Ikiwa Mazishi ni Ibada, basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao

Mwl Makungu bado uko baridi ndugu yangu. Umeongea point sana. Ila sijui kwa nini nimekumbuka ndungu Mwl Deo yule Mwl wa Nyamagana aliyefunga. Alikuaga na maandiko fulani.

Sasa kijana naona baada ya siasa kukuvuruga umepata mvurugano wa idol.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Mfano wako wa Musa na Elia si sahihi na pia mfano wako wa Razaro na tajiri pia si sahihi.
 
Ukiangalia kwa umakini utaona Nimezungumzia wafu wa aina . Wafu ambao miili yao iliishazikwa na wafu ambao wako hai kimwili lkn wamekufa ktk utu wao rohoni /nafsini .
Ni Sawa na kusema Wana macho lakini hawaoni; Waacheni vipofu wapotezane njia wenyewe.

Wana masikio lakini hawasikii, waachane viziwi wapigiane kelele wao kwa wao.

Kwa maana hiyo watahubiriwa na kusikia lakini hawataamini, watonyeshwa hadi miujiza lakini hawatasadiki, hivyo basi waacheni wachague njia waliyoichagua kuuiendea. (Hawa wote wameamua kupotezana).

Ni sawa na kuzikana kwa wafu.
 
kwaiyo aliposema mshahara wa dhambi ni mauti ww unasema hapana alikosea kinachokufa n mwil.🤣😇🤣😇
 
Hivi ni vibaya kuongozwa na mawazo ya mfu wa kimwili?
 
Mnaowasha mishumaa makaburini,

Mnaofanya kumbukumbu ya mfu siku ya arobaini,

Mnaokula nyama msibani acheni,

Jueni kuwa mnafanya IBADA ya wafu.
Wanakula vyakula vya ki-agano,Ibada🙌🙌
 
Nyama msibani inafanyaje?kwani imefanyiwa tambiko lolote?
Vyakula vingi vya misibani,40,3...and the like vinakuwaga vimefanyiwa Ibada!
Sio wote ila %kubwa ...hasa upande wa pili!
Jitahidi sn usiwe mlaji wa hivyo vyakula
 
Hizo paragraph 2 za mwisho ndo ilivyo!
Na sijui kwann wachawi wanapenda sn kufanya vituko msibani!

Kumuongezea ,ma inategemea marehemu amekufaje, mfano km kafa Kwa mpango wa Mungu hakuna shida ila km ndo nguvu za Giza zimemuondoa uwe na uhakika roho za kichawi zitatawala msiba
 
Naaam
 
kwa ujinga huu, lazima Kiranga apate nguvu.
Nafsi hai=udongo+pumzi ya Mungu. hivi vitu vikitengana hakuna uhai wala kujua chochote

Mwa 2:7 SUV​

BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
SOMA VIZURI biblia yako ili usituabishe tunaoiamini

Mhubiri 9:5​

Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa, lakini wafu hawajui chochote, hawana tuzo zaidi, hata kumbukumbu yao imesahaulika.

Mhubiri 9:10​

Kila unachotaka kufanya kifanye kwa nguvu zako zote, maana, hakuna kazi, wala wazo, wala maarifa, wala hekima huko kuzimu unakokwenda.
Yale ya tajiri aliyekufa akakutana na tajiri ni mifano tu
Mfano kuna sehemu kwenye hicho kisa inasema yule masikini alikaa kwenye kifua cha Ibrahim, sasa kama masikini wakifa wanakaa kwenye kifua cha Ibrahim ,hicho kifua ni kipana kiasi gani
 
Udongo+pumzi ya Mungu=nafsi hai
vikitengana hivi vitu hakuna kimojawapo kinaweza kusimama peke yake kikiwa hai
Lazaro na Ibrahim was just teaching example , nothing was real
mfano inasema masikini alikuwa kifuani kwa Ibrahim, so wafu wote wanalala vifuani mwa Ibrahim au, ni kipana kiasi gani
Yesu alisema Lazaro amelala, alivoona wanashangaa ,ndo akawaambia amekufa
Kifo ni kama usingizi, ukisinzia hujui chochote
Ukiamini wafu wana nafsi isiyokufa, unajiletea imani ya mizimu. yaani unakaribisha majini yajigeuze wafu yaje yakutishe kuwa ni mfu kakutokea

Chukua hii Wafu hawajui lolote

Mhubiri 9:5​

kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana tuzo tena; maana hata kumbukumbu lao limesahauliwa.
 
Hoja siyo kufufuka Kwa Samweli Bali mtoa hoja anatukumbusha kuwa roho Huwa hazifi bali miili ndiyo hufa
 
Hoja ni kuwa roho haifi bali humrudia Mungu baada ya kutengana na mwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…