Ijumaa ya leo ikukumbushe tu Sabato ni Jumamosi

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Yesu alifufuka Siku ya kwanza ya Juma.
Leo Ijumaa ndicho kile kinachoitwa Siku Maandalio ya Juma au Siku ya sita.

Jumapili ni Siku ya kwanza ya Juma. Na Sabato kesho ni Jumamosi.

Mambo ya kutafakari.

1: Ni dharau na ukosefu wa adabu kwa Mungu mfalme kuiita Jumapili au ijumaa Sabato. Ni kuhariri sentensi za Mungu.

2: Inatukumbusha Dunia iliumbwa Siku sita za wiki. Hii ya Saba ya Sabato ilikuwa in ofa kwa mwanadamu. Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu. Isingekuwa Sabato wiki ingebaki na Siku sita tu.

3: SABATO imetajwa Mara ya kwanza katika maandiko kabla ya dhambi. Hivyo wazo LA Sabato Galina uhusiano na vivuli vya maagizo ya jangwani.

4: Yesu sio Sabato, wala Sabato sio Yesu. Yesu ni mmiliki au Bwana wa hiyo Sabato. Sabato sio Siku ya wayahudi ni ya Yesu na wanaomfuata.

5: Kukusanyika kwa ibada baada ya Siku sita za kazi kwa Siku isiyo Sabato ya Jumamosi ni kumkosoa na kumdharau Mungu na maagizo yake.

6: Sabato sio kwa ajili ya wakristo. Ni mwanadamu wote. Kama ni mwanadamu na ulikuwa hujui hujachelewa. Nakukumbusha. Ikumbuke Siku ya Sabato.

7: Mungu hakuumba weekend. Alitutengenezea Siku sita za kazi na ya saba ya sabato sio Siku mbili zinazoitwa weekend. Hii taarifa ni muhimu kwako.

Niwatakie ijumaa njema.

Maelekezo ya Mungu hayataki mjadala mrefu yanataka utekelezaji. Huwezi kuhoji kauli za mfalme asiyekosea.
 
Mk 2:27-28 SUV

Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.
Hii imekamilika kabisa.
Mwana wa adamu sio Sabato Bali Bwana wa hivyo Sabato.

Ni mapokeo ya wanadamu kusema ukiwa na Yesu umekuwa na sabato na umepumzika.

Siku ya Leo ni ya kupeana taarifa za msingi za kiroho.
 
AHSANTE SANA MTUMISHI ATAKAYEKUPINGA NI LING'OMBE TU (in Tundu Lissu Voice).

QURAN : AL - BAQARA.

65. Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato, (siku ya mapumziko, Jumaa Mosi) na tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu.

66. Kwa hivyo tukayafanya hayo kuwa onyo kwa wale walio kuwa katika zama zao na walio kuja baada yao, na mawaidha kwa wachamngu.
 
Yesu alikufa Siku ya kwanza ya Juma.
Leo Ijumaa ndicho kile kinachoitwa Siku ya kwanza ya Juma.

Jumapili ni Siku ya kwanza ya Juma. Na Sabato kesho ni Jumamosi.

Mambo ya kutafakari.

1: Ni dharau na ukosefu wa adabu kwa Mungu mfalme kuiita Jumapili au ijumaa Sabato. Ni kuhariri sentensi za Mungu.

2: Inatukumbusha Dunia iliumbwa Siku sita za wiki. Hii ya Saba ya Sabato ilikuwa in ofa kwa mwanadamu. Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu. Isingekuwa Sabato wiki ingebaki na Siku sita tu.

3: SABATO imetajwa Mara ya kwanza katika maandiko kabla ya dhambi. Hivyo wazo LA Sabato Galina uhusiano na vivuli vya maagizo ya jangwani.

4: Yesu sio Sabato, wala Sabato sio Yesu. Yesu ni mmiliki au Bwana wa hiyo Sabato. Sabato sio Siku ya wayahudi ni ya Yesu na wanaomfuata.

5: Kukusanyika kwa ibada baada ya Siku sita za kazi kwa Siku isiyo Sabato ya Jumamosi ni kumkosoa na kumdharau Mungu na maagizo yake.

6: Sabato sio kwa ajili ya wakristo. Ni mwanadamu wote. Kama ni mwanadamu na ulikuwa hujui hujachelewa. Nakukumbusha. Ikumbuke Siku ya Sabato.

7: Mungu hakuumba weekend. Alitutengenezea Siku sita za kazi na ya saba ya sabato sio Siku mbili zinazoitwa weekend. Hii taarifa ni muhimu kwako.

Niwatakie ijumaa njema.

Maelekezo ya Mungu hayataki mjadala mrefu yanataka utekelezaji. Huwezi kuhoji kauli za mfalme asiyekosea.
Mkuu Danny Faure hupo? Ni kitambo sana Jamvini. Kuna wakati niliuliza h7mu umepotea wapi? Good to read from you.
 
Back
Top Bottom