Ijue Mwanza jiji

Ijue Mwanza jiji

Jiji la Mwanza limeundwa na wilaya mbili lakini lina jumla ya kata 20 wakati jiji la Mbeya limeundwa na Manispaa moja tu lakini lina kata 36
 
Kwa wengi msioifahamu Mwanza jiji ( Mwanza city) au The Rock City , ni jiji la pili Tanzania baada ya jiji la Dar es salaam.

Jiji hili lilipewa hadhi ya kuwa Manispaa mwaka 1978 na mwaka 2002 tarehe 07 mwezi wa 07 likapandishwa hadhi ya kuwa jiji la Mwanza , lenye wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana na jumla ya kata 20, 9 Ilemela na 11 Nyamagana . Nyamagana ndio yalipo makao makuu ya jiji la Mwanza.

UTAWALA
Baada ya jiji la Mwanza kupanuka , liligawanywa sehemu mbili yaani halmashauri ya jiji la Mwanza yenye wilaya moja ya nyamagana, hapo kuna mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza, mkuu wa wilaya ya Nyamagana pia halmashauri ya Manispaa ya Ilemela yenye wilaya ya Ilemela , Kuna mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela, mkuu wa wilaya wa wilaya ya Mwanza.

Hapo Ni kiutawala tu lakini huwezi kuitenganisha Mwanza ( Ilemela na Nyamagana) zilizokuwa tarafa za halmashauri ya manispaa ya Mwanza hadi mwaka 2002.

IDADI YA WATU
Kwa sasa tunasubiri takwimu za watu na makazi za mwaka 2022, hata hivyo inakadiriwa kuwa na watu milioni tatu hadi sasa.

VYANZO VYA MAPATO
Biashara, kilimo na ufugaji, kwa takwimu za mwaka huu hadi kufikia mwezi wa 6 mwaka huu halmashauri ya jiji imeweza kuchangia Tsh bilioni 17 Kama pato la ndani huku halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ikichangia Tsh bilioni 10 na kufanya Mwanza jiji kuchangia Tsh bilioni 27 kwa mujibu wa TAMISEMI.

ELIMU
Jiji la Mwanza lina vyuo vikuu kamili viwili , vyenye makao yake makuu jijini Mwanza yaani SAINT AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA ( SAUT) na CATHOLIC UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIEND SCIENCE ( CUHAS) zamani au maarufu Weill Bugando University vyote vinamilikiwa na kanisa katoliki Tanzania kupitia TEC ( Tanzania Episcopal Conference) , hakuna chuo kikuu cha serikali jijini Mwanza ( Serikali Sasa ione umuhimu kujenga chuo kikuu Mwanza, University of Mwanza, ( UoM) kiweze kushinda na UdSm, UDOM, na Nelson Mandela.

WENYEJI
Wenyeji wa jiji la Mwanza ni kabila la Wasukuma ( Wang'weri) , yaani wasukuma wa magharibi .
Karibuni jijini Mwanza kwa fursa mbalimbali.

Imeandikwa na mimi Malika.
Kwa maoni ushauri, karibuni kwenye uzi.
Inakuaje kilimo na ufugaji ikawa moja ya source of income kwenye jiji?

Yaan hapo nyamagana na ilelemela wanalima kwa kiwango hicho?

Au umechanganya mwanza mkoa na jiji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IDADI YA WATU
Kwa sasa tunasubiri takwimu za watu na makazi za mwaka 2022, hata hivyo inakadiriwa kuwa na watu milioni tatu hadi sasa
Mwanza jiji haiwezi kuwa na wakaazi milioni 3. Hata mkoa mzima wa Mwanza hauna idadi hiyo ya watu
 
Tanzania ina majiji 3 tuu ya maana,
Dar,Dom,Arusha..

Hayo mengine ni mlundikano wa maskini mjini tuu.
Mbona mkoa unaoongoza kwa omba omba ni Dom? Sema mwanza inakuumiza kichwa kinoma, walikataa mimba yako nini? Hakuna mtanzania mwenye hela asiyependa kuishi mwanza. Unatutajia arusha kwenye vumbi kama poda 😂😂 Mwanza haitishwi na vinyago km dom au arusha. Mkizingua semeni tuwakatie maji kutoka victoria muendelee na ya chumvi.
 
Hapo kwenye wilaya mbili, mzee umetupiga kakamba flani hivi. Kuna wilaya nyingine kama magu, sengerema, ukerewe, misungwi n.k
Kuna vitu vingi sana hapa vinapwaya, but all in all tunashukuru kwa kupaisha jiji letu

Ameongelea Jiji la Mwanza na sio Mkoa wa Mwanza.
Hivi ni vitu viwili tofauti.
Unapoongelea jiji la Mwanza unamaanisha ni Ilemela na Nyamagana hizi wilaya mbili ndio zinaunda jiji LA Mwanza. Na wanaobeba gharama za uendeshaji ni Nyamagana kama ilivyo kwasasa Dar es salaam Ilala ndio inabeba gharama. Jiji LA Dar es salaam wilaya zake zote zimo ndani ya jiji tofauti na Mwanza, Kwa Mwanza wilaya zenye hadhi ya Manspaa ni mbili tu yaani ilemela na nyamagana tu, zilizobaki zote ni halmashauri za mji wilaya tofauti na Dar wilaya zake zote zina hadhi ya manispaa.
 
Back
Top Bottom