was Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…