IJUE SHERIA: Namna ya kumsaidia ndugu yako kupata dhamana Polisi

IJUE SHERIA: Namna ya kumsaidia ndugu yako kupata dhamana Polisi

tatizo la askari wetu ni kujifanya wanajua sana, ukienda pale ukajifanya unaelewa mambo kama hivi mwisho wa siku yule aliyepo ndani ndio ataumia. watakufanyia sifa kwa kukulaza ndani zaidi ya hata ungejifanya mpole na kama huyajui hayo mambo. asante sana mkuu kwa elimu uliyoitoa ila nikukumbushe tuu police hawatoi elimu hiyo maana ndipo wanapopatia zao za kusuuza makoo.
 
mkuu somo zur,kwa maana hiyo kama nilivyosikia leo kua Tundu Lissu katoka kwa dhamana ya milioni 10 ,inamaana hayo ni maandishi tu ?na hakuna pesa iliyotolewa?

Sio Maandishi tu, inabidi uonyeshe unauwezo wa kulipa hizo pesa, wanaweza kuangalia assets, bank accounts, salary, your job, your business.
 
Dhamana ni haki ya msingi ya mtuhumiwa na siyo hatua Mkuu.

Mbona amesema kuwa ni haki ya mtuhumiwa na makosa yasiyodhaminika? Na ameenda mbele zaidi kuonesha hatua za kufikia hiyo haki.
 
Hakumlazimisha mbali mambo yote anavyodai mzazi wa mtoto wa kike walikua wanakutana gesti kwa makubaliano.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa kama walikuwa wamekubaliana hiyo ni sheria nyingine inayowahusu minors ( watoto wakifanya mapenzi), Kumbaka ni sheria nyingine kabisa. shitaka lilikuwa lipi?

Kwa sababu kumpa mimba mtu siyo illegal. Kumpa mtoto mimba (miaka midogo zaidi ya 18 ni illegal) Kama wote wawili ni watoto na wamekubaliana kufanya mapenzi ni sheria nyingine kabisa? adhabu siyo kubwa sana.

Kwa hiyo tunatakiwa tujue exactly what was he charged for (what was on the charge sheet)?
 
Sasa kama walikuwa wamekubaliana hiyo ni sheria nyingine inayowahusu minors ( watoto wakifanya mapenzi), Kumbaka ni sheria nyingine kabisa. shitaka lilikuwa lipi?

Kwa sababu kumpa mimba mtu siyo illegal. Kumpa mtoto mimba (miaka midogo zaidi ya 18 ni illegal) Kama wote wawili ni watoto na wamekubaliana kufanya mapenzi ni sheria nyingine kabisa? adhabu siyo kubwa sana.

Kwa hiyo tunatakiwa tujue exactly what was he charged for (what was on the charge sheet)?
Wamemfungulia shitaka la kubaka na kusabisha mimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu binafsi nimelipenda darasa ila kitu kimoja sijajua bado kwahiyo ukisikia Fulani kapewa dhamana kwa sh kadhaa mahakamani maaana yake nini hiyo hela analipa ndo anapewa dhamna au ikitokea katoweka mdhamini hulipa hyo hela
 
Mkuu binafsi nimelipenda darasa ila kitu kimoja sijajua bado kwahiyo ukisikia Fulani kapewa dhamana kwa sh kadhaa mahakamani maaana yake nini hiyo hela analipa ndo anapewa dhamna au ikitokea katoweka mdhamini hulipa hyo hela

Ikitokea katoweka ndiyo unalipa. Lakini unabidi uwaonyeshe ushaidi kabisa unaweza kulipa hizo pesa kabla kumpa dhamana.
 
Wamemfungulia shitaka la kubaka na kusabisha mimba.

Sent using Jamii Forums mobile app

sasa kubaka ni shikata kubwa, adhabu ni kubwa zaidi ya kama wote ni watoto walikubariana adhabu yake ni kama warning. Sasa kama wewe unaweza kuchukua mawasiliano yao yote, kwenye phone calls, emails, whatapps, skype's, facebook, instagrams, twitter, text messages, letters, picha, mashahidi (majirani, wanafunzi, marafiki, ndugu) kusema kama walikubariana, waliwaona wanapendana, unaweza kushinda hii case .

Lakini unatakiwa kuwa na evidence (ushahidi) to prove your case. Pia kama unaweza kuongea na huyu Msichana kama akasema anampenda huyu kijana na akulazimishwa bali walikuwa wanapendana na walikubariana utashinda hiyo case.

Mkuu kama unaweza tafuta wakili mzuri akusaidie.
 
kama unawafahamu polisi utaelewa kwamba namna ya kumsaidia ndugu yako kupata dhamana ya polisi ni kwenda na hela mfukoni, kwa mahakamani hakuna hakimu asiyekula rushwa, hata akikuambia hali ni mwongo. hiyo ndiyo dunia ambayo mwenyezi Mungu alipoiumba alitarajia itakuwa na watoa haki, watu wakaamua kuwa hivyo. nimefanya mahakamani muda mrefu hadi leo nafanya mahakamani, hakuna sehemu wanakula rushwa kama polisi na mahakama. anayebisha anyooshe mkono.
 
Asante, umesema dhamana hutolewa bure

maswali:-

1) Kama mtu hana kazi na hana watu wakumdhamini, umesema anaweza kujidhamini mwenyewe, vitu gani itabidi avitoe ili aruhusiwe kujidhamini?
2) Kama mtu alipewa dhamana akakimbia, (kosa lilikuwa dogo kama labda kutukunana), akikamatwa bado anaweza kupewa dhamana ya pili?
3) Unayo List ya makosa watu wanaweza kupewa dhamana na makosa ambayo watu hawawezi kupewa dhamana? iyo itawasaidia watu,
4. Unaweza kuonyesha kuweka website ya government na vifungu vinavyo onyesha rights za mtu aliyekamatwa?



naomba nikujibu kama ifuatavyoo kwa kufuata mtiririko wa maswali yako
1. kama mtu hana kazi na hana mdhamini anaweza kujidhamini kwa kuapewa fomu maalumu atakayosaini na kuijaza ,
2. kwanza napenda nikueleze kuwa kutukana mtu siyo kosa ndogo ni kosa kama makosa mengine tu ya jinai , kwa kuwa amemvunjia mtu utu wake kwa kumdhalilisha kwa kumtusi hivyo lazma sheria ifuate mkondo wake ,. endapo atapatiwa dhamana na kutoroka akitiwa nguvuni inawezekana kutpatiwa dhamana tena kwakuwa atakuwa ameonyesha utovu wa nidhamu kwa kutokamilisha mashart aliyopewa baada ya dhamana
3. makosa ambayo mtu hawezipewa dhamana ni kama Uhujumu uchumi , makosa ya ugaidi, mauaji n.k
4. pitia hapo utapata majibu ya swali la 4 https://tls.or.tz/publication/view/zijue-haki-za-raia-katika-mfumo-jinai2/
 
Dhamana ni Haki na Siyo Upendeleo

Kwa kuwa dhamana ni haki ya mtu, hivyo anapoomba hapaswi kukataliwa bila sababu za msingi. Mahakamani na wanaharakati wa haki za binadamu wamesisitiza mara nyingi kuwa dhamana ni haki ya mshitakiwa pale anapotimiza masharti yake; kumnyima dhamana bila sababu ya msing ni kumkosesha haki ya msingi ya kuwa huru kwa mujibu wa sheria ( Ibara ya 13 kifungu kile cha 1 cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kinasema kwamba “ watu wote ni sawa mbele ya sheria , na wanayo haki, bila ubaguzi wowote, kulindwana kupata haki sawa mbele ya sheria”. Vile vile polisi au mahakama inapokataa kutoa dhamana ni lazima kuwe na sababu nzito zenye kuridhisha kabla ya kufikia uamuzi huo.

Hapa Tanzania uzoefu umeonyesha kuwa ni kesi za mauaji, wizi wa kutumia silaha na uhaini tu ambazo kutokana na uzito wake mtuhumiwa hawezi kuwekewa dhamana ila kesi nyingine zote zilizobaki, mshitakiwa anayohaki ya kuwekewa dhamana, pindi akitimiza masharti ya dhamana na mahakama ikaridhika. Kwa msingi huu dhamana ni haki ya mshitakiwa na kupewa dhamana ni katika kutimiza haki hiyo ya msingi.

Mahakama inaweza kukataa kutoa dhamana iwapo itakuwa imeridhika kuwa kutolewa kwa dhamana kutaharibu maana nzima ya kesi hiyo kuwepo mahakamani, kutavuruga kesi hiyo, au mshitakiwa anaweza kupata madhara ikiwa ataruhusiwa kurudi kwa jamii. Hali hii ndiyo inayosababisha kesi za mauaji na uhaini kukataliwa dhamana kwani adhabu yake ni nzito (kifo) ambapo ni rahisi mshitakiwa kushawishika kutoroka
 
DHAMANA NI NINI?

Dhamana ni hatua ambayo mtuhumiwa wa kosa fulani huachiwa huru kwa muda, ili kusubiri hatua za kufikishwa mahakamani, au kama tayari amefikishwa mahakamani husubiri kuendelea na kesi kwa siku zijazo.

Kwa hiyo, ili lije suala la dhamana ni lazima uwe umetuhumiwa polisi au tayari umefikishwa mahakamani. Ieleweke kuwa kuna aina kuu mbili za dhamana. Kwanza dhamana ya polisi na pili dhamana ya mahakamani. Hapa tunazungumzia dhamana ya polisi.

UKIOMBWA FEDHA KWA AJILI YA DHAMANA KATAA

Dhamana hutolewa bure. Ieleweke wazi kuwa hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana. Mchezo huu wa kuomba fedha ili mtu apate dhamana umetamalaki zaidi vituo vya polisi.

Wewe kama raia, unalotakiwa kujua ni moja tu kuwa hakuna sheria inayomtaka raia kutoa fedha ili apate dhamana. Serikalini hakuna risiti ya malipo ya dhamana. Kama wewe utaamua kutoa fedha hiyo ujue umetoa kwa sababu zako lakini sheria iko hivyo. Ifikie hatua raia wajisimamie kwa kukataa kutoa fedha kununua dhamana.

Hakuna kitu ambacho askari anaweza kukufanya ikiwa utakataa kutoa fedha kwa ajili ya dhamana. Hakipo kabisa kinachohitajika ni ujasiri wako tu kwa kumwambia askari kwamba ‘sikupi fedha kwa kuwa dhamana hainunuliwi.

Usikubali kutoa fedha kwa ajili ya dhamana, ni kosa na fedha hizo ni rushwa. Na hiyo ni kwa dhamana zote — ya polisi pia ya mahakamani. Katika taratibu za kupata dhamana hamna kulipa fedha.

POLISI WANALAZIMIKA KUKUPA DHAMANA

Hapo juu nimesema kuwa ili upate dhamana hutakiwi kutoa chochote kitu isipokuwa kuna mambo yanazingatiwa ili upate dhamana.

Baadhi ya mambo hayo ni haya;

(a) Kisheria ikiwa makazi yako au anuani yako ya makazi inajulikana vyema au haijulikani, lakini umewafanya polisi kuijua na wakajiridhisha kwamba kweli fulani haya ndiyo makazi yake, basi ni sababu ya kupatiwa dhamana. Hii ni kwa sababu lengo kuu la dhamana ni ili utakapohitajika upatikane kwa urahisi.

(b) Ikiwa kosa alilotenda mtu ni la kudhaminika, hakuna haja ya kuendelea kumshikilia. Sheria imeshaweka wazi makosa yapi dhamana ya mtu itolewe na makosa yapi isitolewe. Baadhi ya makosa ambayo mtu hatakiwi kupata dhamana ni kama kuua kwa kukusudia (murder), uhaini (treason), wizi wa kutumia silaha na kadhalika.

Ajabu ni kuwa kwenye vituo vyetu vya polisi unakuta hata mwenye kosa la kutukana naye ananyimwa dhamana. Hii ni kinyume cha sheria na muda umefika wa raia wenyewe kuyakataa haya.

(c) Pia kama mtuhumiwa hana kumbukumbu (criminal records) zozote za uhalifu, nayo ni sababu au kigezo cha kumfanya apewe dhamana haraka. Hakuna sababu ya kuendelea kumshikilia mtu ambaye kwa kumbukumbu hakuwahi kutenda kosa lolote la jinai hapo kabla. Kisheria kutokuwa na kumbukumbu za uhalifu hapo awali ni dalili za uaminifu na ukweli. Hii nayo ni sababu ya kisheria na yafaa izingatiwe sana huko vituo vya polisi.

(d) Pia ikiwa polisi itajiridhisha kwamba mtuhumiwa atatimiza masharti ya dhamana atakayopewa kama kufika siku na saa atakayoamriwa, basi hakuna haja ya kumng’ang’ania. Hii nayo ni kati ya sababu za kisheria ambazo huwa hazipewi nafasi kwenye vituo vya polisi na hivyo kuendelea kulifanya suala la dhamana kuwa gumu.

NAMNA YA KUJIANDAA NA DHAMANA

Ni vema sana unapopata taarifa za ndugu yako kushikiliwa kituo cha polisi kujiandaa na dhamana. Usitoke nyumbani kwenda kituoni bila kujiandaa na dhamana. Na hii ni iwe una uhakika amefanya kosa fulani au huna uhakika. Zaidi kama unajua kosa lake ni la kudhaminika basi umuhimu wa kujiandaa na dhamana huongezeka.

La kuzingatia sana; hakikisha unapotoka nyumbani una barua inayokutambulisha kwa suala la dhamana kutoka Serikali za Mitaa. Ukienda Serikali za Mitaa wanazijua hizi barua. Pia kama ni mwajiriwa usisahau kwenda na kitambulisho chako cha kazi.

Hii husaidia kutopoteza muda kwa kurudishwarudishwa huku ndugu yako akiendelea kusota polisi. Kwa kujiandaa utamwokoa ndugu yako na zahma ya kulala au kukaa selo. Usiende polisi ukiwa hujajiandaa kwa kuwa kufanya hivyo ni kupoteza muda tu.

OMBA KUJIDHAMINI MWENYEWE, INARUHUSIWA

Kuna watu wamekuwa wakikosa dhamana kwa kukosa wadhamini. Lakini polisi wamekuwa hawawaelezi watu hawa haki hii ya kujidhamini wenyewe. Mtu akikosa mdhamini na polisi nao wanakaa kimya mtu anaendelea kusota. Hili si sawa kwa kuwa moja ya majukumu waliyonayo polisi ni kuwaelimisha watuhumiwa haki zao za msingi.

Aidha, kama ulikuwa hujui ndiyo ujue kuanzia leo kuwa inaruhusiwa kujidhamini mwenyewe na ukaondoka kituo cha polisi bila kuhitaji ndugu yeyote kukudhamini.

Unachotakiwa kufanya kama uko mikononi mwa polisi ni kusema tu kwamba ‘nahitaji kujidhamini’ ili upewe fomu maalum uijaze na uondoke. Usisahau kuliomba hili ni haki yako.
ASANTE MKUU KWA ELIMU HII,SWALI LANGU KAMA POLISI AKININYIMA AU AKINISUMBUA AU AKIWEKA MAZINGINGIRA YA RUSHWA ILI NIMDHAMINI AU NIJIDHAMINI MWENYEWE.NI HATUA GANI NIFANYE AU NI ILI HAKI YANGU HII ISIPOTEE BURE?
 
ASANTE MKUU KWA ELIMU HII,SWALI LANGU KAMA POLISI AKININYIMA AU AKINISUMBUA AU AKIWEKA MAZINGINGIRA YA RUSHWA ILI NIMDHAMINI AU NIJIDHAMINI MWENYEWE.NI HATUA GANI NIFANYE AU NI ILI HAKI YANGU HII ISIPOTEE BURE?
unaaswa kumripoti kwa mkuu wake wa kitu na kama mkuu wake wa kituo ukahisi au asipochukua hatua yoyote unaweza fikisha taarifa zako kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
 
Back
Top Bottom