Ikiwa Mazishi ni Ibada, basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao

Ikiwa Mazishi ni Ibada, basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao

Uzi mubashara kabisa huu, kiongozi. Umetoa madini yasiyo hubiriwa madhabahuni. Wanaskip sana hizi habari Wakati zinaonekana wazi kwenye vitabu vya Maandiko matakatifu.
Maandiko yako wazi kabisa . Lkn yanapotezewa na kupindishwa
 
Uzi mubashara kabisa huu, kiongozi. Umetoa madini yasiyo hubiriwa madhabahuni. Wanaskip sana hizi habari Wakati zinaonekana wazi kwenye vitabu vya Maandiko matakatifu.
Somo linalofata litaitwa mifupa iliyosahaulika . Niwaeleze jinsi watu wa Mungu walivyokuwa wanaheshimu wafu mababu zao waliotangulia na kwann walifanya hivyo
 
Biblia ni neno la Mungu,na Biblia inasema "Heri WAFU WAFAO katika bwana"

Wewe unasema huwa tunazika maiti,hatuziki wafu....WAFU HAWAFI wafu wanaishi.....
Maelezo yako ya mwanzo yamejikita kuelezea kwamba unaokufa ni mwili,ila nafsi inaishi,,,hivyo WAFU wanaishi.

Paragraph za chini unatilia mkazo,Hakuna haja ya kuhangaika na WAFU,mfu ni mfu haijalishi utamsafisha kiasi gani haitabadilisha ukweli umeshakufa na anaenda kufukiwa na udongo.

Sasa Huoni unaleta mkanganyiko hapo,,, paragraph ya juu ulituambia WAFU HAWAFI, paragraph ya chini unatuambia WAFU WAKIFA WAMEKUFA.....Sasa hapa ndio kwenye mkanganyiko which is which?
 
Kisayansi.
Sayansi ya Lugha(Isimu); mtu akiyekufa huitwa Mfu au marehemu. Wingi wa Mfu ni wafu. Mwili wa marehemu au Mfu ndio huitwa Maiti. Hiyo ni lugha, tukio la mtu Kufa huitwa kifo au mauti.

Sayansi ya mwili, anatomy, physiology na mambo ya utabibu;
Ukisema MTU amekufa, tafsiri yake Hana ajualo, hajui chochote, Hana uwezo wowote ule. Kwani Viungo vyote (organs) na mifumo ya Viungo (organ systems) zote zimekufa, yaani hazifanyi kazi na hazina uwezo tena WA kufanya kazi. Hiyo ndio tafsiri ya Kifo,

Wafu hawawezi kuzikana Kwa sababu Mfu Hana uwezo wa kufanya Jambo lolote.

Kisa cha Lazaro na tajiri sio kisa halisi, Kwa Sisi wataalamu WA Lugha tunaita Metaphor, huwezi tolea reference ya hoja yako Kwa metaphor (tukio ambalo sio halisi). Ni Sawa na Metaphor (kisa au mfano) wa Mpanzi au Msamaria Mwema.

Metaphor ni moja ya vipengele vya Fasihi simulizi. Hivyo Yesu alitumia tuu Fasihi kubuni kisa hicho ambacho sio halisi.

Kisa cha Sauli, ukikisoma Kwa kina na utambuzi, unakuja kugundua kuwa SAULI HAKUMUONA SAMWELI, Ila Yule Mwanamke mchawi ndiye alimuona(alidanganya Kwa sababu wachawi ni waongo) ni kama wanavyofanya wanamazingaombwe au hawa waganga WA kienyeji WA siku hizi au hawa wafufua Misukule. Uongo mtupu.

Sauli alikuwa akiongea na mtu aliyedhani ni Samweli. Lakini hakuongea na Samweli Kwa sababu hakumwona.

Embu soma hizi Aya;
1 Samweli 28
11Ndipo yule mwanamke akauliza, “Je unataka nikupandishie nani?”
Sauli akasema, “Nipandishie Samweli.”
12 Yule mwanamke alipomwona Samweli, alipiga yowe kwa sauti kuu, naye akamuuliza Sauli, “Mbona umenidanganya? Wewe ndiwe Sauli.”
13 Mfalme akamwambia, “Usiogope. Unaona nini?”
Yule mwanamke akasema, “Naona mungu unapanda kutoka ardhini.”
14 Sauli akamuuliza, “Ni mfano wa nini?”
Yule mwanamke akasema, “Ni mwanaume mzee amevaa joho anayepanda.”
Ndipo Sauli akatambua kwamba ni Samweli. Sauli akasujudu kifudifudi, uso wake hadi ardhini.
.”

Yaani Sauli hakumuona MTU yeyote, yeye alidanganywa na Yule Mwanamke mchawi na sio vinginevyo.
Kusema Samweli alifufuliwa ni Uongo mkubwa. Kwa sababu hakuna ushahidi WA Jambo Hilo. Huyo Sauli mwenyewe aliyetaka Kufufuliwa Kwa Samweli hakumuona. Iweje wewe na Mimi tunayesoma tuseme aliyefufuliwa ni Samweli?

Kisa cha Yesu kutokewa na Musa na Eliya bado hakithibitishi kuwa wafu wanaongea au wanaweza kutenda kama Waliohai.
Hapa hoja kuu ni kuwa Eliya inaripotiwa Hakufa alipalizwa Kwa magari ya farasi yenye Moto. Hivyo Eliya sio Mfu yaani Hakufa.

Musa mambo ni 50"50 Ukisema Hakufa ni Sawa Kwa sababu hakuna ushahidi wa kuwa alikufa. Kwani maandiko ya kisa chake yanaonyesha mwili wake haukupatikana Huko Mlimani. Hivyo akitokea MTU akisema Musa Hakufa atakuwa na hoja Kwa sababu hakuna ushahidi WA kifo chake.

Lakini pia akitokea mtu akisema alikufa, sasa huyu hoja zake lazima zisithibitishwe,

Yud 1:9​

Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee"

Aya hii inaweza kutumiwa kama uthibitisho kuwa Musa alikufa lakini haijitoshelezi na inautata mkubwa. Na inajitatiza kulinganisha na miiko ya maandiko.
Kinachogombewa ni mwili wa Musa Wakati huohuo mwili unatakiwa kurudi mavumbini kama kauli ya Mungu ulivyosema.

KITEOLOJIA;
Mtu aliyehai ambaye amemuasi Mungu huyo huitwa MFU, LAKINI sharti awe Hai katika mwili.
Yaani Nafsi yake imekufa lakini yu hai katika mwili. Nafsi unazungumzia ishu ya Attitude, Akili, fikra, upendo, hasira, chuki, n.k. ni vitu visivyoshikika.

Ni Sawa na mwanandoa aliyeoa au kuolewa. Yupo ndani ya Ndoa lakini aseme Moyo wake umekufa, haumpendi tena mumewe au Mkewe. Lakini haimaanishi MTU huyo kafa.

Wafu Hawana ibada Kwa sababu wamekufa.
Umechambua vizuri hoja Yako,ila Mimi natatizwa sana na wewe unapopendaga kubadilisha maandiko na kuassume mambo Yako.
Hapo kwenye kisa Cha sauli Kwa Nini umekazania kusema yule muonaji alimdanganya Sauli?Kwa ufahamu wangu biblia ni kitabu kipo straight sana,kama alimdanganya kingesema pia,wewe huu mpango wa kubadilibadili mambo umekaa vipi?
 
Mnaowasha mishumaa makaburini,

Mnaofanya kumbukumbu ya mfu siku ya arobaini,

Mnaokula nyama msibani acheni,

Jueni kuwa mnafanya IBADA ya wafu.
Nyama msibani inafanyaje?kwani imefanyiwa tambiko lolote?
 
Umechambua vizuri hoja Yako,ila Mimi natatizwa sana na wewe unapopendaga kubadilisha maandiko na kuassume mambo Yako.
Hapo kwenye kisa Cha sauli Kwa Nini umekazania kusema yule muonaji alimdanganya Sauli?Kwa ufahamu wangu biblia ni kitabu kipo straight sana,kama alimdanganya kingesema pia,wewe huu mpango wa kubadilibadili mambo umekaa vipi?

Watibeli hatubadili mambo. Ila tunaweka mambo vile yanavyotakiwa kuwa
 
Somo linalofata litaitwa mifupa iliyosahaulika . Niwaeleze jinsi watu wa Mungu walivyokuwa wanaheshimu wafu mababu zao waliotangulia na kwann walifanya hivyo
Kwa hiyo kama watu wa Mungu,ambao ndio tunaiga mfano kwao walikuwa wanaheshimu wafu mababu zao waliotangulia,Kwa nini sisi unatusisitizia tuachane na mambo Yao?
 
Wakristo someni Biblia,
Mpate kuijua kweli,
Nayo kweli itawaweka huru,
Mtoa mada katoa neno,
Ila linaukakasi,
Mimi binafsi sikubaliani na tafsiri ya mtoa mada.
Umenena vyema sana dada..... wakristo tunatakiwa kusoma neno na kutafakari
 
Back
Top Bottom