Ijue siri kubwa ya mafanikio ya Yanga

Huu uzi ulikuwa makini sana ni vile kuna baadhi ya watu wameweka ubishi mbele.
 
Hivi Yanga mna akili kweli? Yaani mechi moja tayari mnaona kama mmenyanyua kombe. Kweli aliyewaita Utopolo hakukosea mnakutana na KMC mnajiona mmemaliza

Najua mnajifariji baada ya kushindwa kombe la hisani vyura wakubwa nyie [emoji196]
Maneno ya mwisho ya mtoa mada;
"Muda ni Mwalimu mzuri Sana".
 
Uliijitahidi kubashiri.
 
Kwani Yanga amecheza mechi moja Mkuu.

Umesahau tulivyokimbizwa pale Tanga?

By the way, Nazungumzia Yanga hii ya hivi karibuni kwa ujumla.
Uliongea mambo ya msingi mno 25Aug,2023 na juzi tarehe 5Nov,2023 yakatokea.
Kuna wajinga walikubeza lakini mimi binafsi niliposoma uzi wako nilielewa nini una maanisha,Ni moja ya members mnaotendea haki sana hili jukwaaa akili kubwa katika uwasilishaji wa hoja big up mwamba.
 
Daah wewe jamaa upewe maua yako. Uliliona hili mbali sana asee
 
Hivi Yanga mna akili kweli? Yaani mechi moja tayari mnaona kama mmenyanyua kombe. Kweli aliyewaita Utopolo hakukosea mnakutana na KMC mnajiona mmemaliza

Najua mnajifariji baada ya kushindwa kombe la hisani vyura wakubwa nyie 🐸
Aibu imekujaa unaumbuka saivi.
 
Nakuu maneno ya mleta ya uzi aliyotoa August 25 mwaka huu.
"Hii Yanga ambayo ukikutana nayo inakutesa hadi maji unawezaita Mma? Haijalishi wewe ni nani? Unafikiri ni vipaji pekee? Nasema hivi, Sawa tumechukua Ngao mbele yake, lakini kama tukikutana naye kwenye ligi tukacheza slow hivi? Nasema hivi lazima tunaaibika. Wanaweza wakatengeneza record mpya katika mechi ya derby." Mwisho wa kunukuu

Halafu watu wengine wanajifichia kwenye vivuli vya hujuma, usaliti na uchawi.
 
Hahahahahaha,jamaa aliona mbali siku nyingi
 
Nasubiri kuona Mechi ya kuingia makundi dhidi ya Power Dynamos wanaweza wakamuangushia Jumba hapa au mechi ya ligi na Mtani,
Jamani, manabii hawajafa, bado wanaishi. Wamekufa manabii wa dini, manabii wa soka wanadunda tu.
 
Uliona mbali
Tatizo la mashabiki wengi ni wepesi wa kuua mjumbe badala ya kutafakari ujumbe unaoletwa na mjumbe. Kuna ule msemo "mjumbe hauawi". Hii post ilkuwa ya zaidi ya miezi miwili iliyopita. Watu wali diss lakini matokeo ndiyo hayo bado watu wanatafuta mchawi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…