Ikikupendeza Rais Samia, tunaomba SGR Dar es Salaam - Arusha

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
221
Reaction score
542
Miji ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha ni kanda muhimu sana kiuchumi na kwa pamoja inachangia kiasi kikubwa cha pato la taifa kutokana na kilimo, biashara hasa ya madini, na utalii. Ukizingatia Mlima Kilimanjaro, Oldonyo Lengai, Mlima Meru, Mbuga ya Wanyama Pori ya Saadani, Mbuga ya Wanyama Pori ya Arusha, Tarangire, Manyara, Ngorongoro Crater, na Serengeti National Park, vyote vinapatikana katika kanda hii. Kwa bahati nzuri, vivutio hivi vimekuwa vituo pendwa sana hasa kwa watalii duniani kote na vimeweza kujichukulia tuzo za kimataifa kwa ubora wake.

Arusha na Moshi zimekuwa na hoteli na nyumba nzuri zinazoweza kulaza wageni kwa usiku mmoja, hali inayoongeza idadi ya wageni wengi sana. Hoteli hizo zinatoa ajira kwa vijana, na kampuni za utalii pia huajiri vijana wetu kuwasindikiza wageni hifadhini. Arusha inahost kumbi za mikutano ya kimataifa pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyohudhuriwa na marais na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali, ambao walilala Arusha. Kwa ratiba za kila mwaka, mikutano hiyo hufanyika mara kwa mara, kuonyesha umuhimu wa ukanda huu kiuchumi.

Cha kushangaza, pamoja na umuhimu huu, bado usafiri hasa wa treni kutoka Dar es Salaam haujapewa kipaumbele kinachostahili. Kuna haja ya kuanzisha treni ya kisasa ya umeme (SGR) inayoweza kutumia saa 4 kwa kiwango cha juu kutoka Dar es Salaam hadi Arusha. Mfanyabiashara au mtalii kutoka Rwanda, Burundi, Congo, Msumbiji, Kenya na maeneo mengine aweze kusafiri asubuhi na kufika Dar saa 3 mchana, kufanya shughuli zake, kisha kurudi Arusha jioni. Urahisi wa kufika kanda hii ni nyenzo muhimu ya kuwavutia watalii.

Kupitia andiko hili, nakuomba Mama Rais Samia uuwezeshe mradi huu wa kihistoria na kiubunifu. Uwepo wa SGR utakuachia heshima kubwa kama urithi wa uongozi wako. Tunaamini wachumi, wataalamu, na viongozi wengine watakusaidia kutimiza ndoto hii. Tunakushukuru kwa uwanja wa kisasa wa AFCON Arusha na kwa kutuletea kijana mwenzetu Makonda, ambaye ni mchapa kazi. Mungu akulinde na kukuongoza katika juhudi zako za kuimarisha maendeleo ya taifa letu. Tanesco msimuangushe mama katika hili!
 
Wamiliki wa mabasi watakosa biashara, ngoja waje
Wata compete au wa evolve. Wajikusanye wawe shareholders wa iyo train under one or 2 company, waweke mabehewa mazuri, vichwa vya kisasa, wa manage kila kitu wao, wakusanye mapato, walipe Kodi ya serikali, wagawsne faida yao kila mwaka, serikali ihakikishe umeme wa kutosha. Na bado kihualisia train aitaondoa umuhimu wa mabasi kwa 100% so it is all about development
 
SGR ije kua hivi:

Screenshot_20241226-155356~2.png
 
Sgr ikifika kigoma na mwanza ...inatakiwa phase inayofata ni sgr ya Arusha ,tanga , Moshi...na ikibidi ya mtwara na lindi..halafu tazara nayo igeuke sgr...nchi ipige hatua
Hamtaki tena maendeleo ya watu?

Si kuna wakati mlikataa maendeleo ya vitu!
 
Miji ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha ni kanda muhimu sana kiuchumi na kwa pamoja inachangia kiasi kikubwa cha pato la taifa kutokana na kilimo, biashara hasa ya madini, na utalii. Ukizingatia Mlima Kilimanjaro, Oldonyo Lengai, Mlima Meru, Mbuga ya Wanyama Pori ya Saadani, Mbuga ya Wanyama Pori ya Arusha, Tarangire, Manyara, Ngorongoro Crater, na Serengeti National Park, vyote vinapatikana katika kanda hii. Kwa bahati nzuri, vivutio hivi vimekuwa vituo pendwa sana hasa kwa watalii duniani kote na vimeweza kujichukulia tuzo za kimataifa kwa ubora wake.

Arusha na Moshi zimekuwa na hoteli na nyumba nzuri zinazoweza kulaza wageni kwa usiku mmoja, hali inayoongeza idadi ya wageni wengi sana. Hoteli hizo zinatoa ajira kwa vijana, na kampuni za utalii pia huajiri vijana wetu kuwasindikiza wageni hifadhini. Arusha inahost kumbi za mikutano ya kimataifa pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyohudhuriwa na marais na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali, ambao walilala Arusha. Kwa ratiba za kila mwaka, mikutano hiyo hufanyika mara kwa mara, kuonyesha umuhimu wa ukanda huu kiuchumi.

Cha kushangaza, pamoja na umuhimu huu, bado usafiri hasa wa treni kutoka Dar es Salaam haujapewa kipaumbele kinachostahili. Kuna haja ya kuanzisha treni ya kisasa ya umeme (SGR) inayoweza kutumia saa 4 kwa kiwango cha juu kutoka Dar es Salaam hadi Arusha. Mfanyabiashara au mtalii kutoka Rwanda, Burundi, Congo, Msumbiji, Kenya na maeneo mengine aweze kusafiri asubuhi na kufika Dar saa 3 mchana, kufanya shughuli zake, kisha kurudi Arusha jioni. Urahisi wa kufika kanda hii ni nyenzo muhimu ya kuwavutia watalii.

Kupitia andiko hili, nakuomba Mama Rais Samia uuwezeshe mradi huu wa kihistoria na kiubunifu. Uwepo wa SGR utakuachia heshima kubwa kama urithi wa uongozi wako. Tunaamini wachumi, wataalamu, na viongozi wengine watakusaidia kutimiza ndoto hii. Tunakushukuru kwa uwanja wa kisasa wa AFCON Arusha na kwa kutuletea kijana mwenzetu Makonda, ambaye ni mchapa kazi. Mungu akulinde na kukuongoza katika juhudi zako za kuimarisha maendeleo ya taifa letu. Tanesco msimuangushe mama katika hili!
Isipompendeza je? Watanzania Bado wajinga wengi. Unalipa Kodi unamwandikia individual politician et "ikikupendeza" kwa hiyo siku hizi nchi inajengwa kwa mtu ikimpendeza? Kwanini usiiambie serikali ijenge SGR na si huyo uliyemtaja. Uhalali wa serikali ni wananchi
 
Miji ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha ni kanda muhimu sana kiuchumi na kwa pamoja inachangia kiasi kikubwa cha pato la taifa kutokana na kilimo, biashara hasa ya madini, na utalii. Ukizingatia Mlima Kilimanjaro, Oldonyo Lengai, Mlima Meru, Mbuga ya Wanyama Pori ya Saadani, Mbuga ya Wanyama Pori ya Arusha, Tarangire, Manyara, Ngorongoro Crater, na Serengeti National Park, vyote vinapatikana katika kanda hii. Kwa bahati nzuri, vivutio hivi vimekuwa vituo pendwa sana hasa kwa watalii duniani kote na vimeweza kujichukulia tuzo za kimataifa kwa ubora wake.

Arusha na Moshi zimekuwa na hoteli na nyumba nzuri zinazoweza kulaza wageni kwa usiku mmoja, hali inayoongeza idadi ya wageni wengi sana. Hoteli hizo zinatoa ajira kwa vijana, na kampuni za utalii pia huajiri vijana wetu kuwasindikiza wageni hifadhini. Arusha inahost kumbi za mikutano ya kimataifa pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyohudhuriwa na marais na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali, ambao walilala Arusha. Kwa ratiba za kila mwaka, mikutano hiyo hufanyika mara kwa mara, kuonyesha umuhimu wa ukanda huu kiuchumi.

Cha kushangaza, pamoja na umuhimu huu, bado usafiri hasa wa treni kutoka Dar es Salaam haujapewa kipaumbele kinachostahili. Kuna haja ya kuanzisha treni ya kisasa ya umeme (SGR) inayoweza kutumia saa 4 kwa kiwango cha juu kutoka Dar es Salaam hadi Arusha. Mfanyabiashara au mtalii kutoka Rwanda, Burundi, Congo, Msumbiji, Kenya na maeneo mengine aweze kusafiri asubuhi na kufika Dar saa 3 mchana, kufanya shughuli zake, kisha kurudi Arusha jioni. Urahisi wa kufika kanda hii ni nyenzo muhimu ya kuwavutia watalii.

Kupitia andiko hili, nakuomba Mama Rais Samia uuwezeshe mradi huu wa kihistoria na kiubunifu. Uwepo wa SGR utakuachia heshima kubwa kama urithi wa uongozi wako. Tunaamini wachumi, wataalamu, na viongozi wengine watakusaidia kutimiza ndoto hii. Tunakushukuru kwa uwanja wa kisasa wa AFCON Arusha na kwa kutuletea kijana mwenzetu Makonda, ambaye ni mchapa kazi. Mungu akulinde na kukuongoza katika juhudi zako za kuimarisha maendeleo ya taifa letu. Tanesco msimuangushe mama katika hili!
Ok
 
Tatizo huko mizigo hakuna.Tanga ,Arusha na Kilimanjaro mizigo Yao kuu ni mbege.Sasa Sgr wabebe mbege?
 
Bandari ya Tanga can serve mizigo ya kilimanjaro, Arusha, Manyara provably na Some part of Singida etc....mbege ni sehemu ndogo ya mizigo bro...grow up uache ujinga!
 
Back
Top Bottom