Washawasha
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 16,717
- 13,176
Hongereni Mwanza
Nalog off Z
Nalog off Z
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeeleza vizuri sana, ila unachanganya kati ya wilaya na Halmashauri.Ameongelea Jiji la Mwanza na sio Mkoa wa Mwanza.
Hivi ni vitu viwili tofauti.
Unapoongelea jiji la Mwanza unamaanisha ni Ilemela na Nyamagana hizi wilaya mbili ndio zinaunda jiji LA Mwanza. Na wanaobeba gharama za uendeshaji ni Nyamagana kama ilivyo kwasasa Dar es salaam Ilala ndio inabeba gharama. Jiji LA Dar es salaam wilaya zake zote zimo ndani ya jiji tofauti na Mwanza, Kwa Mwanza wilaya zenye hadhi ya Manspaa ni mbili tu yaani ilemela na nyamagana tu, zilizobaki zote ni halmashauri za mji wilaya tofauti na Dar wilaya zake zote zina hadhi ya manispaa.
Umeeleza vizuri sana, ila unachanganya kati ya wilaya na Halmashauri.
Majiji yanaundwa na Halmashauri wala sio wilaya.
Ndio maana utakuta yanaitwa HALMASHAURI YA JIJI LA ...
Kama tu Ukiwa katika roundabout ya Impala au pale Mianzini au sanawari mataa unasalimiwa "TAKWENYA'Inakuwaje umekutana na mtu katikati ya jiji mfano sokoni hamjuani lakini anakuongelesha kisukuma? Huu ni ushamba uliopitiliza.
Me nilikua najua hv pia ila Tamisemi wakaja na tofauti kabisambona hizi huzisemiView attachment 2320103View attachment 2320104
Majiji yanapata wp maeneo ya mashamba,!? Sheria za majiji ikoje kuhusu mashamba?Inakuaje kilimo na ufugaji ikawa moja ya source of income kwenye jiji?
Yaan hapo nyamagana na ilelemela wanalima kwa kiwango hicho?
Au umechanganya mwanza mkoa na jiji?
Sent using Jamii Forums mobile app
Majiji yanapata wp maeneo ya mashamba,!? Sheria za majiji ikoje kuhusu mashamba?
Kwahyo ume mind sio [emoji3]Stick kwenye uzi wako wa Depo!! Mwanza Mjini hicho kitu hakipo hata Shy kama mtu hakufaham hicho kitu sijakiona kabisa ila vijjini ilo suala lipo Sana na ndio nlpo natafuta mlo wangu wa kila siku
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Sio mwaka 2002 ni mwaka 2000 ndo Mwanza ilikuwa JijiKwa wengi msioifahamu Mwanza jiji ( Mwanza city) au The Rock City , ni jiji la pili Tanzania baada ya jiji la Dar es salaam.
Jiji hili lilipewa hadhi ya kuwa Manispaa mwaka 1978 na mwaka 2002 tarehe 07 mwezi wa 07 likapandishwa hadhi ya kuwa jiji la Mwanza , lenye wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana na jumla ya kata 20, 9 Ilemela na 11 Nyamagana . Nyamagana ndio yalipo makao makuu ya jiji la Mwanza.
UTAWALA
Baada ya jiji la Mwanza kupanuka , liligawanywa sehemu mbili yaani halmashauri ya jiji la Mwanza yenye wilaya moja ya nyamagana, hapo kuna mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza, mkuu wa wilaya ya Nyamagana pia halmashauri ya Manispaa ya Ilemela yenye wilaya ya Ilemela , Kuna mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela, mkuu wa wilaya wa wilaya ya Mwanza.
Hapo Ni kiutawala tu lakini huwezi kuitenganisha Mwanza ( Ilemela na Nyamagana) zilizokuwa tarafa za halmashauri ya manispaa ya Mwanza hadi mwaka 2002.
IDADI YA WATU
Kwa sasa tunasubiri takwimu za watu na makazi za mwaka 2022, hata hivyo inakadiriwa kuwa na watu milioni tatu hadi sasa.
VYANZO VYA MAPATO
Biashara, kilimo na ufugaji, kwa takwimu za mwaka huu hadi kufikia mwezi wa 6 mwaka huu halmashauri ya jiji imeweza kuchangia Tsh bilioni 17 Kama pato la ndani huku halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ikichangia Tsh bilioni 10 na kufanya Mwanza jiji kuchangia Tsh bilioni 27 kwa mujibu wa TAMISEMI.
ELIMU
Jiji la Mwanza lina vyuo vikuu kamili viwili , vyenye makao yake makuu jijini Mwanza yaani SAINT AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA ( SAUT) na CATHOLIC UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIEND SCIENCE ( CUHAS) zamani au maarufu Weill Bugando University vyote vinamilikiwa na kanisa katoliki Tanzania kupitia TEC ( Tanzania Episcopal Conference) , hakuna chuo kikuu cha serikali jijini Mwanza ( Serikali Sasa ione umuhimu kujenga chuo kikuu Mwanza, University of Mwanza, ( UoM) kiweze kushinda na UdSm, UDOM, na Nelson Mandela.
WENYEJI
Wenyeji wa jiji la Mwanza ni kabila la Wasukuma ( Wang'weri) , yaani wasukuma wa magharibi .
Karibuni jijini Mwanza kwa fursa mbalimbali.
Imeandikwa na mimi Malika.
Kwa maoni ushauri, karibuni kwenye uzi.
Kwamba jiji la Mwanza lina kata 20?Yaani tumekukaribisha juzi juzi unaanza kujifanya kujua hili jiji?Hapo kwenye wilaya mbili, mzee umetupiga kakamba flani hivi. Kuna wilaya nyingine kama magu, sengerema, ukerewe, misungwi n.k
Kuna vitu vingi sana hapa vinapwaya, but all in all tunashukuru kwa
Kata? Wapi nmeongelea kata mkuu?Kwamba jiji la Mwanza lina kata 20?Yaani tumekukaribisha juzi juzi unaanza kujifanya kujua hili jiji?
Laki 6 ilikua Arusha na Mwanza ilikua 1.2 milion,ukiondoa Dar es Salaam mji wa Mwanza ni mji wa pili kwa kua na watu wengi zaidiJiji la mwanza haliwezi kufika watu mil 3 never, sensa iliyopita population ilikua laki sita na nusu ilemela na nyamagana sasa itafikaje mil 3 kwa muda mfupi hivi ?,mwanza iko over rated
Hapo Ilemela ipo omitted soma vizuri uziMwanza nilijua ni jiji lenye hela kuliko Arusha, lakin kumbe limepitwa na Arusha banah,,
1. Dar-75.3B
2. Dom-45.1B
3. Arsh-24.3B
4. Mwnz-17.7B
5. Tanga-17.4B
6. Mby-16B
Yaani ikizubaa Tanga wanapga kiwiko
Mkuu inaonekana hujui hata ulichoandika.Hujazungumza habari za kata?🤣🤣Kata? Wapi nmeongelea kata mkuu?
Besides, i was born and raised in mwanza, how come umenikaribisha?
👆👆👆👆 this is exactly what i wroteHapo kwenye wilaya mbili, mzee umetupiga kakamba flani hivi. Kuna wilaya nyingine kama magu, sengerema, ukerewe, misungwi n.k
Kuna vitu vingi sana hapa vinapwaya, but all in all tunashukuru kwa kupaisha jiji letu
Haya mtaalam mwenye PHD ya mwandiko, kusoma na ku-quote comments kutoka chuo cha Jamii Forum , nisaidie kunionyesha wapi nmeandika masuala ya kata hapo juu?Mkuu inaonekana hujui hata ulichoandika.Hujazungumza habari za kata?🤣🤣
🤣🤣🤣🤣🤣Sorry mkuu nilikosea kuquote post yako nilimtarget mleta mada👆👆👆👆 this is exactly what i wrote
Haya mtaalam mwenye PHD ya mwandiko, kusoma na ku-quote comments kutoka chuo cha Jamii Forum , nisaidie kunionyesha wapi nmeandika masuala ya kata hapo juu?
Au ulikurupuka usingizini vidole vinawasha kutype?
Punguza chuki kwa watu wa Mwanza, mlengo wako wa kisiasa isiwe shida kwetu.Tanzania ina majiji 3 tuu ya maana,
Dar,Dom,Arusha..
Hayo mengine ni mlundikano wa maskini mjini tuu.
Amezungumzia Jiji la Mwanza siyo mkoa was MwanzaHapo kwenye wilaya mbili, mzee umetupiga kakamba flani hivi. Kuna wilaya nyingine kama magu, sengerema, ukerewe, misungwi n.k
Kuna vitu vingi sana hapa vinapwaya, but all in all tunashukuru kwa kupaisha jiji letu