IJUE SHERIA: Namna ya kumsaidia ndugu yako kupata dhamana Polisi


Jiongeze mtoto wa kiume usipende kutafuniwa kila kitu.....na hili ndio tatizo letu vijana sisi siku hizi hatutaki kusumbua akili zetu kabisa jamaa amekupa elimu kiasi basi nawe sumbua akili basi hata kidogo. TAFUTA KATIBA YA TANZANIA SOMA
 
Jiongeze mtoto wa kiume usipende kutafuniwa kila kitu.....na hili ndio tatizo letu vijana sisi siku hizi hatutaki kusumbua akili zetu kabisa jamaa amekupa elimu kiasi basi nawe sumbua akili basi hata kidogo. TAFUTA KATIBA YA TANZANIA SOMA

Siyo kwa ajiri yangu, ni kwa ajiri ya kuwasaidia wengine hambao hawajui watapata hayo maelezo wapi. Yani itakuwa vizuri kama hapa kutakuwa na maelezo yote (one stop shop) kuwa mambo ya dhamana (different scenarios).

Mtu anaweza kukamatwa halafu hana muda mwingi wa kutafuta information about his right, labda yuko ndani (Jela). Na labda anapewa dakika kumi tu kutumia simu yake. Sasa kama anaweza kuja hapa na akapata kitu kitakachomsaidia ni vizuri, au wewe unaonaje? Hii ndiyo maana ya majadiliano kusaidiana.

Unajua ukiwa unataka dhamana hauwezi tu kumwambia polisi sheria ina sema ni haki yangu na kupata dhamana.

Inabidi ujue kipengele kinachokupa dhamana, hata akiende kukisoma anaona uko kweli. Inabidi useme kutokana na katiba, section.., paragraph ..., kifungu namba..., sheria ya mwaka... inanipa haki ya kupata dhamana. Kwahiyo naomba dhamana kutokana na hiyo kipengele cha katiba ya Tanzania. Watajua unajua kitu gani unachosema na unajua sheria na umesoma katiba.

Mkuu, Mwache Mkuu aliyeanzisha uzi ajibu au mtu mwingine. Calm down a little bit life is too short.
 
Samahani mkuu mie imenikuta tatizo la kukosa dhamana kwa mdogo wangu anayeshitakiwa kwa kumpa ujauzito.mwanagunzi japo sina uhakika kama kweli aliempa ni huyu mdogo wangu,,,, ajabu nilifuata taratibu zote za kupata dhamana kutoka serikali ya kijiji kuanzia kwa mwenyekiti wangu wa kitongoji.mpaka ofisi ya mtendaji kijiji na kata na nikapewa nakala za utambulisho,

Ajabu kufika mahakamani hakimu baada ya kumsomea mashitaka yake mdogo wangu na kusema dhamana iko wazi akaomba watu wawili wa kumdhamini nikatoka mie na ndugu yangu kila mmoja na vielelezo husika tatzo likaja hakimu kutotambua udhibitisho wetu akidai tuwasilishe hati za mali isiyohamishika kama nyumba au kiwanja wakati vielelexo vyote kutoka kwa afsa mtendaji vikieleza bayana maana kama hati sehemu ninapoishi hakuna hati wala ofa. Ningependa kujua hii ni sawa kweli mkuu maana baada ya kutoa pesa kiasi cha laki tano dhamana ilikubaliwa hapo ndipo nilibaki na mshangao..

Na ningependa kujua kosa.la watoto kupeana ujauxito.linadhaminika au la maana mdogo wangu ana miaka kumi na sita lakini kahitimu kidato cha nne.mwaka jana na kubahatika kuendelea na masomo lakini aliyepewa mimba.ana umri wa.miaka kumi na nane hivyo ningependa kujua aliyebakwa ni yupi kati ya hawa watoto'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole na maswahibj ya dogo ila dogo mbaya kamtia mimba mtu anayemzidi umri.
 
Hivi polisi akikunyima dhamana kwa makusudi unaweza kuwafungulia kesi na wao kwa kosa hilo la kukunyima dahamana?? Maana mtu anaweza kuonga polisi ilimladi ulale ndani tuuuu..
 
Shukrani kwa elimu mkuu,,umefanya vema sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dhamana ni haki ya msingi ya mtuhumiwa na siyo hatua Mkuu.
Nafahamu hilo mdau ila katika kuhakikisha unapata haki yako ya misingi lazma kuna hatua unazofuata . hivyo kama ilivyo katika damana , ili uweze kumwekea mtu dhamana kuna masharti na hatua lazma uzikamilishe ndipo upate haki yako
nashukuru sana mkuu
soma hyo attachment niliyokutumia hapo utaweza kupata A B C ya vifungu vinavyoonyesha haki za mtu aliyetiwa nguvuni , pia kitakuonyesha makosa gani mtu atapatiwa dhamana na yapi hawezi patiwa dhamana na ni kwa nini . mfano makosa ya uhujumu uchumi na mauaji kwa kukusudia huwezi patiwa dhamana
 

Attachments

Yani ukijua sheria ni raha sana..
Ngoja nianze kusoma OUT...
Maana sasa ukisema utafute mwanasheria ujue lazima uwe na ela ndeefu...

Kujua sheria ni kama kujua lugha...huwezi pata shida mjini...
Asante kwa darasa la bure kaka!
 

nzuri, thanks.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana mbunge wa Singida Mashariki Mhe.Tundu Lissu, kinyume na maombi yaliyowekwa na mawakili wa Jamhuri ya kuzuia asipewe dhamana.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri amesema, baada ya kupitia hoja za serikali na majibu ya mawakili wa utetezi, haoni mantiki ya kuzuia dhamana kwa Lissu. Hivyo mahakama hiyo imemuachia Lissu kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.10 milioni, kila mmoja.!
 
mkuu somo zur,kwa maana hiyo kama nilivyosikia leo kua Tundu Lissu katoka kwa dhamana ya milioni 10 ,inamaana hayo ni maandishi tu ?na hakuna pesa iliyotolewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…