Ijue Rwanda, Kagame, Museveni na Uvamizi wao katika Ardhi ya Congo


Nami naona kama kweli walisaini hiyo makubaliano basi ni lazima Kabila akubali,

Watu walipoteza maisha yao kwa hiyo makubaliana sharti watimiziwe
 
Mkuu MKAMASIMBA

Nimeweka vyanzo vingi sana vya makusanyo yangu ya makala haya, mimi ni Mtanzania tena Mhehe wa Nyololo Iringa, sina sababu ya kuwapendelea Watutsi ikiwa kuna habari zaidi za Wahutu,

Nimesimulia yale niyajuayo kupitia vyanzo vyangu, ikiwa kuna lolote unalolijua ambalo litaweka uwiano wakihistoria kati ya Watutsi na Wahutu basi ni vema uweke hapa wote tufaidi
 
 
Mkuu hujamwelewa hasa anachozungumza,Katika hili tukiweka hisia tukautenga ukweli halisi tutakuwa tunakosea,
Mkuu YN, KOBA ana akili sana - tukumbuke ana wajibu wa kumtetea PK na ndugu zake which's healthy, binafsi nafikili wakati mwingine tusimulahumu SANA. Siku moja nilicheka sana, aliwahi kuanzisha thread za kumlahumu/shutumu PK na kutoa link zenye kuweka chumvi mno za kumsema sema sana PK. Kilicho nishangaza baadhi ya wana JF wali swallow hook, line, and sinker wakifikili ndugu KOBA kamugehuka PK!! Mimi nilijua hiyo ni janja ya KOBA anataka kuwachota akili wasomaji - ni hilo tu, na ndicho kilicho tokea. Kunisema kwamba kumbe mimi ni mtu wa Kigoma hiyo ni njia mmoja wapo ya kutuma ujumbe fulani kwa kuwa amekwisha nisoma na kujua kwamba deep down siwachukii Watutsi per se, kinacho nichukiza ni viongozi wao kupenda penda kupigana vita na kuwa na mawazo ya kifahidhina ambayo ndio yanaweza kuwa chanzo cha kufanya Raia wa maziwa makuu kushindwa kuelewana na kuanzisha vurugu zisizo na kikomo, mimi sina matatizo na Watutsi wahadirifu walio wengi, nilisha sema nimebahatika kukaa nao kwa karibu tangu nikiwa mdogo nimejifunza mambo mengi kuhusu tamaduni zao, lugha yao, falme zao, matazo yao ya jadi na Wahutu, imani zao nk.
 

Kibanga nadhani umetoka kwenye mstari kishabiki!

mtoa thread amejitahidi kugusa maeneo mengi iwapo unataarifa pia tuwekee tusome. Napingana na wewe kuwa Amini alivamia Tanzania kupiga watusi, huo ni uwongo nadhani unataka kuchafua mada sijui Kwa lengo gani. Ikumbukwe kua hata Obote alikuwa hapa Tanzania baada ya kupinduliwa na TAnzania iliendelea kumheshimu Kama head of state wa Uganda. Nadhani hilo ndilo lilimchukiza sana Idd Amin. Pia habari ya kagame na Museveni kuandaliwa na Nyerere Kwa makusudi ya kutawala Rwanda na Uganda ni uzushi wa wahutu hasa walioshiriki mauaji ya kimbali.
 

Kibanga nadhani umetoka kwenye mstari kishabiki!

mtoa thread amejitahidi kugusa maeneo mengi iwapo unataarifa pia tuwekee tusome. Napingana na wewe kuwa Amini alivamia Tanzania kupiga watusi, huo ni uwongo nadhani unataka kuchafua mada sijui Kwa lengo gani. Ikumbukwe kua hata Obote alikuwa hapa Tanzania baada ya kupinduliwa na TAnzania iliendelea kumheshimu Kama head of state wa Uganda. Nadhani hilo ndilo lilimchukiza sana Idd Amin. Pia habari ya kagame na Museveni kuandaliwa na Nyerere Kwa makusudi ya kutawala Rwanda na Uganda ni uzushi wa wahutu hasa walioshiriki mauaji ya kimbali.
 
Read between the lines! "inasemekana.....halafu kuhusika sio lazima uwepo physically"
Mkuu unajuwa watu wengine ufikilia wahusika lazima wawe kwenye tukio ndio wahusike na uharifu!! Ukweli wa mambo ni kwamba kulikuwa na tofauti kubwa ya approach au tuseme stratergy ya vita vya msituni kati ya Fred na Kagame, Fred ali-prefer softly softly approach i.e kuelimisha raia kwenye area iliyokombolewa na wapiganaji wa msituni kabla hawajasongo mbele kwenye area nyingine, the idea behind all this ni kwamba kwa kufanya hivyo watahungwa mkono na raia wa Rwanda bila ya kujali ukabila, Kagame na radical wenzake waliona approach ya Fred itawachelewesha sana! Wenyewe walikuwa wanataka approach ya voda fasta. Kati ya Fred na Kagame, Fred alikuwa na experience kwenye nyanja ya vita kuliko Kagame, Fred vile vile aliwahi kushiriki katika vita vya ukombozi wa Msumbiji kama mafunzo, Kagame taaluma yake ilikuwa ni upande wa Intelligency aliyo somea hapa Tanzania. Sasa nini kilitokea - Fred aliongozana na wanajeshi wenzake wa Kitutsi kutoka Uganda na kwenda mpakani mwa Rwanda na Uganda kuanzisha vita vya kumung'oa Rais Habyalimana madarakani yeye akiwa kama kamanda wao, inaelezwa kwamba siku ya kwanza au ya pili Fred alipigwa risasi ya kichwani na kufariki hapo hapo! Wanadai aliuwawa na risasi za adui lakini hiyo si kweli aliye muua na afisa mwenzake ambaye akupendelea approach ya Fred ya softly softly wanasema siyo kwamba Mh.Kagame hakujua kitakacho mtokea Fred eventually kwa kuwa muuaji alikuwa na kawaida ya kuwasiliana na Mh.Kagame akiwa masomoni Merikani sasa nani alitoa amri ya kumumaliza Fred haijulikani. One more thing Fred alikuwa very close na familia ya M7 kuanzia M7 mwenyewe na mkewe na mdogo wake M7 Mh. Col. Salim Saleh, kwa hiyo kifo cha Fred kiliwauzunisha sana. Mkewe M7 aliwahi kunusurika kifo wakati wa vita vya msituni kati ya jeshi la OBOTE na M7, mama huyo alikuwa intercepted kwenye kizuizi cha barabarani na majeshi ya OBOTE, ni Fred na makomando wenzake ndio walimuokoa mama huyo(Jannet). Inasemekana vile vile kwamba M7 alitumia ujanja wa kumpeleka PK kwenye mafunzo ya kijeshi huko Merikani ni (kama alilazimishwa vile) ili hasiwepo wakati vita ya kukomboa Rwanda i.e alipendelea Fred ndiye aongoze vita hiyo - kwa nini? That's a million dollar question, inaelekea M7 na PK don't trust each other by 100% personally namuonaga PK yuko straight forward he speaks his mind without mincing words 'am not sure about M7, miaka ya nyuma walihai kukorofishana walikaa muda mrefu bila ya kujuliana hali!! Kagame hana mchezo bwana.
 

Mkuu umeongea ukweli tupu,

Tatizo ndugu wengi hapa wanazungumza kwa hisia zaidi badala yakuusaka ukweli
 
Ni kichekesho wanyarwanda wana mipango kabambe ya kuiba ardhi ya congo wakati bomu la vita ya ukabila linanunikia nchi kwao. Wa sikilize ushauri wa Rais. kikwete na waishi kwa amani. Maisha ya kunyanyasana kikabila,dini na vinginevyo yamepitwa na wakati.
 
MALCom umenena kweli hilo linawezekana. Ila history hutufundisha tutokako, bado tunahitaji elimu ya kutosha. Kweli mgogoro wa Congo umenifundisha sana historia ya nchi za maziwa makuu. Kumbe wahutu, watusi pia wako Tanzania, Uganda Burundi na Rwanda? Kweli?
 

Kuna mmoja wawadau amelieleza hapo kurasa za nyuma akisema Mwalimu Nyerere alimsaidia PK kuingia madarakani jambo ambalo sio kweli
 
king king Yericko Nyerere

acheni kulalamika huu ndio muda muafaka wa kujipanga na kuikomboa nchi yenu kutoka kwenye mikono ya dikteta huyu anayenuka damu.
 
Last edited by a moderator:

jilaumuni nyie mnaotangatanga, wabongo ni imara! jipangeni huu ndiyo muda wa kuikomboa nchi yenu!
 
jilaumuni nyie mnaotangatanga, wabongo ni imara! jipangeni huu ndiyo muda wa kuikomboa nchi yenu!

Humu ndani kuna watu wanashabikia vita,tena wao risasi ikipigwa ndio watakua wa kwanza kutimua,majambazi yamawashinda eti mnataka vita ya kukomboa tanzania,tanzania imevamiwa nanani? nyie ndio mnaitwa wachochezi shauri yako,kesho usije sema nilikua natania tu,acha watanzania na wanyarwanda waishi kwa amani wapambane na adui umasikini na ujinga.
 

mbona unaishi maisha ya kujishuku? Tanzania haijavamiwa bado tuna uwezo mkubwa sana wa kuwadhibiti hata mpaka wa kagera vita ikianza hamsogei, nilikuwanawahamasiha wahutu waache kulalamika wadai kwa nguvu haki yao ya kuishi kwa amani bila ubaguzi ndani ya rwanda .
 
 
Jeshi la Polisi Tanzania, Usalama wa
Taifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi
Tanzania JWTZ pamoja na Viongozi
wote wa Mikoa husika hakikisheni
mnaendelea na msako wa
kuwaondoa Wahamiaji haramu wote
yaani wale wanaoishi bila Vibali. Pia
zichukuliwe hatua kali za kisheria
kwa wale wahamiaji haramu ambao
hawakutii ule muda muafaka
tuliowapa warudi kwao. Napenda
kuwahakikishia ya kuwa zoezi hili
halitaishia mkoani Kagera tu, bali
Tanzania nzima. Serikali yenu
inafahamu vema walipo hawa
wahamiaji haramu hususani kutoka
Rwanda. Ndugu Wananchi wa
Tanzania, Serikali yetu imepeleka
Batalioni nchini Congo ili kulinda
amani kukabiliana na kukabiliana na
waasi wanaojulikana kwa jina la m23
nchini humo.
Waasi hawa m23 wataondoka nchini
DRC muda si mrefu kwa kipigo kizito
watakachokipata kutoka kwa
majeshi ya UN yaliyopo DRC
yakiongozwa na Brigedia Jenerali
James Mwakibolwa. Wakishaondoka
Congo UTAPITA MSAKO WA HALI YA JUU
SANA ILI KUWAONDOA WARWANDA
NCHINI HUMO. Napenda
kuwahakikishia ya kwamba HAKUNA
NCHI YOYOTE INAYOWEZA IKATUTISHIA
AMANI WATANZANIA. Tunaliamini JWTZ
kwa kuwa lipo Imara sana, ndani na
nje ya Tanzania.
Ni mimi Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia JamiiForums. Mungu Ibariki
Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni kwa Kunisikiliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…