Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Neno NIA ulilotumia hapa litafasiriwe pia kama UTASHI au HIARI. Hakuna Nia/Utashi/Hiari kwenye mkataba.Mpira si biashara ya utumwa. Mchezaji wajibu wake unaambatana na nia ya kutimiza huo wajibu, ukiondoa nia basi ni sawa na huna huyo mchezaji hata kama utalazimisha awepo kikosini. Kuwa na wachezaji 20 wasio na nia ya kuipigania timu ni bora wasiwepo tu. Ni sawa na kufuga mbuzi wafukuze paka wezi wa kuku. Utasema una walinzi ila ni kama huna tu.