witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,704
- 47,260
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
True...makanisa mengi yapo against na Bible sijui why[emoji848]Mkristo anaongozwa na Biblia, ukiona hakuna katazo huko ujue kuna mtu kaamua kuongeza maneno yake...
No!Hiyo ilikuwepo kabla ya Yesu kuja.....
Kama imani ya kanisa lako inakuruhusu kula nyama wewe kula tu BILA KUHOJI AU KUINGILIA IMANI YA WENGINENaombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu. Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
Wakristu gani wamekatazwa kula nyama Ijumaa kuu?Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu. Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
Duh[emoji2][emoji2],et vitabu visingetosha[emoji28][emoji28][emoji28]Unapingana na maandiko.Kuna sehemu kwenye injili,niliiona mwaka 1960 kabla ya Uhuru wa Tanganyika,kwamba kama yote aliyoyatenda na kuhubiri bwana Yesu yangeandikwa,vitabu vya dunia hii visingetosha.
KANISA KATOLIKI ndio walioweka.Hiyo Amri aliweka Nani?na ukiivunja inakuwaje?
Kwa hiyo baba yako akijitolea kufa kwa ajili yako utafurahia hata kama amekuokoa hutohuzunika?😁Kufa kwa Yesu kristo msalabani ni jambo la furaha, shangwe na ushindi katika imani ya Kikristo maana ndio lilizaaa ukombozi, sasa kwanini watu wakae na huzuni, unyonge na kujinyima?
Wakristo kuleni vinono leo.
NdiyoJ
Je ukila ni dhambi?
Asante mkuu kwa ufafanuziJibu: KWANZA kabisa kabla ya kwenda mbali, lazima tujue kuwa, maana yetu ya msingi katika kutokula nyama, ni moja tu; ile ya KUFUNGA STAREHE.
Lazima tujue na kukubali ukweli kuwa, Ijumaa Kuu ni siku ya mateso na kifo cha Bwana Wetu Yesu Kristo.
Sisi tunafahamu kwamba, haya yote yaani mateso hadi kifo cha Yesu msalabani, yamempata kutokana na dhambi zetu hivyo, nasi tunakusudia kuacha starehe zetu na hivyo, tunafunga ili tujutie dhambi zetu.
Hii ni kusema kuwa, tunafunga ili tupate kuzitubia dhambi tulizozifanya na hivyo, katika kufunga Mungu atuonee huruma na atusamehe dhambi zetu na za wenzetu wengine ambao ni wadhambi kama sisi.
Kufunga huku, ni mapambano baina yetu na dhambi pamoja na mkuu wa dhambi yaani shetani.
Kristo anasema katika Injili ya Marko 6:26 kwamba, katika kesi na masuala fulanifulani, shetani hatoki pasipo sala na kufunga.
Basi, tunapaswa kutambua kuwa hayo tunayoyafanya ni juhudi zetu katika kujichomoa toka kwenye ufalme wa dhambi na mfalme wake yaani SHETANI, na kujiweka mikononi mwa Mfalme wa watakatifu yaani, MUNGU MWENYEZI.
Sasa, suali linakuja hivi, KWA NINI SISI WAKRISTO(WAKATOLIKI) tunaacha kula nyama katika siku hiyo ya Ijumaa Kuu? Nadhani kwetu, hili ndilo suala la msingi.
Ndugu msomaji, tutambue kuwa kuwa, katika suala la kufunga, inampasa mtu kuchagua kitu kizuri cha kukiacha. Kwa mfano, huwezi kufunga kitu kama kula ugali wa muhogo wakati ugali wa namna hiyo kwako ni shida, bali unafunga kitu kizuri kama labda kula wali na pilau. Huko ndiko kweli kufunga, kujikatalia na kujitesa kwa toba.
Ieleweke kuwa, tangu enzi zile za kale, huko ilikoanzia dini yetu na huko lilikoanzia zoezi la kufunga, waamini waliacha kula nyama na vitu vitokanavyo kama vile siagi na maziwa kwa vile vilikuwa ni vitu vinavyochukuliwa na kueleweka kuwa ni vya anasa na vile vilivyowakilisha anasa vilipopatikana.
Badala yake, watu katika sehemu na siku hizo, walipotakiwa kufunga, walikula vitu visivyo vya starehe kama vile samaki na mboga za majani.
Hilo, ndilo tulilolipokea kutoka kwa wamisionari kwamba, tunapofunga tuache kuvitumia vitu vya anasa na starehe; nyama ikiwa ikiwa kitu kimojawapo.
Hata hivyo ndugu msomaji, kwa vile vitu vya starehe sio nyama peke yake hapa duniani, sote tunaombwa, kila mmoja akague vitu vyake vya starehe na hivyo, aviache siku ya kufunga.
Ikiwa kwako sigara ni starehe na anasa, basi nia afadhali kuacha siku ile ya kufunga.
Na kama kwako kuogelea ni anasa na starehe, ni afadhali kuacha huko kuogelea siku ile ya kufunga.
Ikiwa ni kuenesha gari, ni afadhali kuacha siku ile ya kufunga. Na ikiwa ni kucheza disko au muziki, basi yafaa kuacha kwa ajili ya kufunga na kadhalika, na kadhalika ili mradi tu, hizo anasa tuziache kando nasi tupate muda wa kuhuzunika na dhambi zetu tukiomba toba kwa Bwana Wetu Yesu Kristo aliyesulibiwa kwa ajili ya dhambi zetu.
Kabla sijamalizia, napenda nikudokeze sababu mojawapo BINAFSI inayowafanya wengine wafunge nyama siku ya IJUMAA KUU.
Hii ni ile sababu ya kufananisha nyama ya kuliwa na mwili au nyama ya Bwana Wetu Yesu Kristo aliyepigwa mijeledi na kutobolewa na kuchubuliwa na kuachwa ikivuja damu nyingi.
Hii ni hali ambayo huwafanya wengine, washindwe kula nyama wakiona maiti ya mtu yeyote.
Nasisitiza kuwa, sababu hii nimeiita SABABU YA KIBINAFSI kwa sababu Kanisa linapowaomba watu wafunge kula nyama siku ya Ijumaa Kuu, lina hoja moja tu, ile ya kuacha starehe na KUFUNGA, siyo hiyo nyingine ya kuona nyama ya kuliwa kama kitu kinachofanana na nyama au mwili wa Bwana Wetu Yesu Kristo.
Basi hii ni sababu ya pili lakini, ni sababu ya waamini binafasi kuona hivyo na ndivyo wanavyosadiki.
Aidha, ndugu msomaji, tukumbuke kwamba, ikiwa kwetu nyama si starehe, au anasa, maaskofu wetu wanao uwezo wa wa kuturuhusu kuila, ikiwa tutaipata siku ya Ijumaa Kuu wakati kama haiwezekani kuitunza hadi kesho yake.
Kesi hii ni ya pekee vinginevyo, kama kwetu nyuma ni starehe pia, kama tunavyoipenda, basi katika siku ya Ijumaa Kuu, tufunge kuila na siku hiyo basi baada ya kuacha sterehe hiyo, tukumbuke dhambi zetu na kutubu toba ya dhati inayotoka ndani.walizoea
Kuna dini zaidi ya 1000 duniani.. siyo lazima uwe mkatoliki.. waachie wanaoaminiUkatoliki una makando kando mengi sana!
Sasa umecheka nini??, Acha kuchekacheka wakati watu tupo serious na Mfungo.D
Duuu!? Yaani unafananisha kutokula nyama kutokana na kuteswa Kwa Yesu na kutokula nyama kutokana na mwizi kukatwakatwa utumbo nje hahahaha ninecheka Kwa kweli
Yesu ni Kristu mwenyewe.Yaani yeye ndiye mwanzilishi wa UkristuHivi Yesu alikuwa dini gani?
Hakuna andiko lolote lile ila imekuwa utamaduni tu,wanaunganisha dots kwamba kumwagika Kwa damu ya Yesu pale msalabani siku kama ya leo ndiyo wakaweka kama kautamaduniNaombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu. Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
Kufufuka kwa Yesu Kristu ndilo jambo la furaha zaidiKufa kwa Yesu kristo msalabani ni jambo la furaha, shangwe na ushindi katika imani ya Kikristo maana ndio lilizaaa ukombozi, sasa kwanini watu wakae na huzuni, unyonge na kujinyima?
Wakristo kuleni vinono leo.
Unashauriwa kuacha kula chochote kinachokupa furaha siku ya Ijumaa kuu na kuacha matendo yoyote ya anasa kwa kuwa ni siku ya huzuniKula nyama siyo alama ya furaha..inategemea a na mazingira...Kuna watu kunywa maziwa ni tendon la furaha...so sikubaliani na wewe