NANI AMEKUAMBIA USISHIKE, USIONJE WALA USIGUSE NYAMA LEO?
Waumini wa huko Kolosai nao walidanganywa kama wewe, wakafundishwa kwamba eti wasiguse, wasionje wala wasishike vyakula vya aina fulani, wakapewa mafundisho ya kusisitiza umuhimu pia wa kushika siku fulani na sikukuu fulani fulani zikakatazwa eti kwa sababu tarehe za sikukuu hizo hazikujulikana dhahiri. Mambo haya yalimchanganya sana Epafra, mwanzilishi na mchungaji wa kanisa la Kolosai. Alipotuma ujumbe kwa Paulo, Paulo baba yake wa kiroho akaliandikia kanisa ujumbe huu;
Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
Kol 2:20-23 SUV
Sisi tuliokufa pamoja na Kristo, hatutaki tena mafundisho ya awali ya ulimwengu, yanayotuweka chini ya amri isiyohusiana na mpango wa Mungu wa wokovu. Kuna watu wanapenda sana dini za kukatazwa katazwa kila kitu, wanafikiri ndio utakatifu. Utakatifu sio kukatazwa kila kitu, bali ni kukatazwa yale tu yanayoharibu hekalu la Mungu, yaani mwili. Eti, usishike, usionje, usiguse! Ndio inasaidia msalaba kutenda kazi vizuri?
Ujumbe kwa Wakolosai unatufundisha kwamba hakuna kitu unachoweza kuongeza kwenye kifo cha Yesu Kristo ili kifanye kazi vizuri, yaani HUWEZI KUIBORESHA KAZI YA MSALABANI ETI ILI IWE BORA ZAIDI, NI BORA, INAJITOSHEKEZA. Yoh. 19:30
MAKANISA YANAYOFUNDISHA KWAMBA LEO WATU WASILE NYAMA YAMEJITUNGIA TU, HAKUNA MAAGIZO HAYO KWENYE BIBLIA. Makanisa yanayofundisha kuabudu malaika, kushika siku, na kutokusheherekea pasaka, YAMEJITUNGIA TU MAAGIZO HAYO. HAYO NI MAAGIZO YA WANADAMU, SIO MUNGU.
Mafundisho yasiyoweza kuzizuia tamaa za mwili hayafai katika kutunza wokovu na kumtukuza Kristo aliyeinuliwa juu sana aliye kichwa cha Kanisa. Sisi sio watu wa kawaida, maana tulihamishwa tayari, hatuwezi kujifunza mambo ya kule tulikohama, TULIHAMISHWA.
Naye alituokoa katika nguvu za giza, AKATUHAMISHA na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Kol 1:13-14 SUV
Oscar Wissa
Phm Mtoni Sabasaba
Dar Es Salaam, Tanzania
Facebook, Instagram & Twitter: evoscarmaulid