Ijumaa ya leo ikukumbushe tu Sabato ni Jumamosi

Ijumaa ya leo ikukumbushe tu Sabato ni Jumamosi

YAANI UKIONA MKIRSTO ANAPINGA JUU YA SABATO JUA KABISA AKILI YAKE HAIKO SAWA,HAIWEZEKANI MTUME MUHAMMAD ASIYE MKRISTO AJUE MAANDIKO KUWAZIDI WAKRISTO WENYEWE KUHUSU SABATO,HAKUWA NA BIBLIA WALA KATEKISIMU.

KUNA WAKATI NAAMINI KABISA UISLAM NA MTUME MUHAMMAD WANA HOJA ZA MSINGI JUU YETU WAKRISTO NA IMANI YETU - AKILI YETU SIO NZURI KABISA.

QURAN - AN - NISAAI 4 : 47

"Enyi mlio pewa Kitabu! (mayahudi na wakristo)Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tulivyo walaani watu waliovunja Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu (Sabato) ni lazima ifanyike."
 
Yesu alikufa Siku ya kwanza ya Juma.
Leo Ijumaa ndicho kile kinachoitwa Siku Maandalio ya Juma au Siku ya sita.

Jumapili ni Siku ya kwanza ya Juma. Na Sabato kesho ni Jumamosi.

Mambo ya kutafakari.

1: Ni dharau na ukosefu wa adabu kwa Mungu mfalme kuiita Jumapili au ijumaa Sabato. Ni kuhariri sentensi za Mungu.

2: Inatukumbusha Dunia iliumbwa Siku sita za wiki. Hii ya Saba ya Sabato ilikuwa in ofa kwa mwanadamu. Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu. Isingekuwa Sabato wiki ingebaki na Siku sita tu.

3: SABATO imetajwa Mara ya kwanza katika maandiko kabla ya dhambi. Hivyo wazo LA Sabato Galina uhusiano na vivuli vya maagizo ya jangwani.

4: Yesu sio Sabato, wala Sabato sio Yesu. Yesu ni mmiliki au Bwana wa hiyo Sabato. Sabato sio Siku ya wayahudi ni ya Yesu na wanaomfuata.

5: Kukusanyika kwa ibada baada ya Siku sita za kazi kwa Siku isiyo Sabato ya Jumamosi ni kumkosoa na kumdharau Mungu na maagizo yake.

6: Sabato sio kwa ajili ya wakristo. Ni mwanadamu wote. Kama ni mwanadamu na ulikuwa hujui hujachelewa. Nakukumbusha. Ikumbuke Siku ya Sabato.

7: Mungu hakuumba weekend. Alitutengenezea Siku sita za kazi na ya saba ya sabato sio Siku mbili zinazoitwa weekend. Hii taarifa ni muhimu kwako.

Niwatakie ijumaa njema.

Maelekezo ya Mungu hayataki mjadala mrefu yanataka utekelezaji. Huwezi kuhoji kauli za mfalme asiyekosea.
Sawa msabato, sisi tunamfuata Bwana wa sabato wewe fuata siku ya Jumamosi.
Simple tuu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo mi myahudi mkuu
Kila mkristo ni myahudi na mzao wa Ibrahim kwa imani ya Yesu.

Galatians 3:29
[29]And if ye be Christ's, then are ye Abraham's seed, and heirs according to the promise.
Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Wale watu was Jangwani ni Baba zetu was imani kama Paulo alivyowaandikia wazungu wa Corintho kuwa wale ni Baba zao wakati wao sio wayahudi.

Taarifa ni power.
 
Sawa msabato, sisi tunamfuata Bwana wa sabato wewe fuata siku ya Jumamosi.
Simple tuu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Mimi sio Msabato. Mimi ni mtoto was Mfalme. Raia was ufalme wa mbinguni ninayeishi hapa duniani kwa Muda tu.

Sasa mtoto wa Mfalme ni shangwe na raha kufuata agizo LA mfalme wangu Bwana wa Sabato aliyeifanya Siku hiyo kwa ajili yangu.

Asiyeikumbuka Sabato anamdharau Yesu.

Maana anasema hana maana ya Yesu kutengeneza Siku Saba kwa kuonheza moja ya Sabato.

Dini yoyote inayodharau na kupinga imeasi taratibu za ufalme wa Mungu.

Kupinga sabato ni mapokeo.
 
UNAKUTANA NA MTU KAKOMAA KABISA OH JUMAPILI NDIYO SAHIHI, SABATO NI KWA AJILI YA WAYAHUDI.

HEBU TUWAZE.

KITABU CHA MATENDO YA MITUME KIMEANDIKWA MIAKA ZAIDI YA ISHIRINI (20) BAADA YA UFUFUKO NA KUPAA KWA YESU.KATIKA KIPINDI CHOTE HIKI WAKRISTO WA AWALI ( KANISA LA MITUME LILIENDELEA KUISHIKA SABATO (JUMAAMOSI).

●HIVI HUYO YESU ALIKUWA HAWAONI? ALIKUWA HAONGEI NAO HAO MITUME?

●KWANINI ASIWAZUIE ILI WAABUDU KATIKA SIKU YA UFUFUKO WAKE (JUMAPILI)?.

MATENDO YA MITUME 16 : 12 - 13.

12Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.

13Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo.
 
Sawa msabato, sisi tunamfuata Bwana wa sabato wewe fuata siku ya Jumamosi.
Simple tuu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
AMRI YA NNE.

IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE,SIKU SITA FANYA KAZI,UTENDE MAMBO YAKO YOTE,LAKINI SIKU YA SABA NI SABATO YA BWANA MUNGU WAKO.

Yohana 14:15,21 (YESU)

[15]Mkinipenda, mtazishika amri zangu.

[21]Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

1 Yohana 2:3-4 (MITUME)

[3]Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

[4]Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.

1 Yohana 5:2-3
[2]Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.

[3]Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
 
Tunasali jumapili kusheherekea ufufuko wa bwana wetu Yesu Kristo
Mwafanya vyema.
Ila Leo nilikiwa nakumbusha tu hayo ni maamuzi ya watu kama Mimi na wewe.

Ukiona vyema chagua kufuata hili LA Mungu hayo ya watu ukaacha.

Itakulipa sana.

Kufa na kufufuka kwaYesu mfuasi wa Yesu anasherekea kila Siku sio tukio kama LA kifo cha Mwanadamu maarufu.
 
Hatujakataa tunajua vizuri jumapili ni siku ya kwanza ya juma msifikiri hatujui.
 
Tunasali jumapili kusheherekea ufufuko wa bwana wetu Yesu Kristo
>Kwa hiyo WEWE ni mwerevu zaidi ya MITUME si ndiyo?.

Kwamba PAULO NA MITUME wengine hawakujua kuwa YESU kafufuka wakaendelea na ibada ya kila SABATO?

Hiyo ruhusa ya kusali JUMAPILI kwenye maandiko matakatifu inapatikana wapi ili na mimi nianze kusali?

HEBU ONA HAPA MITUME WANAVYOELEZA NINI WALIENDELEA KUFANYA MIAKE 25 BAADA YA YESU KUFUFUKA.

MATENDO YA MITUME 16 : 12,13.

12 Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.

13 Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali.
 
Yesu alikufa Siku ya kwanza ya Juma.
Leo Ijumaa ndicho kile kinachoitwa Siku Maandalio ya Juma au Siku ya sita.

Jumapili ni Siku ya kwanza ya Juma. Na Sabato kesho ni Jumamosi.

Mambo ya kutafakari.

1: Ni dharau na ukosefu wa adabu kwa Mungu mfalme kuiita Jumapili au ijumaa Sabato. Ni kuhariri sentensi za Mungu.

2: Inatukumbusha Dunia iliumbwa Siku sita za wiki. Hii ya Saba ya Sabato ilikuwa in ofa kwa mwanadamu. Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu. Isingekuwa Sabato wiki ingebaki na Siku sita tu.

3: SABATO imetajwa Mara ya kwanza katika maandiko kabla ya dhambi. Hivyo wazo LA Sabato Galina uhusiano na vivuli vya maagizo ya jangwani.

4: Yesu sio Sabato, wala Sabato sio Yesu. Yesu ni mmiliki au Bwana wa hiyo Sabato. Sabato sio Siku ya wayahudi ni ya Yesu na wanaomfuata.

5: Kukusanyika kwa ibada baada ya Siku sita za kazi kwa Siku isiyo Sabato ya Jumamosi ni kumkosoa na kumdharau Mungu na maagizo yake.

6: Sabato sio kwa ajili ya wakristo. Ni mwanadamu wote. Kama ni mwanadamu na ulikuwa hujui hujachelewa. Nakukumbusha. Ikumbuke Siku ya Sabato.

7: Mungu hakuumba weekend. Alitutengenezea Siku sita za kazi na ya saba ya sabato sio Siku mbili zinazoitwa weekend. Hii taarifa ni muhimu kwako.

Niwatakie ijumaa njema.

Maelekezo ya Mungu hayataki mjadala mrefu yanataka utekelezaji. Huwezi kuhoji kauli za mfalme asiyekosea.
Ndugu Mitale, wakristo walio wengi wanaabudu Siku ya Kwanza a.k.a Jumapili kwa sababu hizi (baadhi).
  1. Yesu Kristo alifufuka Siku ya Kwanza ya Juma (Mt.28:1). Ufufuko wa Yesu ndio wokovu wenyewe; labda kama huamini katika wokovu.
  2. Wakristo wa Mwanzo walikutana Siku ya Kwanza kwa ajili ya kuumega mkate; "Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.” (Mdo.20:7). Labda kama huamini andiko hilo au kama wewe sio mkristo au hujui maana ya kuumega mkate.
  3. Wakristo wa Mwano walipumzika Siku ya Kwanza; "Siku ya Kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake: ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja.” (1Kor.16:2); labda kama huamini hilo andiko au wewe sio mkristo unaweza kupinga.
  4. Kanisa liliundwa rasmi Siku ya Kwanza almaarufu kama Pentekoste; Mdo 2:1-6; "Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi."; pengine ungetamani andiko hili lisiwepo ila ndio hivyo tena.
Sitaki kuamini kwamba Bi. Ellen ana ufahamu wa siri za Mbinguni kumzidi Roho Mtakatifu au watakatifu wa mwanzo akina Petro, Paulo, na mitume wengine walioishi na kula pamoja na BWANA akiwaahidi kumtuma Roho Mtakatifu kukamilisha kazi yake. Iko hivi, amini chochote upendacho ila usikashifu au kudharau waaminicho wengine. Huo ndio uungwana.
 
SASA WEWE NA WANAFUNZI WA YESU MWENYE AKILI NANI? WAO JUMAMOSI WANALIKUWA WANAPUMZIKA.

JUMAPILI SHAMBANI KUPIGA JEMBE,TENA SIKU YA UFUFUO KABISAA.
ENDELEENI KUINGIZANA CHAKA.

MARKO 16 :12

9Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo wabaya saba. 10Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia. 11Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona, hawakuamini.

Yesu anawatokea wanafunzi wawili

(Luka 24:13-35)

12Baadaye Yesu aliwatokea wanafunzi wawili akiwa na sura nyingine. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda shambani.
Sasa mzee hapo si walikuwa hawajui km Yesu atafufuka!!!,Lkn baada ya kujua kuwa Yesu alifufuka siku ya Jumapili,Mitume walianza kukutanika kwaajili ya Ibada siku ya Jumapili km ilivyo Leo rejea 1Kor.16:1-2.
 
Kwa Mujibu was maandiko.
Jumapili ni Siku ya wanafunzi was Yesu kwenda shambani sio kanisani.

Luka 24:13-
...Walikuwa wanakwenda shambani.

Mapokeo yananguvu ingawa yatashindwa na ukweli.
Wewe Hujui tu, Hapo walikuwa hawajui km atafufuka.Hata hivyo kwenda shambani sio hoja kwasababu Biblia haijasema km walikuwa wanaenda shambani kufanya nini? km walikwenda kutembea tu je??.
 
QURAN AL - MUQADASWI.
Screenshot_20220415-124802_Gallery.jpg
 
Back
Top Bottom