Ikiwa Tundu Lissu ameridhia kununuliwa gari ya kifahari na wananchi. Akiwa Rais atafuta manunuzi ya V8?

Ikiwa Tundu Lissu ameridhia kununuliwa gari ya kifahari na wananchi. Akiwa Rais atafuta manunuzi ya V8?

Suijaona hoja hata moja; kuyafanya maswala makuu ya nchi hii kuelezwa kwa mfano 'abstract' kama huu unao uweka mbele kuwa kielelezo.
Kuna mwanafunzi mmoja baada ya kusoma matokeo ya mtihani wake, akaona amepata 49.05, Kwa kuwa palikuwa na chance ya kukata rufaa,

Akalipia rufaa Ili mtihani wake urudiwe kusahihishwa mbele ya Lecture yule,

Sasa siku ilipofika, mtihani ukaletwa usahihishaji ukarudiwa UPYA,

Mwalimu yule wa kihaya aliyejulikana Kwa Jina la Bishagazwe akasahihisha na kurudia marks zile zile 49.05,

Sasa mwanafunzi yule akalia sana na kumwomba mwalimu atafute namna ya kujaza 0.5 Ili achomoke kwenye mtihani Ule akidai jambo lile liko chini ya uwezo wake.

Mwalimu yule akatulia Kwa muda Kisha akampa pole sana mwanafunzi yule, na mwanafunzi yule aliporudi katika Hali ya kuchangamka akiamini mwalimu amemuelewa, haya ndiyo majibu ya mwisho ya mwalimu.

Mwalimu alimjibu, nasikitika sana na ningependa nikusaidie mwanangu, ila Sina pa kuitoa hiyo 0.5, na haipo namna ingine zaidi ya kurudia mwaka Kwa SoMo hili Moja.

......mwisho wa simulizi.....

Sasa Kalamu umeamua kabisa kutoona HOJA yoyote ilhali mwanzoni uliniuliza nini Hasa Nia ya kuandika thread hii🤔
 
Bora uchangiwe ununuliwe kuliko utumie nguvu ya uongozi wako kununua kwa makusudi wakati watu wako wanateseka
 
Hata kummuliza Lissu ikiwa atakuwa Rais ataanza na mchakato wa Katiba mpya pia ni udhaifu,

Maana pia hiyo haiko mikononi mwake, Katiba mpya ni takwa la wananchi.

Kuhusu V8 tunataka kauli yake na chama chake
Ili akumbushwe.

Karibu 🙏
Magufuli alisema katiba mpya sio kipaumbele chake. Hata Samia mwanzoni alisema katiba isubiri kwanza. Hivi sasa hii nchi inaendeshwa kwa presidential prerogatives na decrees. Suala la kuwa katiba mpya ni takwa la wananchi halijawa na maana kabisa hadi sasa.

CHADEMA wamesisitiza wakiingia madarakani katiba mpya ndio itakuwa ajenda yao namba moja. Wanadai wanataka kurekebisha mfumo mzima wa utawala wa nchi. Wanaweza kabisa kupuuza na wasifanywe kitu katika haya mazingira ya banana republic.

Sasa wewe mkuu unataka tusumbuke na hisia za Lissu kuhusu ma-V8? Badala ya hatua za uhakika za kudhibiti hilo? Unataka kusikia tu kauli yake? Kama ile ya “maendeleo hayana chama”?

Kama Lissu akiwa madarakani na bado akawa na uwezo wa kuongoza nchi kwa presidential decrees & prerogatives badala ya yale sisi tunayotaka atakuwa hatufai!
 
Jawabu lipo ndani ya swali lako.
Wananchi kuamua wenyewe kwa hiari yao kununua kitu fulani ni tofauti na wananchi hao kuamuliwa na viongozi wao (hasa kwenye vitu wasivyoviridhia).
 
Kuna mwanafunzi mmoja baada ya kusoma matokeo ya mtihani wake, akaona amepata 49.05, Kwa kuwa palikuwa na chance ya kukata rufaa,

Akalipia rufaa Ili mtihani wake urudiwe kusahihishwa mbele ya Lecture yule,

Sasa siku ilipofika, mtihani ukaletwa usahihishaji ukarudiwa UPYA,

Mwalimu yule wa kihaya aliyejulikana Kwa Jina la Bishagazwe akasahihisha na kurudia marks zile zile 49.05,

Sasa mwanafunzi yule akalia sana na kumwomba mwalimu atafute namna ya kujaza 0.5 Ili achomoke kwenye mtihani Ule akidai jambo lile liko chini ya uwezo wake.

Mwalimu yule akatulia Kwa muda Kisha akampa pole sana mwanafunzi yule, na mwanafunzi yule aliporudi katika Hali ya kuchangamka akiamini mwalimu amemuelewa, haya ndiyo majibu ya mwisho ya mwalimu.

Mwalimu alimjibu, nasikitika sana na ningependa nikusaidie mwanangu, ila Sina pa kuitoa hiyo 0.5, na haipo namna ingine zaidi ya kurudia mwaka Kwa SoMo hili Moja.

......mwisho wa simulizi.....

Sasa Kalamu umeamua kabisa kutoona HOJA yoyote ilhali mwanzoni uliniuliza nini Hasa Nia ya kuandika thread hii🤔
Hiyo hadithi uliyo eleza hapo haina tofauti yoyote na mada uliyo weka hapa mkuu 'Rabbon'. Utanisamehe sana kama huelewi ninacho lenga mimi.

Hizi hadithi ni 'superficial' kama ilivyo mada yenyewe.

Utaanzia wapi ku'extrapolate' habari ya kiongozi kuchangiwa gari, kwa hiari ya wachangaji wenyewe, tena asio wajuwa, na wala wao bila ya kutaka upendeleo maalum toka kwa kiongozi huyo, ambaye hata haijulikani kama safari zake za kisiasa zitamfikisha wapi!

Sasa wewe naomba unieleze unavyo ujuwa uadilifu wa hawa viongozi; kwa mfano huyu tuliye naye sasa hivi' ulijuwa kuwa atakuwa ni kokoro la uchafu unaoonekana sasa hivi?

Kuna vipimo vingi sana vya kujua mwelekeo wa kiongozi hata kabla haja shika madaraka. Ukizungumzia dalili hizo kwa Tundu Lissu, nami nitaungana nawe kujadili "hoja" hizo kwa umakini mkubwa zaidi ya hii unayoona wewe ndiyo hoja.

BTW: hiyo stori yako ya huyo mwanafunzi na mwalimu. Hukutakiwa umpe jukumu hilo mwalimu huyo huyo kusahihisha hiyo karatasi ya mwanafunzi kama kweli ulitaka haki ifanyike
Hata kama mtihani huo ungekuwa ni katika mtindo wa 'multiple choice', bado kungekuwa na fursa tele za kuipata hiyo 0.5 iliyo kosekana na mwanafunzi kuendelea na shule yake.
Naelewa jinsi shule zetu zilivyo kwa kufanya walimu kuwa kama miungu mbele za wanafunzi; hali ambayo ni tofauti sana na kwingineko duniani.
Bila shaka utakuwa umenielewa vizuri.
 
CHADEMA wamesisitiza wakiingia madarakani katiba mpya ndio itakuwa ajenda yao namba moja. Wanadai wanataka kurekebisha mfumo mzima wa utawala wa nchi. Wanaweza kabisa kupuuza na wasifanywe kitu katika haya mazingira ya banana republic.
Binafsi naamini kwamba fursa ya kutengeneza Katiba Mpya, ambayo ushiriki wa wananchi utapewa kipaumbele ndiyo hasa utakuwa msingi wa "kubadili mfumo mzima wa utawala wa nchi". Sijui kama itakuwa ni sahihi kwa chama cha siasa tena kama CHADEMA kulifanya jambo hilo.
Vinginevyo, CHADEMA wanaweza wakajikuta katiuka malalamiko yale yale yanayo elekezwa kwa CCM sasa hivi.
 
Maana yake mchakato kamili unaoshirikisha wananchi na wawakilishi wao kikamilifu lazima uhusishwe. Serikali itakuwa muwezeshaji tu na si muamuzi.

Serikali ya sasa haitaki kuwezesha; tena inazuia mchakato usifanyike.
 
Salaam, Shalom!!

Naomba majibu yawe mafupi na yaliyoshiba HOJA, vyama tuweke pembeni.

NB: Swali gumu linahitaji jibu gumu! Swali jepesi lijibiwe pia kiuwepesi!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏.
Ile pesa alikula yote
Kwasasa hana gari na pesa hana
 
Salaam, Shalom!!

Naomba majibu yawe mafupi na yaliyoshiba HOJA, vyama tuweke pembeni.

NB: Swali gumu linahitaji jibu gumu! Swali jepesi lijibiwe pia kiuwepesi!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏.
Makonda acha maneno maneno yako
 
Back
Top Bottom