Ikiwa Mazishi ni Ibada, basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao

Uzi mubashara kabisa huu, kiongozi. Umetoa madini yasiyo hubiriwa madhabahuni. Wanaskip sana hizi habari Wakati zinaonekana wazi kwenye vitabu vya Maandiko matakatifu.
Maandiko yako wazi kabisa . Lkn yanapotezewa na kupindishwa
 
Uzi mubashara kabisa huu, kiongozi. Umetoa madini yasiyo hubiriwa madhabahuni. Wanaskip sana hizi habari Wakati zinaonekana wazi kwenye vitabu vya Maandiko matakatifu.
Somo linalofata litaitwa mifupa iliyosahaulika . Niwaeleze jinsi watu wa Mungu walivyokuwa wanaheshimu wafu mababu zao waliotangulia na kwann walifanya hivyo
 
Mnaowasha mishumaa makaburini,

Mnaofanya kumbukumbu ya mfu siku ya arobaini,

Mnaokula nyama msibani acheni,

Jueni kuwa mnafanya IBADA ya wafu.
 
Biblia ni neno la Mungu,na Biblia inasema "Heri WAFU WAFAO katika bwana"

Wewe unasema huwa tunazika maiti,hatuziki wafu....WAFU HAWAFI wafu wanaishi.....
Maelezo yako ya mwanzo yamejikita kuelezea kwamba unaokufa ni mwili,ila nafsi inaishi,,,hivyo WAFU wanaishi.

Paragraph za chini unatilia mkazo,Hakuna haja ya kuhangaika na WAFU,mfu ni mfu haijalishi utamsafisha kiasi gani haitabadilisha ukweli umeshakufa na anaenda kufukiwa na udongo.

Sasa Huoni unaleta mkanganyiko hapo,,, paragraph ya juu ulituambia WAFU HAWAFI, paragraph ya chini unatuambia WAFU WAKIFA WAMEKUFA.....Sasa hapa ndio kwenye mkanganyiko which is which?
 
Umechambua vizuri hoja Yako,ila Mimi natatizwa sana na wewe unapopendaga kubadilisha maandiko na kuassume mambo Yako.
Hapo kwenye kisa Cha sauli Kwa Nini umekazania kusema yule muonaji alimdanganya Sauli?Kwa ufahamu wangu biblia ni kitabu kipo straight sana,kama alimdanganya kingesema pia,wewe huu mpango wa kubadilibadili mambo umekaa vipi?
 
Mnaowasha mishumaa makaburini,

Mnaofanya kumbukumbu ya mfu siku ya arobaini,

Mnaokula nyama msibani acheni,

Jueni kuwa mnafanya IBADA ya wafu.
Nyama msibani inafanyaje?kwani imefanyiwa tambiko lolote?
 

Watibeli hatubadili mambo. Ila tunaweka mambo vile yanavyotakiwa kuwa
 
Somo linalofata litaitwa mifupa iliyosahaulika . Niwaeleze jinsi watu wa Mungu walivyokuwa wanaheshimu wafu mababu zao waliotangulia na kwann walifanya hivyo
Kwa hiyo kama watu wa Mungu,ambao ndio tunaiga mfano kwao walikuwa wanaheshimu wafu mababu zao waliotangulia,Kwa nini sisi unatusisitizia tuachane na mambo Yao?
 
Wakristo someni Biblia,
Mpate kuijua kweli,
Nayo kweli itawaweka huru,
Mtoa mada katoa neno,
Ila linaukakasi,
Mimi binafsi sikubaliani na tafsiri ya mtoa mada.
Umenena vyema sana dada..... wakristo tunatakiwa kusoma neno na kutafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…