Ijumaa Kuu na katazo la kula nyama

Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu. Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
Kama imani ya kanisa lako inakuruhusu kula nyama wewe kula tu BILA KUHOJI AU KUINGILIA IMANI YA WENGINE

KATAZO LA KULA NYAMA SIKU YA IJUMAA KUU NI SHERIA YA KANISA KATOLIKI

AHSANTE
 
Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu. Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
Wakristu gani wamekatazwa kula nyama Ijumaa kuu?
 
Unapingana na maandiko.Kuna sehemu kwenye injili,niliiona mwaka 1960 kabla ya Uhuru wa Tanganyika,kwamba kama yote aliyoyatenda na kuhubiri bwana Yesu yangeandikwa,vitabu vya dunia hii visingetosha.
Duh[emoji2][emoji2],et vitabu visingetosha[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hiyo Amri aliweka Nani?na ukiivunja inakuwaje?
KANISA KATOLIKI ndio walioweka.

Kama ni kosa au sio kosa, kwa mtazamo wangu ni KOSA, kwa aliye mKatoliki - kwasababu hayo ni mapatano/makubaliano ni sheria ya kanisa. Kula nyama kama kanisa lako limekataza na wewe UMEKULA huo ni UTOVU wa nidhamu 🤣🤣. Na KIROHO ipo wazi kabisa, ukivunja mapatano/makubaliano/maagano unastahili VITASA/adhabu.

Kumbuka pia: maPadri wa KATOLIKI hawaoi, Ila waChungaji wa Lutheran wanaoa!
Kwahiyo Kuna mambo ambayo ni SHERIA zilizowekwa na KANISA/dhehebu.
 
Kufa kwa Yesu kristo msalabani ni jambo la furaha, shangwe na ushindi katika imani ya Kikristo maana ndio lilizaaa ukombozi, sasa kwanini watu wakae na huzuni, unyonge na kujinyima?

Wakristo kuleni vinono leo.
Kwa hiyo baba yako akijitolea kufa kwa ajili yako utafurahia hata kama amekuokoa hutohuzunika?😁
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi
 
Ukatoliki una makando kando mengi sana!
Kuna dini zaidi ya 1000 duniani.. siyo lazima uwe mkatoliki.. waachie wanaoamini

Unasema wakatoliki wana makando kando WEWE NI MUNGU MPAKA UHUKUMU DINI YA WENGINE? JE UNA HAKIKA KUWA IMANI YAKO NDIYO MUNGU ANAYOIPENDA?😁
 
D

Duuu!? Yaani unafananisha kutokula nyama kutokana na kuteswa Kwa Yesu na kutokula nyama kutokana na mwizi kukatwakatwa utumbo nje hahahaha ninecheka Kwa kweli
Sasa umecheka nini??, Acha kuchekacheka wakati watu tupo serious na Mfungo.
 
Ukimaliza hilo pia naomba andiko linalosema uvute pumzi ya oksijeni na ule ugali maharage [emoji1][emoji1][emoji1] Wasabato wapuuzi sana
 
Vip wale wenzetu wanaojifanya mchana hawali kitimoto ila usiku baadhi wanaitandika balaa.
 
Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu. Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
Hakuna andiko lolote lile ila imekuwa utamaduni tu,wanaunganisha dots kwamba kumwagika Kwa damu ya Yesu pale msalabani siku kama ya leo ndiyo wakaweka kama kautamaduni
 
Kufa kwa Yesu kristo msalabani ni jambo la furaha, shangwe na ushindi katika imani ya Kikristo maana ndio lilizaaa ukombozi, sasa kwanini watu wakae na huzuni, unyonge na kujinyima?

Wakristo kuleni vinono leo.
Kufufuka kwa Yesu Kristu ndilo jambo la furaha zaidi
 
Kula nyama siyo alama ya furaha..inategemea a na mazingira...Kuna watu kunywa maziwa ni tendon la furaha...so sikubaliani na wewe
Unashauriwa kuacha kula chochote kinachokupa furaha siku ya Ijumaa kuu na kuacha matendo yoyote ya anasa kwa kuwa ni siku ya huzuni

Siyo kuacha kula nyama pekee bali jambo lolote la furaha au anasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…