Ikitokea dada yangu na kaka yangu wamesalitiwa na wenza wao nitamuonea huruma zaidi kaka yangu kuliko dada

Ni kama haupo proud na gender yako shida ni nini dear?
Iam very proud and blessed to be a woman.

Nikuulize hivi.
Boyfriend wako akikupenda kiasi cha kukununulia zawadi ya gari ila akachepuka ofcoz utaumia ila wewe ukimchit huyo biyfriend wako yeye ataumia zaidi coz yeye kajitoa zaidi yako.

Sasa mimi kusema hivi ndo sipendi jinsia yangu.?

Laiti ungejua ninavyoshukuru kuumbwa mwanamke.Naangalia sacrifice anazofanya mume wangu kwa ajili yangu najiuliza mim ningeweza.Na anafanya hivi simply sababu mimi ni mwanamke na anaamini niko fragile sitakiwi kupata mastress na misukosuko so anabeba mizigo yangu mingi akiamini yeye ana nguvu za ku handle shuruba zaidi yangu.
 
Kila mtu afanye kinachompendeza, ukiona pesa kwako ndio maisha Sawa, mapenzi Sawa, Ndoa na familia Sawa, kila mtu awe huru
 
😃😃
Nashangaza kwa sababu mtizamo wangu ni old school.
Nawaza kama walivyokua wakiwaza bibi zetu waleee wa enzi zile tunaowasifia kuwa ndoa zao zikidumu.
Wale ambao hawakuhudhuria kitchen party gala wala wa kabla ya Beijing.
Sawa mama upo sahihi
Kuchagua njia yako ni nzuri sana hata ikitushanganza wengine kwako linabaki kua chagua bora
 
Sawa mama 😊
 
Naunga mkono hoja kicwa na miguu
 
Bt men are way better off than women when it comes to the underlying issue of " infidelity"

Mwanaume aweza akawa anamcheat mkewe ila ndoa yake bado ikawa imara especially kwa mwanaume husika anataka responsibilities zake ipasavyo.

Mimi nakazia idea za mleta mada
 
Uzuri leo hujatumia kiingereza chako kile😃.

My love,simkandamizi mwanamke wala simshushi mwanamke na kumuinua mwanaume ila ukweli ni kwamba tayari mwanaume yuko juu hata nisiposema tayari mwanaume yupo juu.

Yupo juu kwa sababu,wote tunajua wanaume ndio wanahudumia wanawake.Ni dunia nzima ila Afrika ni zaidi.

Mwanaume anaanza kuwa juu yako kwa kukulipia mahari(kama kakununua fulani hivi uwe property yake) then anatafuta makazi anakua kama anakufuga kwa kukulisha na kukupa huduma zote mpaka siku utakayozeeka ubakie na jino moja la mbele.Mpaka hapo nani yuko juu?

Na wanawake wote tunajua kuwa mwanaume ndo anatakiwa awe juu ndo mana mashoga zetu wanaohudumia wanaume tunawacheka na kuwakalia vikao vya umbea .Utasikia mwenzangu nasikia ile ingejimenti ringi kanunua bibie..Heheee,usinambie halooo.😃.Kwanini tuone ajabu?

Siku zote mwanaume ndo mtoaji ndo mana hakuna makahaba wa kiume wanaojiuza barabarani sababu wasingepata wateja ambao ni wanawake sababu wanawake hatujazoea kutoa hela zetu kwa wanaume.Ila makahaba wa kike hadi wanajenga na kusomesha kwa hela za wanaume.

Binafsi naona niko sahihi kuwa ukimsaliti mtu anayekupambania ataumia zaidi ya wewe ukisalitiwa na anayekuhudumia.

Hapa nimeongelea maumivu,
Sisapoti usaliti na ninqjua kuna magonjwa ila incase usaliti umetokea huu ndo mtazamo wangu.
 
Ni ngumu sana kuona madhara ya usaliti kama hauvai viatu vya mwingine. You are a man, nategemea wengi wenu mfurahishwe na bandiko la prida, and so far anajua kuwafurahisha. (Hii ni falsafa yake ya siku zote)

Tuje kwenye uhalisia, mnapima stability ya ndoa kwa vigezo gani? Mnapima kudumu kwa ndoa bila kuangalia afya ya ndoa?

You have 0 idea ni kiasi gani wanawake wanajitibu magonjwa ya ngono kimya kimya na yanajirudia (recurring)

Hamjui ni kwa namna gani usaliti unaharibu someone’s mental state. Hata sina haja ya kueleza hili.

Kaka kama wewe ni msaliti, jua mwanamke wako atakusaliti eventually au na yeye anakusaliti at the moment , sababu kikawaida mwanadamu huwa anachoka kuvumilia unfairness. (Somehow hamuelewi kwanini usaliti hauishi 😂💔)
 
Mpenzi tu anauma sembuse mume.
Ni kweli ila maumivu hayalingani.Unafikiri kwanini wanasema mke wa mtu sumu na sio mume wa mtu sumu?

Mtu anavaa anajinyima ajili ya mkewe then ukajipigie?Ndo hao wanauliwa na kulawitiwa.Mtu anaumia sana.
 
Mtazamo wake upo sawa tu. Na wa kwako upo sawa pia.

Sio kila mwanamke anaupinga mfumo dume. Na sio kila mwanaume anaukubali.

Nilichogundua haya mambo ya mahusiano hayana msimamo mmoja.
 
 
Nakuona kama mwanamke aliyechanganyikiwa.
Upo radhi kukaa kwenye uozo ili tu uonekane upo kwenye ndoa.
Aisee bro/sista seems kwenye ulimwengu wako halisi una madharau sanaa!

Kupitia maandishi yako kwa mtu makini hapati shida kulijua hilo,unatoa wapi guts za kuandika uliyoandika hapo juu kuhusu muunganiko wa watu wazima wenye akili zao?wewe msafi sana na smart sana au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…