Ijumaa Kuu na katazo la kula nyama

Ijumaa Kuu na katazo la kula nyama

Siku ya huzuni unaanzaje kula vinono?Anateswa,kutwezwa,kutokwa damu na kusulubiwa msalabani hadi kufa.Kula nyama ni kiashiria cha furaha na ufahari.Kwa nini ulie huku unacheka?Halafu ni siku moja tu/masaa machache nini kinakushinda?Kwani kila siku huwa unakula nyama?
Pasaka sio siku ya huzuni. Ni siku ya ushindi, siku ya ukombozi, ni kipindi ambacho kifo, kaburi, na mauti vilishindwa! Hapa ndipo penye nguvu ya u-Kristo. Usisahau, u-Kristo sio dini .

JESUS IS SAVIOR!
 
kwhyo misibani kula wali nyama...haifai? 😀
 
Siku ya huzuni unaanzaje kula vinono?Anateswa,kutwezwa,kutokwa damu na kusulubiwa msalabani hadi kufa.Kula nyama ni kiashiria cha furaha na ufahari.Kwa nini ulie huku unacheka?Halafu ni siku moja tu/masaa machache nini kinakushinda?Kwani kila siku huwa unakula nyama?
Vinono ni nyama tu??
 
Kwa hiyo msibani tunapokula nyama tafsiri yake tunafurahia kifo cha marehemu?
 
Mnafurahia marehemu alivyokufa hamjamlipa fedha zake.Na wengine hufurahi kuwahi kumrithi mjane

Lk 23:28 SUV​

Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

Sasa nani amlilie yesu wakati siku anayoteswa waliokuwa wanamlilia aliwadhihaki kuwa "jililieni nyinyi na familia zenu"
 
TAFSIRI NA UFAFANUZI WA SHERIA YA KANISA KATOLIKI YA KUTOKULA NYAMA SIKU YA IJUMAA KUU

"funga Jumatano ya majibu usile nyama siku ya Ijumaa kuu"

KWANZA kabisa kabla ya kwenda mbali, lazima tujue kuwa, maana yetu ya msingi katika kutokula nyama, ni moja tu; ile ya KUFUNGA STAREHE.

Lazima tujue na kukubali ukweli kuwa, Ijumaa Kuu ni siku ya mateso na kifo cha Bwana Wetu Yesu Kristo.

Sisi tunafahamu kwamba, haya yote yaani mateso hadi kifo cha Yesu msalabani, yamempata kutokana na dhambi zetu hivyo, nasi tunakusudia kuacha starehe zetu na hivyo, tunafunga ili tujutie dhambi zetu.
Hii ni kusema kuwa, tunafunga ili tupate kuzitubia dhambi tulizozifanya na hivyo, katika kufunga Mungu atuonee huruma na atusamehe dhambi zetu na za wenzetu wengine ambao ni wadhambi kama sisi.

Kufunga huku, ni mapambano baina yetu na dhambi pamoja na mkuu wa dhambi yaani shetani.

Kristo anasema katika Injili ya Marko 6:26 kwamba, katika kesi na masuala fulanifulani, shetani hatoki pasipo sala na kufunga.
Basi, tunapaswa kutambua kuwa hayo tunayoyafanya ni juhudi zetu katika kujichomoa toka kwenye ufalme wa dhambi na mfalme wake yaani SHETANI, na kujiweka mikononi mwa Mfalme wa watakatifu yaani, MUNGU MWENYEZI.

Sasa, suali linakuja hivi, KWA NINI SISI WAKRISTO(WAKATOLIKI) tunaacha kula nyama katika siku hiyo ya Ijumaa Kuu? Nadhani kwetu, hili ndilo suala la msingi.

Ndugu msomaji, tutambue kuwa kuwa, katika suala la kufunga, inampasa mtu kuchagua kitu kizuri cha kukiacha. Kwa mfano, huwezi kufunga kitu kama kula ugali wa muhogo wakati ugali wa namna hiyo kwako ni shida, bali unafunga kitu kizuri kama labda kula wali na pilau. Huko ndiko kweli kufunga, kujikatalia na kujitesa kwa toba.

Ieleweke kuwa, tangu enzi zile za kale, huko ilikoanzia dini yetu na huko lilikoanzia zoezi la kufunga, waamini waliacha kula nyama na vitu vitokanavyo kama vile siagi na maziwa kwa vile vilikuwa ni vitu vinavyochukuliwa na kueleweka kuwa ni vya anasa na vile vilivyowakilisha anasa vilipopatikana.

Badala yake, watu katika sehemu na siku hizo, walipotakiwa kufunga, walikula vitu visivyo vya starehe kama vile samaki na mboga za majani.
Hilo, ndilo tulilolipokea kutoka kwa wamisionari kwamba, tunapofunga tuache kuvitumia vitu vya anasa na starehe; nyama ikiwa ikiwa kitu kimojawapo.

Hata hivyo ndugu msomaji, kwa vile vitu vya starehe sio nyama peke yake hapa duniani, sote tunaombwa, kila mmoja akague vitu vyake vya starehe na hivyo, aviache siku ya kufunga.

Ikiwa kwako sigara ni starehe na anasa, basi nia afadhali kuacha siku ile ya kufunga.
Na kama kwako kuogelea ni anasa na starehe, ni afadhali kuacha huko kuogelea siku ile ya kufunga.

Ikiwa ni kuenesha gari, ni afadhali kuacha siku ile ya kufunga. Na ikiwa ni kucheza disko au muziki, basi yafaa kuacha kwa ajili ya kufunga na kadhalika, na kadhalika ili mradi tu, hizo anasa tuziache kando nasi tupate muda wa kuhuzunika na dhambi zetu tukiomba toba kwa Bwana Wetu Yesu Kristo aliyesulibiwa kwa ajili ya dhambi zetu.

Kabla sijamalizia, napenda nikudokeze sababu mojawapo BINAFSI inayowafanya wengine wafunge nyama siku ya IJUMAA KUU.
Hii ni ile sababu ya kufananisha nyama ya kuliwa na mwili au nyama ya Bwana Wetu Yesu Kristo aliyepigwa mijeledi na kutobolewa na kuchubuliwa na kuachwa ikivuja damu nyingi.
Hii ni hali ambayo huwafanya wengine, washindwe kula nyama wakiona maiti ya mtu yeyote.

Nasisitiza kuwa, sababu hii nimeiita SABABU YA KIBINAFSI kwa sababu Kanisa linapowaomba watu wafunge kula nyama siku ya Ijumaa Kuu, lina hoja moja tu, ile ya kuacha starehe na KUFUNGA, siyo hiyo nyingine ya kuona nyama ya kuliwa kama kitu kinachofanana na nyama au mwili wa Bwana Wetu Yesu Kristo.
Basi hii ni sababu ya pili lakini, ni sababu ya waamini binafasi kuona hivyo na ndivyo wanavyosadiki.

Aidha, ndugu msomaji, tukumbuke kwamba, ikiwa kwetu nyama si starehe, au anasa, maaskofu wetu wanao uwezo wa wa kuturuhusu kuila, ikiwa tutaipata siku ya Ijumaa Kuu wakati kama haiwezekani kuitunza hadi kesho yake.

Kesi hii ni ya pekee vinginevyo, kama kwetu nyuma ni starehe pia, kama tunavyoipenda, basi katika siku ya Ijumaa Kuu, tufunge kuila na siku hiyo basi baada ya kuacha sterehe hiyo, tukumbuke dhambi zetu na kutubu toba ya dhati inayotoka ndani.
 
Lk 23:28 SUV​

Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

Sasa nani amlilie yesu wakati siku anayoteswa waliokuwa wanamlilia aliwadhihaki kuwa "jililieni nyinyi na familia zenu"
Acha kusoma Bible kikasuku utakwama.
 
Pasaka sio siku ya huzuni. Ni siku ya ushindi, siku ya ukombozi, ni kipindi ambacho kifo, kaburi, na mauti vilishindwa! Hapa ndipo penye nguvu ya u-Kristo. Usisahau, u-Kristo sio dini .

JESUS IS SAVIOR!
Ndiyo kijijini kwenu walivyokuhadithia?
 
Siku ya huzuni unaanzaje kula vinono?Anateswa,kutwezwa,kutokwa damu na kusulubiwa msalabani hadi kufa.Kula nyama ni kiashiria cha furaha na ufahari.Kwa nini ulie huku unacheka?Halafu ni siku moja tu/masaa machache nini kinakushinda?Kwani kila siku huwa unakula nyama?
Unachekesha sana we mtu. Unamaanisha kama unamsiba usile chakula kuzuri. Kuna watu leo hata mida hii wanakunywa mipombe lakini eti nyama hawali
 
Iyo ni amri ya kanisa Mkuu, na Biblia inasema lililofungwa/funguliwa duniani na mbinguni limefungwa/funguliwa (sikumbuki kifungu).

Na hiyo hiyo inasema tiini mamlaka iliyowekwa (sikumbuki kifungu) ikamalizia kwa kusema, wewe ni mwamba na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa (sikumbuki kifungu).

Sasa ni kuwa kanisa liliasisiwa na Yesu kupitia Petro, hilo kanisa likajitengenezea amri zake 6, tukasisitiziwa liliofunguliwa duniani na mbinguni limefunguliwa.

Tukaona isiwe shida sana, bado tukaambiwa tuzitii mamlaka na moja ya amri za moja ya mamlaka tulizoambiwa tuzitii ni kutokula nyama ijumaa kuu. Sasa sisi tufanyeje mleta uzi?
 
Unashauriwa kuacha kula chochote kinachokupa furaha siku ya Ijumaa kuu na kuacha matendo yoyote ya anasa kwa kuwa ni siku ya huzuni

Siyo kuacha kula nyama pekee bali jambo lolote la furaha au anasa
Anasa hazipaswi kufanyiwa Ijumaa juu pekee
 
Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu.Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
Inaweza ikawa ni MAPOKEO kama ilivyo BIDAA kwa waislamu
 
Back
Top Bottom